Nawaunga Mkono Madaktari

Nawaunga Mkono Madaktari

Mbona unafanya kazi nzuri tu keep doing. Huitaji kuwashawishi wanchi unahitaji kuitaka serikali kuvunja hiyo MoU. Tatizo nikuwa huoni serikali ndiyo inahusika na yote mawili -la MoU na la madaktari.
Hii hataweza kujibu.

@Topical, ukigusia tena hii issue sehemu yoyote kabla ya kujibu hii basi utajitoa nishai mwenyewe, kwasababu namimi ntakueleza the same thing na sidhani kama utaweza kujibu.
 
WAZIRI MKUU UNAVYOMALIZANA NA MADKTARI WETU USISAHA KWAMBA NA WAALIMU TUKO HAPA MLANGONI TUNASUBIRI KUJA NDANI MWAKO HAPO KUPEWA CHETU

Waziri Mkuu, kuondoa tu mtu kwenye cheo chake kisha kesho unampa kazi ya ubalozini wala haitusaidi kitu chochote hapa. Nasema mawazo ya kitu gani kifanyike ni hayo hapo chini kwa faida ya mustakabali na ustawi mzuri wa taifa letu.

Pia usisahau kukamilisha mambo ya walimu wetu hapa hapa kesh kesh maana usiombe wale wakigoma nchi hii tumekwisha kwa kuwa wako hadi katika ngazi ya kila kijiji wa nchi hii.

Nasema usiombe waalimu wakimwaga sumu huko kote vijijini utasikia hadi zile 'gala za kura za maruani za CCM' huko vijijini nazo zimechomwa moto sasa sijui Wa-Kijani itakuaje hadi hapo!!!!! Enyi viongozi wetu wa upinzani, kama CCM wao bado hawalioni hatari kubwa hii walimu wakigoma kote nchini - kawakumbusheni juu ya hilo!

WaTanzania tusisahau kwamba lugha pekee wanayoielewa hii serikali ya Pinda na Kikwete ni lugha ya Migomo na Maandamano tuuuuuuuuuu!! Hivyo kila chama cha upinzani nayo ielewe hilo juu ya jinsi gani ya kufanya mawasiliano na serikali ya CCM mkaelewana.

MAFISADI kutuibia koote kule serikalini na kuendelea tu kubadilishiwa vyeo hapa na pale na sisi kugeuzwa mazezeta yote ni kutokana na ukweli kwamba lugha murua wa kuwasiliana na serikali hii iliojaa watu wenye KIBURI CHA KOBE hatukuifahamu hata tone. Na huo ndio ukweli wa mambo.

Serikari ya CCM, mdharau mwiba miguu huota ...?


Madaktari wetu wasikilizwe kwa kina, mfumo wa sekta ya afya na utibabu ufumuliwe haraka kwa faida ya wadau wake.

Hivyo, na posho za bwerere kwa walaghai wa wananchi kule bungeni wapewe manesi wetu pamoja na walimu ambao wanafanya kazi katika mazingira magumu mno kututumikia sisi jamii ya Tanzania.
 
Serikali imefanya miscalculation kubwa sana ya kutoelewa hisia za taifa. Walifikiria kuwa wananchi watawakasirikia madaktari na madaktari watapoteza support. So far, overwhemingly wananchi wako na madaktari! It just make sense!
Serikali wame miscalculate kweli kweli mgomo wa drs.....na ndio sababu wamechelewesha kukaa nao huku wakisubiri support ya wananchi/wagonjwa....pia wakitanguliza vitisho(kama walivyozoea)......sasa nadhani serikali wametambua tabia ya kudanganya wananchi mwisho wake unafika sasa.....this is a very big lesson to them.Wananchi wanaelewa ili watibiwwe vizuri lazima madaktari wawe wametulia na pia mazingira ya utoaji huduma lazima yawe mazuri...this is natural....hapa hakuna cha maskini wala tajiri....kila mtu angependa atibiwe vizuri....hakuna maskini anaependa kutibiwa akiwa amelala chini(hata kama kwake analala chini)au wamama kujifungua na kulala chini(e.g nenda temeke hospital..its so bad there) au mgonjwa kutibiwa na daktari ambaye ana frustrations/stress za maisha kutokana na matatizo ya nyumba au usafiri wa kumfikisha kazini........all these basic needs for doctors/patients have made a very good sense to the whole strike saga..and hence a very good justification for the whole cause.......
 
Samahani...nadandia treni kwa mbele...! Mkuu hii ya 40,000 kumuona daktari umeshaisema mara nyingi na kama kumbukumbu zangu hazijakosea ulishawahi kusema pia kuna wakati mlishindwa kumlipia mgonjwa wenu kwenye hizi hospitali zinazopokea ruzuku ikabdi mumpeleke India... Hivi hauwezi kweli kutuambia jina la hiyo hospitali? Ni hilo tu.
- Mkuu sielewi nia yako lakini kama nisemavyo sina Unafiki, nitasema kweli daima uongo kwangu ni mwiko..

kuna kesi mbili hapa tofauti, ipo ile ya kwenda India (Apollo) ambayo tulianza na KCMC na ipo ya mdogo wangu kutibiwa Muhimbili ambayo tulilipa Tsh 40,000 kumwona Daktari baada ya kupata vipimo toka kwa daktari mwingine mhindi ni kilema yuko Upanga kwa Tsh 80,000 kisha akafanyiwa Operation ndogo kwa Tsh 600,000 lakini bado hajapona. Tumefanya tena vipimo kujaribu kutazama haswa kinachosmbua ni kitu gani maana miaka mingi sasa.

Ningeungana sana na madaktari kama madai yao yangekuwa dhidi ya serikali na hayahatarishi maisha ya wananchi. Unagoma kudai haki yako bila kuathiri sheria nyingine, ndivyo sheria zilivyo tungwa kwa kutazama uzito wa swala. Kenya wamewahi kufanya mgomo lakini waliweza kuendelea kutibia wananchi wenye ulazima wa kupata matibabu..
Yes, yawezekana kabisa madai ya hawa madaktari yakawa na msingi lakini unapomtumia mwananchi kama humanshield ktk vita baina yako na serikali hapo mkuu wangu sintokubaliana nao kabisa acha mbali najua fika hakuna daktari bingwa nchini mwenye maisha mabaya - hakuna!..

Madaktari wanazo njia nyingi sana ambazo ni haramu ktk viapo vya Udaktari lakini zimehalalishwa nchini kutokana na Azimio la Zanzibar. Mtu kasomeshwa bure kwa gharama zaidi ya Usd 120,000 na kodi za wananchi, anapewa nyumba, maji na umeme bure bado wanaweka madai kwa sababu ya wajinga wengine WABUNGE ambao nao ati wanajiita wasomi wanalishwa bure na kodi za wananchi bila hata aibu wanajitapa kwamba wao ndio serikali (wabunge ndio mawaziri). Yaani mfumo mzima wa RUKSA ndio sababu kubwa ya migogoro na nchi yetu kuingia bondeni tukakwama. Na kwa ujinga ule ule wa Ruksa, tunabishana sana juu ya viti , nauli zetu na dereva awe nani badala ya kutazama tutaliondoa vipi gari letu toka ktk shimo hili tulokwama. Usafiri ni gari sio maisha ya kila mtu wakati hatuwezi tembea kwa miguu kwenda tunakotaka.

Hii nchi kweli inatawalika au ndio akili za wasomi wetu.
 
W/M Pinda amekuwa na tabia ya kusema vitu ambavyo hafatilii utekelezaji wake baadae.
Kwa hili nawapongeza madaktari kwa msimamo wao na kwa kufatilia maazimio yalomaliza mgomo wa awali.
Kwa upande mwingine msimamo huo wa madaktari utakuwa fundisho zuri kwa serikali na watendaji wake ili wawe makini na wahaidi yanayotekelezeka tu na sio kutoa ahadi zisizotekelezeka ili wapigiwe makofi.
 
hivi kuwaondoa mponda na nkya inahitaji bajeti kiasi gani?ni upuuzi kuwasimamisha watendaji wakuu wizarani halafu ukaogopa kuwawajibisha wanasiasa!
 
hii serikali inakera sana!
Madaktari Aluta Continuaa, gomeni mpaka mwisho, wananchi tuko nyuma yenu
 
Siungi mkono kugoma madaktari, huyo pinda na hao viranja wa madaktari kwny huo mgomo zaidi hapo naona ni siasa imetawala.....lakini ukipelekwa mahospitalini tht time mgomo ume'cotton fire' ndio utajua madhara yake.
Unaunga mkono mgomo huu kwa kuwa sasahv uko kwny laptop unabofya, huumwi wala huna ndugu au jamaa wa karibu anayehitaji uwepo wako angalau wa kumfariji tu....
Just imagine mkeo yuko leba anakaribia kujifugua, uchungu umemshika....labda njia ndogo hatoweza kujifungua kwa njia ya kawaida at the same time ana Low Blood Pressure hivyo hata ikilazimu aongezwe njia lakini hawezi kupush option pekee ni Operation,Ndio mtoto wa kwanza huna uwezo kifedha na madaktari ndio wanagoma. Utafanyaje?
 
hivi kuwaondoa mponda na nkya inahitaji bajeti kiasi gani?ni upuuzi kuwasimamisha watendaji wakuu wizarani halafu ukaogopa kuwawajibisha wanasiasa!

Jack your always straight, keet it up.
 
W/M Pinda amekuwa na tabia ya kusema vitu ambavyo hafatilii utekelezaji wake baadae.
Kwa hili nawapongeza madaktari kwa msimamo wao na kwa kufatilia maazimio yalomaliza mgomo wa awali.
Kwa upande mwingine msimamo huo wa madaktari utakuwa fundisho zuri kwa serikali na watendaji wake ili wawe makini na wahaidi yanayotekelezeka tu na sio kutoa ahadi zisizotekelezeka ili wapigiwe makofi.

Kuondolewa kwa Waziri na Naibu wake = kutekelezwa kwa madai ya madakitari.
 
Pinda ni mtoto wa mkulima asiye mkulima...nadhani ni mtoto wa mkulima aliyekulia mjini.
 
Pinda ni mtoto wa mkulima asiye mkulima...nadhani ni mtoto wa mkulima aliyekulia mjini.

ni mmoja kati ya walaghai hapa mjini. Amekutana na watu ambao wanahitaji jibu la 1+1 iwe 2 na siyo 1+1 jibu 11. Hii nchi tutafika tu,hata kwa kuwa na makovu mpaka kwenye moyo lakini tutafikishana tu. Wamezoea kutupelekesha kama madebe matupu sasa hivi yamejaa mavi!
 
Madktari gomeni kuanzia leo ;nawaunga mkono mia kwa mia na jk nenda ulaya kale bata baba sisi tutagoma mpaka kieleweke
 
Umenena vyema sana, wananchi ni jukumu letu kuwaunga mkono ma dr katika kudai ubireshwaji wa sekta ya afya maana inatuhusu sisi sote
 
mwanakijiji unaunga mkono madaktari kwa sababu wewe upo nje ya nchi huathiriki wewe wala ndugu yako na adha tunayopata sisi watanzania maskini.
 
kuunga mkono mgomo wa madaktari ni sawa na kuunga mkono vifo vya watanzania maskini.hii ni aibu kwa mtu mwenye akili timamu
 
Pumbafu wewe... umejaaa udini tuuu pasipo kujua unachoandika... Yaani nia yako ilikuwa kuuponda ukristo na mfumo wa kikrustu uliokuwepo kisa wakoloni wa kijerumani walikuwa wakristo... Hujui kama na waarabu walitawala... wao wameacha nini ambacho kinaonekana??

Wameacha shule ngapi au hospitali ngapi.... iwe Znz au Bara... Acha uzuzu kabisa... Na by the way hospitali za missionary si lazima ziwe za wakristu hata waislam wanazo... ni charitable institutions, mwehu wewe..
Mkuu umeifanya jumapili yangu ya leo iwe mwanana
 
Tunawaunga mkono madaktari kwa madai yao lakini pia hatutawaunga mkono kwa hatua kali za mgomo ambao utaathiri sehemu kubwa ya huduma za AFYA nchini. Safari hii mkigoma jaribuni sana kuhakikisha huduma zile muhimu Emergency zinaendelea kufanya kazi na punguzo lilwe ktk huduma zinginezo na zifikie pungufu la isiyozidi asilimia 30 au 40 ambayo nina hakika impact yake inatosha kabisa kuwasukuma viongozi wetu kufikiria Upya.

Isipokuwa nanyi kumbukeni kwamba sisi wananchi hatukubalini na swala la Posho, na kama mishahara iongezwe basi iongezwe sehemu zote kulingana na maisha kwa sababu hakuna nafuu kwetu sisi iikiwa nyie mtaongezewa mishahara lakini manesi na wahudumu wengine wasipate ongezeko. Hawa ndio tunakutana nao kabla yenu ktk mapokezi na hawa ndio watakao tuomba rushwa na kadhalika maana maisha magumu hayapo kwenu tu. Posho zote zikatwe isipokuwa zile ambazo zinatokana na huduma za Hospital nje ya makazi yenu na ambazo mtatakiwa kuwakilisha stakabadhi za matumizi yake ofisini mkirudi.

Jambo jingine, pamoja na kukubaliwa matakwa yenu, nanyi mkubali kupoteza baadhi ya incentive mnazopewa ikiwa ni pamoja na ku operate Private Hospitals isipokuwa mnaweza kufungua Phamacies.. Ongezeko la mshahara lazima liambatane na ufanisi wa kazi pamoja na muda wetu kutumika zaidi ktk Hospital za serikali na sio ku refer wagonjwa ktk hospital zenu binafsi ambako wagonjwa huwa treated on private terms.
 
Kweli kabisa ukitokea mgomo mwingine halafu watu wakaanza kulia "madaktari" badala ya "kikwete" tutakuwa ni watu wa ajabu kweli kweli!
 
Back
Top Bottom