Navutiwa kujiunga CHADEMA. Nahitaji kujua MSIMAMO wa CHAMA kuhusu Masuala muhimu yafuatayo.

MoseKing

JF-Expert Member
Jul 5, 2017
4,924
8,911
1- Je, CHADEMA Ina amini katika FALSAFA za Mwalimu Nyerere ?

2- Ni upi msimamo was CHADEMA kuhusu Mahakama ya KADHI?

3- Ni upi msimamo wa CHADEMA kuhusu HALI YA MUUNGANO?
- Wanaunga mkono serikali TATU, MBILI, MOJA, MKATABA au KUVUNJA Muungano?

4- Je, CHADEMA Wana amini kipi kuhusu SOKO HURIA?

Je, Serikali iwe inafanya UDHIBITI wa Wafanyabiashara I'll wasiwe wanapandisha Bei za bidhaa na HUDUMA kwa.kuwapangia Bei ya bidhaa au wawache huru Wafanyabiashara SOKO LIAMUE?

5- CHADEMA Wana msimamo gani katika MASLAHI YA WANASIASA vs WANA TAALUMA?

6- Je,. CHADEMA wanaamini MFUMO wetu wa UWAKILISHI wa Wanawake kupitia VITI MAALUM Ni SAHIHI?

Ahsante
 
Bora ukawekeza nguvu zako kwenye shughuli zako za kika siku za kukuingizia kipato. Hayo mambo ya siasa waachie wenyewe. Ukilazimisha kuingia huko, basi ujiandae kutoka ukiwa umechoka kweli kweli.

Kiufupi tu siasa za Bongo ni pasua kichwa. Kuanzia CCM, CHADEMA, NCCR-Mageuzi, ACT Wazalendo, TLP, nk. Vyama vyote hivyo ni mali ya watu, na siyo taasisi kama unavyo ona kwa nje.
 
1. Chadema ipo mrengo wa kati, so inaamini positive ideologies za nyerere na zile za kijima haizikubali.
 
2. Chadema ni muumini wa secular government so mambo ya kadhi ilipendekeza waislam waunde chombo chao kinachohusu dini yao na wasikifungamanishe hicho chombo na serikali kabisa.
 
3. Chadema ni mashabiki wa katiba pendekezwa ya jaji warioba ambayo majority ya watz walipendekeza serikali tatu, so automatically chadema ni serikali tatu.
 
4. Chadema ni muumini wa mixed economy, so inakwenda na mazuri ya soko huria na pia mazuri ya closed economy, so automatically chadema ikishika dola itatembea mule mule kwenye theory za economy.
 
5. Chadema haimbani mwanasiasa wala mfanyabiashara ktk maslahi yake, yenyewe inasisitiza kufuata sheria na katiba ili kuepusha mgongano wa kimaslahi.
 
Ungeuliza msimamo kuhusu ruzuku?
Msimamo kuhusu wabunge wa viti maalum..

Msimamo kuhusu Zanzibar...
Kuhusu Ruzuku nimeuliza. Ingawa nataka kujua kwa ujumla wake Kama waitrrr wanaona vyama vya siasa kupewa Ruzuku Ni SAHIHI au sahihi

Na ukubwa wa mishahara ya Wanasiasa ni sahihi au si sahihi.

Msimamo kuhusu Zanzibar nadhani ipo hapo kwenye suala la Muungano.

Kuhusu viti maalum naongezea.
 
1- Je, CHADEMA Ina amini katika FALSAFA za Mwalimu Nyerere ?

2- Ni upi msimamo was CHADEMA kuhusu Mahakama ya KADHI?

3- Ni upi msimamo wa CHADEMA kuhusu HALI YA MUUNGANO?
- Wanaunga mkono serikali TATU, MBILI, MOJA, MKATABA au KUVUNJA Muungano?

4- Je, CHADEMA Wana amini kipi kuhusu SOKO HURIA?

Je, Serikali iwe inafanya UDHIBITI wa Wafanyabiashara I'll wasiwe wanapandisha Bei za bidhaa na HUDUMA kwa.kuwapangia Bei ya bidhaa au wawache huru Wafanyabiashara SOKO LIAMUE?

5- CHADEMA Wana msimamo gani katika MASLAHI YA WANASIASA vs WANA TAALUMA?

Ahsante
Huvutiwi popote sema tuu unataka kujua wanasimama wapi kwenye masuala hayo
 
1- Je, CHADEMA Ina amini katika FALSAFA za Mwalimu Nyerere ?

2- Ni upi msimamo was CHADEMA kuhusu Mahakama ya KADHI?

3- Ni upi msimamo wa CHADEMA kuhusu HALI YA MUUNGANO?
- Wanaunga mkono serikali TATU, MBILI, MOJA, MKATABA au KUVUNJA Muungano?

4- Je, CHADEMA Wana amini kipi kuhusu SOKO HURIA?

Je, Serikali iwe inafanya UDHIBITI wa Wafanyabiashara I'll wasiwe wanapandisha Bei za bidhaa na HUDUMA kwa.kuwapangia Bei ya bidhaa au wawache huru Wafanyabiashara SOKO LIAMUE?

5- CHADEMA Wana msimamo gani katika MASLAHI YA WANASIASA vs WANA TAALUMA?

Ahsante
Ujamaa ulishafeli
Kadhi ni mambo ya waislamu wenyewe
Serikali tatu
Soko huria ndio mpango mzima
Taaluma iheshimiwe
 
Njoo chama mapinduzi huko utahangaika tu halafu utarudi tu CCM Ni taasisi hao wengine Ni saccos au vikundi vya kupiga ruzuku tuu CCM HOYEEEEE
download-1.jpg
 
Chadema ni chama cha wachaga kinaamini katika principles za umangi meza.

Soma kuhusu malengo ya Chaga party ndio umo umo inapita Chadema.
Dhihaka za ukabila sio kitu kizuri cha kukifurahia

Sisi sote waTanzania tukosoane kwa staha.
 
Back
Top Bottom