Nawaunga Mkono Madaktari

Nawaunga Mkono Madaktari

Mkuu usipofushwe na msimamo wako wa kiimani hadi ushindwe kufikiria. Hospitali za tanzania zina milkiwa na makundi matatu
1. Serkali
2. Non profit organizations e.g msikiti, kanisa, NGO
3. Private eg Agakhan, Hindu mandal, buruani, TMJ, THI, etc

Serkali haina hospitali za kutosha kutibu wananchi wake wala kusomesha vijana wake wanaotaka kujiunga na taasisi za utibabu na uuguzi. Ili kuendeleza huduma hizo serkali ilitafuta alternative ambayo ni kutumia facilities za non profit organizations. Miaka ya nyuma serkali ilifanya ubabe ikazitaifisha na kujipachika illegal ownership.

Baada ya serkali kushindwa kuziendesha ilizirudisha kwa wamilki halali zikiwa katika hali mbaya. Kwa hali ya kawaida serkali ilitakiwa kulipa compensation au basi ijitegemee kwenye hii huduma ya afya lakini bahati mbaya serkali haikufanya chochote kati ya hayo na badala yake bado inawategemea walewale iliyowadhulumu.
Sasa serkali inawajibu wa kutoa huduma za afya kwa jamii lakini haina facilities za kutosha, je ni nani anaemtegemea mwenzake hapa? kanisa au serkali?

Mkandara nakushauri uonane na mbunge wako ili utoe malalamiko yako kwa serkali yako na uiulize ina mpango gani wa kujitegemea kwenye huduma za afya badala ya kutogemea facilities za kanisa
Hospitali za kanisa zitaendelea kufanya kazi za kutoa huduma kwa walengwa bila millioni 90 za serkali ya magamba kwa sababu wao ni non profit making organizations, tena serkali ikiacha kupeleka wagonjwa wake huko ndo huduma zitakuwa bora zaidi kwani wahudumiwa watapungua

Thubutu, bila 90 bilions hata kujenga wasingejenga mkuu unaweza kuwadanganya watoto wadogo, besides majengo mengi yalijenga wakati na serikali ya kikoloni ambayo ilikuwa inaendeshwa kikristo; hivyo walipata fedha za serikali toka enzi za utawala wakoloni (fedha za umma)

Waliposhindwa kuzi-maintain ndio wakafanya lobbying kuibia serikali, sasa badala hata ya kuboresha huduma wamenogwa na ufisadi hawana tofauti na serikali ..nafikiri wanashirikiana katika kuiba..
 
Serikali kushindwa ilitokea lini na hiyo research ya alternative ilifanywa lini na kupitia vyombo gani maana bungeni haikupita sasa wewe nambie maamuzi haya yalifikiwa vipi na wakati gani maana nakumbuka wakati wa Nyerere tulikuwa hatuna Hospital kabisa zaidi ya zile za kanisa na bado tulipewa huduma vizuri bila madaktari kugoma...
 
Kanisa lina lawama kubwa kwakuwa wanapewa 90bil kila mwaka kuboresha hospitali za bugando, KCMC, etc lakini inavyoonekana hawakutumia kuboresha huduma hizi ..wamezifisadi..kama kawaida

Serikali ina lawama kubwa kwakuwa imeshindwa a. kuwafuatilia kanisa wasile hizo fedha za umma, b. kushindwa kubersha hospitali zake..

Utaona kuna tatizo letu ni a. Serikali kwa kushirikiana na kanisa katika kutunyonya na kutunyonga..wananchi wanatakiwa watambue hilo

Ni Tanzania pekee katika hii dunia ndio sehemu ambako watu ni wajinga na bado ujinga wao kwao ukawa ni jambo la fahari mbele za watu wengine. Muwe mnatembea mjionee wenyewe. Maneno ya kuambiwa na mtu ambaye hajasoma, hajui kitu ni sumu. Kama vigezo vya uongozi ktk imani zenu vitabakia kufuga ndevu chafu za hudhurungi, kuvaa makubazi na suruali njiwa bila kuzingatia elimu, basi kamwe hamtabadilika.

Kama una nia ya kufahamu, nenda Teule Hospital pale Muheza, halafu fanya uchunguzi wa kiwango cha huduma, nani anasimamia mapato na matumizi, gharama za matibabu ni kiasi gani na matibabu hutolewa kwa nani, halafu tuone kama ukirudi bado utakuwa unapinga MoU!

Ushauri wangu kwa wanaJF wote: Tuwe makini na ushauri na maagizo tunayopewa na mtu/watu wasio na elimu na ufahamu wa maarifa ya dunia. Wenye umri kidogo mtakubaliana na mimi kuwa zamani gari la Msalaba Mwekundu (RED CROSS) lilistahili kukimbiwa kwa kuwa kutokana na simulizi za wazee wetu ambao hawakuwa na elimu na ufahamu juu ya shughuli za Red Cross, tuliambiwa hao ni WANYONYA DAMU a.k.a MUMIANI. Si ajabu leo kuona kuna watu na akili zao wanaielezea MoU kwa mtindo ule ule tulioelezewa kuhusu Red Cross. Je turudie ujinga wa miaka ya 80?

MoU ni jambo lililofanyika kwa akili na sio kwa hisia. Nitaendelea kusisitiza kuwa, ukiishi buguruni na kutibiwa fungus zako AMANA kamwe huwezi jua umuhimu wa MoU, ukitaka kuujua katibiwe MUHEZA (Teule Hospital), Ndanda Mission, n.k

Watanzania tuwe na utashi wa kutumia akili zetu bila shuruti.
 
Kuna mtu aliwahi kuniambia kuna matatizo 10 ambayo yapo kwa binadamu hayakwepeki, lakini la 11 ni la kujitakia, sasa naanza kuamini alichoniambia.
Hata mimi alinambia hivyo hivyo lakini lile la kwanza ndio unalo na hulikubali ingawa limekuganda kama luba.
 
Serikali kushindwa ilitokea lini na hiyo research ya alternative ilifanywa lini na kupitia vyombo gani maana bungeni haikupita sasa wewe nambie maamuzi haya yalifikiwa vipi na wakati gani maana nakumbuka wakati wa Nyerere tulikuwa hatuna Hospital kabisa zaidi ya zile za kanisa na bado tulipewa huduma vizuri bila madaktari kugoma...

Maamuzi ya serikali kunyang'anya hospitali na shule za taasisi za dini yalifanywa na bunge gani? Ukitumia akili kidogo utagundua idadi ya watu wkt wa Nyerere na sasa ni tofauti kwa asilimia kubwa. Na nashukuru kuwa unatambua kuwa Hospitali zilikuwa za kanisa tu, na sio misikiti.
 
Thubutu, bila 90 bilions hata kujenga wasingejenga mkuu unaweza kuwadanganya watoto wadogo, besides majengo mengi yalijenga wakati na serikali ya kikoloni ambayo ilikuwa inaendeshwa kikristo; hivyo walipata fedha za serikali toka enzi za utawala wakoloni (fedha za umma)

Waliposhindwa kuzi-maintain ndio wakafanya lobbying kuibia serikali, sasa badala hata ya kuboresha huduma wamenogwa na ufisadi hawana tofauti na serikali ..nafikiri wanashirikiana katika kuiba..

Inaonesha kati ya hawa wakoloni waliopata kuwepo East Afrika, Muarabu tu ndie alikuwa mwema. Yeye hakuiba fedha kujenga shule wala hospitali, alishushiwa tu fedha na allah akajenga misikiti Kilwa, Bagamoyo na Mtwara. Natumaini mwarabu angetawala zaidi, Tanzania ingekuwa na maendeleo kama Saudia Arabia, na hakika tusingekuwa tunasaidiwa tende mwezi mtufuku
 
Ni Tanzania pekee katika hii dunia ndio sehemu ambako watu ni wajinga na bado ujinga wao kwao ukawa ni jambo la fahari mbele za watu wengine. Muwe mnatembea mjionee wenyewe. Maneno ya kuambiwa na mtu ambaye hajasoma, hajui kitu ni sumu. Kama vigezo vya uongozi ktk imani zenu vitabakia kufuga ndevu chafu za hudhurungi, kuvaa makubazi na suruali njiwa bila kuzingatia elimu, basi kamwe hamtabadilika.

Kama una nia ya kufahamu, nenda Teule Hospital pale Muheza, halafu fanya uchunguzi wa kiwango cha huduma, nani anasimamia mapato na matumizi, gharama za matibabu ni kiasi gani na matibabu hutolewa kwa nani, halafu tuone kama ukirudi bado utakuwa unapinga MoU!

Ushauri wangu kwa wanaJF wote: Tuwe makini na ushauri na maagizo tunayopewa na mtu/watu wasio na elimu na ufahamu wa maarifa ya dunia. Wenye umri kidogo mtakubaliana na mimi kuwa zamani gari la Msalaba Mwekundu (RED CROSS) lilistahili kukimbiwa kwa kuwa kutokana na simulizi za wazee wetu ambao hawakuwa na elimu na ufahamu juu ya shughuli za Red Cross, tuliambiwa hao ni WANYONYA DAMU a.k.a MUMIANI. Si ajabu leo kuona kuna watu na akili zao wanaielezea MoU kwa mtindo ule ule tulioelezewa kuhusu Red Cross. Je turudie ujinga wa miaka ya 80?

MoU ni jambo lililofanyika kwa akili na sio kwa hisia. Nitaendelea kusisitiza kuwa, ukiishi buguruni na kutibiwa fungus zako AMANA kamwe huwezi jua umuhimu wa MoU, ukitaka kuujua katibiwe MUHEZA (Teule Hospital), Ndanda Mission, n.k

Watanzania tuwe na utashi wa kutumia akili zetu bila shuruti.
Utayasema yote lakini kwa sababu wewe ni kizazi kipya hutaelewa. Zamani enzi za mkoloni, wazazi wetu walikuwa wakitolewa damu na wakoloni walitumia magari haya kwenda vijijini kukusanya damu..Hivyo ukweli upo kwamba Red cross walienda vijijini na kutaka wananchi wajitolee damu na kama ujuavyo mwafrika hatoi damu yake hovyo..Kwa hiyo kulikuwa na ukweli kwamba magari ya Red coss yalikuwa yakutumika zaidi kutafuta damu za watu badala ya kupeleka wagonjwa Hospitalini. nia njema lakini walikuwa mumiani kweli..Iwe akili ya wazee wetu au upendavyo ilitokea hivyo.

Hili swala la MoU sii la kujitolea na wala hata kama sina elimu halifai hata kwa kulumanga kuona serikali ikiingia ubia na kanisa kuendeleza huduma hizi. Tuna fail kwa sababu na kama tulivyo fail ktk Ujamaa zilikuwepo sababu ambazo wengi hatuzikubali lakini ndio ukweli kwamba serikali ilimiliki nguzo zote za uzalishaji na huduma japokuwa kulikuwepo na Private Hospital na shule. Sisi tunatazama source ya matatizo ya Afya na Elimu nchini leo hii na kama serikali inahusika basi vile vile CSSC inahusika pia... mengineyo jaza mwenyewe.
 
Sasa kama halina shida ya fedha hizi mnachokililia hapa kitu gani.. Kina nani serikali ilisema imeshindwa kuwahudumia? nambieni nani alosema hivyo? hamtaki mnabakia kutunga maneno tu.. Lini serikali ilitangaza kushindwa kuwahudumia wananchi ktk Afya na ELimu kama sio kamba zenu..Nasema hivi ruzuku zifutwe na serikali ichukue jukumu hilo peke yake aiachane na maswala la kanisa yabakie kanisani..Nilitegemea wewe mwenye akili za binadamu utaelewa sawa kabisa na kujiunga nami maana kanisa linajiweza kabisa na hilo nalijua sana..

Hii ndio sababu nasema serikali haina sababu ya kutoa ruzuku ikiwa wananchi tunatozwa gharama kubwa. Acha za kanisa ziwe private tutatia akili, na wengine tunajibanza humo humo ktk hospitali za kata kama zitajengwa. Maana sasa hivi hatujui jukumu ni la nani maana CSSC hupewa fedha na mahesabu yao hatutakiwi kujua wanazitumia vipi..wee tukana weee utachoka tu mimi nakuja na hoja!

Tunacholilia wapi? Hivi hiki ni kilio cha wakristo au cha madaktari? Kama unamaanisha madaktari wa Bugando, KCMC, TEULE n.k basi huo ndio ule uelewa mdogo unaokusumbua. Wale wanaripoti kwa serikali na sio kwa kanisa, usiwe mvivu wa kufikiri. Nenda kule Ubungo Kibangu, kuna Hospitali pale ya kanisa (imejengwa na inamilikiwa na kanisa) nenda ukatazame je madaktari pale wamegoma?

Shida yenu ni elimu tu, nitawakumbusha hili kila mara. Na ndio maana unaongea maneno ya kujikaanga mwenyewe. Kama nia yako ulitaka kuelezea ni jinsi gani kanisa limeshindwa kuwalipa madaktari BUGANDO, KCMC, TEULE n.k mpk wameamua kugoma, jibu ni kuwa wanafanya kazi chini ya serikali na ndio maana wameigomea serikali na hawakuligomea kanisa. Udini unakufanya huoni facts
 
Hivi kabla ya mgomo wagonjwa walikuwa wanapata huduma nzuri na watu walikuwa hawafi kwa sababu walikuwa wanapewa huduma nzuri mahospitalini?

Watu walikuwa wanakufa na pia walikuwa hawapewi huduma nzuri lakini kwa mgomo huu huduma zimesitishwa na vifo vitaongezeka zaidi,kila mtanzania ana haki ya kuishi hivyo serikali ishugulikie swala la madaktari ili kuwapa wananchi wake haki ya kuishi.
kuhusu swala la kubinafsisha sekta ya afya ama kuwa na shares na makanisa ama misikiti sidhani kwamba ni suluisho kwani kiukweli ni kwamba huduma za afya zitakuwa juu kwa maana ya gharama.Tunaitaji reformation ya viongozi wetu na nam
 
Maamuzi ya serikali kunyang'anya hospitali na shule za taasisi za dini yalifanywa na bunge gani? Ukitumia akili kidogo utagundua idadi ya watu wkt wa Nyerere na sasa ni tofauti kwa asilimia kubwa. Na nashukuru kuwa unatambua kuwa Hospitali zilikuwa za kanisa tu, na sio misikiti.
Wewe unafikiri Nyerere aliamka asubuhi na kutangaza Azimio la Arusha? Mkuu Idadi ya watu haijengi hoja kwani leo Nyumba zilizojengwa nchini nazo zimejengwa na kanisa au serikali! vipi mkuu wangu mbona wakati wa Nyerere tulikuwa hatuna sabuni wlaa dawa ya mswaki leo Mengi anatengeneza vitu hivyo na hatumpi ruzuku?. Unataka kujenga hoja kwa sababu ya dhiki zilizopo..

Business means business! na serikali haitakiwi kuweka mkono wake. Mimi ni mhafidhina na nazungumzwa kama mhafidhina wala sio swala la Udini kama manvyofikiria. Serikali inafanya matumizi ambayo hayahitajiki kabisa, maana kanisa linaweza kabisa kujitosheleza. Wewe mgonjwa ukienda Hospital iwe ya kanisa au private ndipo serikali inatoa subsidy kwa tiba uloipata sio kutoa fungu la Bil 90 hatujui kanisa wamezitumia vipi. Hii ni nooo nooo! Sasa kama wananchi wengi hawaendei ktk hospital hizo, hizo fedha wanazifanyia nini na tunazi account vipi?..

Mimi nasema sikubaliani na Muafaka wa MoU, wewe tazama kwa jicho lolote lile lakini sio kuniita sina akili wakati wewe mwenyewe unaamini vitu vya ajabu ajabu.. na sitaki kwenda huko... lakini kubali tu kwamba serikali yetu haifungamani na dini yoyote na kutoa ruzuku kwa kuweka muafaka na kanisa ni makosa ya kikatiba. Itolewe ruzuku kwa wagonjwa iwe umekwenda KCMC, Kariuki au Hindu Mandal mgonjwa ndiye awe na chaguo la kutibiwa wapi na hiyo ruzuku yake inamfuata kule alikotibiwa - Kabish!
 
Utayasema yote lakini kwa sababu wewe ni kizazi kipya hutaelewa. Zamani enzi za mkoloni, wazazi wetu walikuwa wakitolewa damu na wakoloni walitumia magari haya kwenda vijijini kukusanya damu..Hivyo ukweli upo kwamba Red cross walienda vijijini na kutaka wananchi wajitolee damu na kama ujuavyo mwafrika hatoi damu yake hovyo..Kwa hiyo kulikuwa na ukweli kwamba magari ya Red coss yalikuwa yakutumika zaidi kutafuta damu za watu badala ya kupeleka wagonjwa Hospitalini. nia njema lakini walikuwa mumiani kweli..Iwe akili ya wazee wetu au upendavyo ilitokea hivyo.

Hili swala la MoU sii la kujitolea na wala hata kama sina elimu halifai hata kwa kulumanga kuona serikali ikiingia ubia na kanisa kuendeleza huduma hizi. Tuna fail kwa sababu na kama tulivyo fail ktk Ujamaa zilikuwepo sababu ambazo wengi hatuzikubali lakini ndio ukweli kwamba serikali ilimiliki nguzo zote za uzalishaji na huduma japokuwa kulikuwepo na Private Hospital na shule. Sisi tunatazama source ya matatizo ya Afya na Elimu nchini leo hii na kama serikali inahusika basi vile vile CSSC inahusika pia... mengineyo jaza mwenyewe.

Inaonesha hata sasa bado hujui Red Cross wanafanya nini, yaelekea kutojua (ujinga) ni ibada kwako. Sasa kama magari yalitumika kukusanya damu, hiyo inamaanisha kuwa kuna ukweli kuwa mtu alitolewa damu yote na kufa akatupwa mtaroni? The same ndio mnavyoambiana kuhusu MoU. Umekiri kuwa nia ya Red Cross ilikuwa njema, lkn haikufahamika hivyo so as MoU. Nitaendelea kusisitiza kuwa, hautaifahamu nia nzuri ya serikali na kanisa kuhusu MoU kama unaishi buguruni maisha yako yote. Nenda kwenye FIELD uone mambo yalivyo.

Wale madaktari wanawajibika kwa serikali na ndio maana wameigomea na hawakuligomea kanisa. Na nakukumbusha kuwa, kanisa halipewi fedha na serikali, fedha hutolewa kama RUZUKU KWA HUDUMA ZA JAMII.

Samahani ndugu, mimi sio mwalimu. Naomba nikiri kuwa nimeshindwa kukuelimisha kwa kuwa sina taaluma ya kumuelewesha mtu ambaye dhamira yake ya awali ni kutokuelewa. Endelea kupinga MoU, sisi tutaendelea kujenga mashule na hospitali zaidi kwa kuwa tunaamini kuwa ukiwa na malaria na polio utatuambukiza na sisi pia.

Alamsik bin-nooor!
 
Tunacholilia wapi? Hivi hiki ni kilio cha wakristo au cha madaktari? Kama unamaanisha madaktari wa Bugando, KCMC, TEULE n.k basi huo ndio ule uelewa mdogo unaokusumbua. Wale wanaripoti kwa serikali na sio kwa kanisa, usiwe mvivu wa kufikiri. Nenda kule Ubungo Kibangu, kuna Hospitali pale ya kanisa (imejengwa na inamilikiwa na kanisa) nenda ukatazame je madaktari pale wamegoma?

Shida yenu ni elimu tu, nitawakumbusha hili kila mara. Na ndio maana unaongea maneno ya kujikaanga mwenyewe. Kama nia yako ulitaka kuelezea ni jinsi gani kanisa limeshindwa kuwalipa madaktari BUGANDO, KCMC, TEULE n.k mpk wameamua kugoma, jibu ni kuwa wanafanya kazi chini ya serikali na ndio maana wameigomea serikali na hawakuligomea kanisa. Udini unakufanya huoni facts
Sasa wewe mwenye akili timamu.. hao madaktari wa serikali walioko Bugando na KCMC wamegoma kwa sababu zipi? maana tumeambiwa sio swala la posho tu bali na mengineyo (soma hapo juu kichwa cha mada). Haya mengineyo yanahusiana vipi na Hospitali hizi?.
Wee endelea kutukana na kuniita mdini lakini unashindwa hoja vile.

Kisha nakuomba pia uiweke hapa muafaka wa MoU (Constitution) artical 1 hasa kifungu - D kinasema nini? na utupe ufafanuzi wewe uloenda shule..
 
Wewe unafikiri Nyerere aliamka asubuhi na kutangaza Azimio la Arusha? Mkuu Idadi ya watu haijengi hoja kwani leo Nyumba zilizojengwa nchini nazo zimejengwa na kanisa au serikali! vipi mkuu wangu mbona wakati wa Nyerere tulikuwa hatuna sabuni wlaa dawa ya mswaki leo Mengi anatengeneza vitu hivyo na hatumpi ruzuku?. Unataka kujenga hoja kwa sababu ya dhiki zilizopo..

Business means business! na serikali haitakiwi kuweka mkono wake. Mimi ni mhafidhina na nazungumzwa kama mhafidhina wala sio swala la Udini kama manvyofikiria. Serikali inafanya matumizi ambayo hayahitajiki kabisa, maana kanisa linaweza kabisa kujitosheleza. Wewe mgonjwa ukienda Hospital iwe ya kanisa au private ndipo serikali inatoa subsidy kwa tiba uloipata sio kutoa fungu la Bil 90 hatujui kanisa wamezitumia vipi. Hii ni nooo nooo! Sasa kama wananchi wengi hawaendei ktk hospital hizo, hizo fedha wanazifanyia nini na tunazi account vipi?..

Mimi nasema sikubaliani na Muafaka wa MoU, wewe tazama kwa jicho lolote lile lakini sio kuniita sina akili wakati wewe mwenyewe unaamini vitu vya ajabu ajabu.. na sitaki kwenda huko... lakini kubali tu kwamba serikali yetu haifungamani na dini yoyote na kutoa ruzuku kwa kuweka muafaka na kanisa ni makosa ya kikatiba. Itolewe ruzuku kwa wagonjwa iwe umekwenda KCMC, Kariuki au Hindu Mandal mgonjwa ndiye awe na chaguo la kutibiwa wapi na hiyo ruzuku yake inamfuata kule alikotibiwa - Kabish!

Ndio maana nakwambia wewe ni mjinga. Serikali haina dhamira ya kuchukua hospitali za watu bila sababu za msingi. Kairuki, Aghakan, Hindu Mandal na Ibrahim Haji ni hospitali zilizopo mjini. Lengo la serikali kutoa ruzuku ni kwa maeneo ambayo serikali haijafikisha huduma. Hospitali ulizozitaja zote zipo mjini ambako tayari serikali inao uwezo wa kutoa huduma. Tofauti hapa ni kwamba, kanisa limefika ambapo hao kina hindu mandal hawajafika. Sasa sioni ni ubongo gani unakuongoza kuona kuwa ruzuku ni fasheni. Kule kijijini mgonjwa hana chaguo, ataenda tu kwenye hospitali ya misheni kwani ndio iliopo. Kwa nini unapenda kubisha wkt hujatembea?

Kulaumu nayo ni ibada kwako, ndio maana unajiita mhafidhina bila kuwa na utashi wa kujitegemea. Wewe endelea kupinga MoU, lkn waislamu wanaotibiwa Teule Hospital hawajui unalia nini kwani wao wanatibiwa kwa gharama sawa na amana au mwananyamala. Wewe unayeishi kwa kusikia toka kwa Sheikh Isa ponda na bassaleh endelea kupinga MoU na kudai misikiti ijengwe mashuleni bila kuwa na utashi wa kujenga shule zenu.

Na unaposema 90bn hatujui kanisa wamezitumia vipi ni ujinga ndugu yangu. Mara ngapi nikueleze kuwa fedha zimetolewa kwa hospitali na sio kanisa? Mara ngapi nikueleze kuwa hata mhasibu wa hospitali inayopata ruzuku ya serikali anaajiriwa na kusimamiwa na serikali na sio kanisa? Unaposema hamjui, wewe na nani? Yule anayewajibika kujua za TANROADS zimetumikaje ndio anawajibika kujua na za BUGANDO zimetumikaje. Yule anayewajibika kujua za MEM na MEMKWA zimetumikaje ndio anawajibika kujua za KCMC zimetumikaje. Wewe na huyo mwenzio (unayemwakilisha unaposema 'hatujui') sio kigezo cha kukosekana uhalali wa MoU. Waislamu wenzako wanaotumia hizi hospitali watakushangaa kwa kuwasemea.

Na kwa kuwa unajifanya (ki unafiki) kuwa si udini unakuongoza kusema haya yooote kuhusu MoU, acha basi nikukumbushe kuwa:
1. Zile fedha zilizoaminika kurejeshwa EPA hazijulikani zilipo (bila shaka hizi unajua habari zake jinsi zilivyotumika ndio maana upo kimya)
2. Kesi ya RADA imezua mashitaka kwa waingereza waliotuuzia na wanapata kibano lkn wezi wenzao wa hapa kwetu wanatesa mjengoni (bila shaka unajua jinsi fedha za rada zilivyotumika)
3. Juzi hapa kakamatwa mtumishi wa bodi ya mikopo kwa wizi wa fedha (bila shaka unajua zinavyotumika kwa kuwa unafuatilia kama ilivyo ada ya majukumu yako)
Haya ni machache tu kati ya ambayo umeshayapitia na kuona yako sawa kwa kiyo lazima ulalamike juu ya hizi za KCMC na BUGANDO kwa kuwa wamekunyima taarifa bila kuzingatia kuwa wewe ndio unatakiwa uwe wa kwanza kujua zimetumikaje.

Eeeh Mungu nipe akili, maisha yasiwe mzigo!

Hivyo vitu vya ajabu ajabu unavyovisema juu ya imani yangu wewe viseme tu, mimi sina mashaka juu ya kile ninachoamini. Na kama imani itatakiwa iwe msingi wa maisha yetu, basi jua kuwa mimi ni mwanaume kwa hiyo sina cha kuhofia ktk ahadi za yale tunayotakiwa kuyatarajia tukifika peponi. (mabikira na wine: ni wanawake ndio hatujui wameahidiwa nini)
 
Hivi kweli wewe umeenda shule? hizo Hospital zilizozitaja ni ktk kutoa mfano wa mwananchi kuwa na uwezo wa kuchagua Hospitali gani aende kutibiwa na ndiko ruzuku iende, sikusema maswala la mjini wala shamba vijijini. Ikiwa serikali imeweza jenga Shule hadi vijijini kila kata ina shule zaidi ya moja kwa nini bado serikali inatoa ruzuku kwa CSSC? Nambie hospital za misheni zilizokuwa vijijini kabla ya muafaka 1992 halafu kama hizi hazikujengwa baada ya muafaka.. kama wao waliweza serikali ilishindwa vipi?.

Hujanijibu maswala ya mwanzo umerukia huku na huko mara Rada sijuii EPA, hapa ni swala la Muafaka wa MuO mengine yatakuwa na mada yake tutayajadili... weee vipi msomi gani uloshindwa hata kujadili vitu rahisi kama hivi unakurupuka na matusi matupu.. Hayo ya sheikh Ponda yananihusu mimi kivipi mbona hata mimi namwona mjinga tu ktk maswala ya siasa kama wewe kwa kugubikwa na udini..wee weka hapa artical ya kwanza ya muafaka hasa kifungu cha D utanielewa na wengine pia watajua nazungumza kitu gani..

Hivi ktk fikra zako unafikiri mimi siwezi tukana?
 
Nadhani kubwa katika mgomo huu wa madaktari sio mishahara na maslahi, ni kumuonyesha kwa vitenda JK kwamba nchi hii sio yake na familia yake kama anavyofikiri kwamba leo akiamua tu mradi mtu ni right religion kwake basi ataweza kumpa utukufu wa kuwakalia watanzania wasomi, wenye uwezo, ujuzi nk kichwani simply because yeye ameamua. Madaktari wasirudi nyuma na madai yao yaongezeke kwamba uongozi mzima wa wizara hiyo ufukuzwa mara moja. jamani Pinda ni janga lingine jipya la taifa hili, hivi alikua wapi wakati huyo concubine wa yule chief secretary aliyoondoka kwa aibu na ukabila wake, nashukuru kwamba hata jina nimeshamsahau. wafukuzwe na kushitakiwa, huyo mtasiwa aliyegeuzwa paka mzee afukuzwe kwenye chama cha madaktari milele hakuna cha mwaka mmoja, Nkya nae ajumuishwe. Pinda alikua wapi wakati wizara hiyo ikiwachezea madaktari, acha wananchi tufe leo lakini kesho ya watoto wetu iwe tofauti na huu ushenzi. nchi imemshinda kikwete hana kitu
 
Ni Tanzania pekee katika hii dunia ndio sehemu ambako watu ni wajinga na bado ujinga wao kwao ukawa ni jambo la fahari mbele za watu wengine. Muwe mnatembea mjionee wenyewe. Maneno ya kuambiwa na mtu ambaye hajasoma, hajui kitu ni sumu. Kama vigezo vya uongozi ktk imani zenu vitabakia kufuga ndevu chafu za hudhurungi, kuvaa makubazi na suruali njiwa bila kuzingatia elimu, basi kamwe hamtabadilika.

Kama una nia ya kufahamu, nenda Teule Hospital pale Muheza, halafu fanya uchunguzi wa kiwango cha huduma, nani anasimamia mapato na matumizi, gharama za matibabu ni kiasi gani na matibabu hutolewa kwa nani, halafu tuone kama ukirudi bado utakuwa unapinga MoU!

Ushauri wangu kwa wanaJF wote: Tuwe makini na ushauri na maagizo tunayopewa na mtu/watu wasio na elimu na ufahamu wa maarifa ya dunia. Wenye umri kidogo mtakubaliana na mimi kuwa zamani gari la Msalaba Mwekundu (RED CROSS) lilistahili kukimbiwa kwa kuwa kutokana na simulizi za wazee wetu ambao hawakuwa na elimu na ufahamu juu ya shughuli za Red Cross, tuliambiwa hao ni WANYONYA DAMU a.k.a MUMIANI. Si ajabu leo kuona kuna watu na akili zao wanaielezea MoU kwa mtindo ule ule tulioelezewa kuhusu Red Cross. Je turudie ujinga wa miaka ya 80?

MoU ni jambo lililofanyika kwa akili na sio kwa hisia. Nitaendelea kusisitiza kuwa, ukiishi buguruni na kutibiwa fungus zako AMANA kamwe huwezi jua umuhimu wa MoU, ukitaka kuujua katibiwe MUHEZA (Teule Hospital), Ndanda Mission, n.k

Watanzania tuwe na utashi wa kutumia akili zetu bila shuruti.

Kweli Tanzania inaongoza kwa wajinga na bado hujui kuwa ni mjinga, KUTETEA UFISADI kisa unafanywa na kanisa,

Acha story za Muheza ukijidai as muheza ni mbali sana mimi naijua muheza in out, gharama za muheza ni kubwa kupita hospitali zote za serikali kwa gharama pamoja na kwamba wanapokea ruzuku; kujidai tu kwamba wewe ndio unaufahamu kupita wengine ndio UKILAZA wenyewe?? UFISADI wa KANISA kwako lazima utoke mapofu kwasababu unafaidi without auditing (goverment auditors)..

MoU ni sawa tu RICHMOND in making lakini hiyo ni kati ya kanisa na serikali na wanaofaidi hayo malipo wanajuana wenyewe???

Nenda ulizia bei ya diagnosis muheza halafu uliza pale mwananyamala ndio utaona UWIZI wa mwaka..
 
​Napinga migomo ya madaktari lakini naunga mkono kama wangefanya maandamano baada ya kazi kwani mwisho wa siku katika mgomo wao watanzania wa kipato cha chini ndio wanaoteseka na si viongozi wa serikali kwani wao wataenda kutibiwa nje ya nchi na kuacha wanyonge wakifa
Hao watanzania wa kipato cha chini kama wanateseka, basi na wao waibane serikali, na siyo madokta, naunga mkono hoja.
 
Dk. Mponda asema mishahara ya madaktari imerekebishwa kiasi kwamba wao sasa hivi wanapata mishahara mikubwa zaidi kuliko watumishi wengine wowote wa sekta za uma. Source: Jambo, TBC
 
Mgomo wa madaktari una athari kubwa sana kwa taifa letu. Lakini hili kwa viongozi wetu ambao hata mafua wanatibiwa nje sidhani kama wanaliona. haya yote ni matokeo ya Posho za wabunge kujipangia na kuanza kulipana bila kupitia taratibu maalumu. Binafsi naona huo ni mwanzo tu bado makundi mengine ya wafanyakazi yatagoma. Lakini hivi mshahara na malipo yao yakoje? Anayejua please atujuze maana kuna kauli kaitoa waziri wa afya jana anasema eti madaktari ndio kada inayolipwa mishahara mikubwa. sikujua analinganisha na kundi gani. Labda tatizo ni kundi lenye wafanyakazi wengi sana ndo maana wanaogopa kuongeza/kuwapa maslahi yao kwa wakati. kwa sababu binafsi nafikiri kada yenye wafanyakazzi wengi ni matatizo matupu. bajeti ya mishahara ikija inagawiwa pasu regardless mko wa wangapi.

Sasa iweje kazi za wengi kama walimu, madaktari, askari na zinazofanana ni lini zitathaminiwa na serikali yetu????
 
kabla ya mgomo watu walikuwa wanapata hudumu kwa kiwango fulani, lakini kama mgomo ukiendelea basi huduma zitasimama kabinsa na vifo vitaongezeka mara dufu, na vifo vyenyewe vitakuwa vya watanzania masikini wasioweza kwenda hospitali za gharama kubwa. uwepo wa hospitali za umma unasaidia kwa kiwango kikubwa kuliko kutokuwepo kabisa

Kwani kuna mtu aliyeletwa duniani kuokoa roho za watu? hawa madr ni kama ww na mm na udr kwao ni kaz kama uhasibu ama uhandis. wanafanya kaz kuendesha familia zao na wana mahitaji sawa na watu wa profsn zingine. Tuache ingiza suala la vifo na maslai yao. kwahiyo ni bora familia zao zife kwa kutujali sisi? kama ni lawama bac ziende kwa serikali yetu inayoongozwa na viziwi wanaoamini ktk karne hii bado udaktari na ualim ni wito. nilitegemea tuwashinikize waziri wa afya na katibu wake mkuu wajiuzulu kwa kushindwa kuzuia mgomo kutokea ambao unaleta madhara mengi kwa watz. Hapa serikali inatakiwa kuwajibika. MM nashindwa kuelewa watz cjui katuloga nani. hapa uchaguzi ukija kesho utaona watu hawa hawa wanaolalamika huku wametinga nguo za kijani wakikimbia barbarani na kuimba maisha bora kwa kila mtz. Kama haya ndo maisha bora we better shut our mouth as we have got nothn to discuss here
 
Back
Top Bottom