Tamko la NHIF kuhusu mapitio ya Kitita cha Mafao cha NHIF

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,462

YAH: TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAPITIO YA KITITA CHA MAFAO CHA NHIF CHA MWAKA 2023

Ndugu wanahabari, Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa niaba ya Kamati ya kupitia Kitita cha Mafao cha NHIF cha mwaka 2023, naomba nitoe taarifa kwa umma yenye lengo la kukanusha taarifa iliyotolewa tarehe 27 Februari, 2024 na Vyama vya Watoa Huduma Binafsi za Afya (APHFTA, Christian Social Services Commission -CSSC, na BAKWATA) na pia nitoe ufanunuzi kwa umma kuhusu jukumu la Kamati yangu iliyoundwa na Mheshimiwa Waziri wa Afya na kazi iliyofanyika.
Ndugu wanahabari

Mtakumbuka kwamba maboresho wa Kitita cha Mafao cha mwaka 2023 yalianza tangu mwaka 2018 kufuatia maelekezo yaliyotolewa na Wizara ya Afya iliyoelekeza Mfuko kufanya mapitio ya Kitita cha Mafao na bei zake kwa kuzingatia Mwongozo wa Matibabu nchini Toleo la mwaka 2017.

Kitita cha Mafao kinachotumika hivi sasa kilifanyiwa maboresho kwa mara ya mwisho mwaka 2016. Hivyo, kutokana na maendeleo katika teknolojia ya tiba na mabadiliko ya bei katika soko la huduma za afya pamoja na uwezo wa kugharamia, Mfuko umelazimika kufanya mapitio katika Kitita hicho ili kwenda sambamba na mahitaji yaliyopo na hali halisi ya utoaji wa huduma za afya nchini.

Vilevile, kwa kuzingatia takwa la kifungu cha 15.2 cha mkataba baina ya Mfuko na Watoa Huduma kinautaka Mfuko kutoa taarifa kwa watoa huduma kuhusu kusudio la kufanya maboresho ya kitita miezi mitatu kabla ya kuanza utekelezaji. Katika kutekeleza takwa hilo, Mfuko ulitoa notisi ya kusudio la kufanya maboresho ya Kitita chake tarehe 01 Agosti 2022 kupitia barua yenye Kumb Na. EA.35/269/01-A/32 kwa lengo la kutoa muda kwa watoa huduma wote kujiandaa na kutoa maoni kabla ya kuanza utekelezaji wake. Hata hiyo pamoa na juhudi hizo, kitita cha NHIF hakikuweza kutangazwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wenzetu wa APHFTA kutaka ushirikishwaji zaidi.

Tarehe 04 Januari 2024 Mheshimiwa Ummy A. Mwalimu (Mb), Waziri wa Afya aliunda kamati ya kitaalamu kwa lengo la kumshauri kuhusu maboresho ya kitita cha Mafao cha mwaka 2023. Aidha, Kamati ilijumuisha wataalam kutoka Serikalini ikijumuisha Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Watumishi wa Umma (PSSSF), pamoja na Taasisi zisizo za kiserikiali ikiwemo Asasi Zisizo za Kiserikali, Taasisi binafsi inayohusika na masuala ya Bima, Taasisi ya Kimataifa inayohusika na utoaji wa ushauri katika masuala ya ukaguzi wa mahesabu na kod.

Mheshimiwa Waziri alitoa hadidu za rejea kwa Kamati kama ifuatavyo:-
Kusikiliza wadau wa pande zote husika ikiwemo APHFTA, MAT, CSSC, BAKWATA na NHIF ili kupata uelewa wa maudhui ya kitita cha mafao cha mwaka 2023 na hoja zilizowasilishwa;

Kupitia mapendekezo ya bei yaliyowasilishwa na watoa huduma wa sekta binafsi kuhusu kitita cha mafao cha mwaka 2023 ikiwemo gharama za huduma na bei za dawa katika kitita cha mafao cha mwaka 2023;
Kufanya uchambuzi wa gharama halisi (actual costing) kwa huduma za upasuaji, procedures na vipimo vinavyofanyika mara kwa mara katika kitita cha mafao cha mwaka 2023;

Kuandaa mapendekezo ya bei za huduma na dawa katika maeneo yaliyolalamikiwa bila kuathiri uhai na uendelevu wa Mfuko;

Kufanya mapitio ya skimu nyingine za bima ndani na nje ya nchi zinazotoza malipo ya ziada (Co-payment) na kutoa mapendekezo kuhusu suala la uchangiaji gharama kwa wanachama wa NHIF; na
Kubaini na kushauri juu ya jambo lolote litakalokuwa na tija katika utekelezaji wa kitita cha mafao cha NHIF cha 2023.

HATUA ZILIZOPITIWA NA KAMATI KATIKA KUTEKELEZA HADIDU ZA REJEA

Kufuatia hadidu za rejea za kufanya mapitio ya Kitita cha Mafao, Kamati ilitumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na ;
Kufanya vikao na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), watoa huduma wa sekta binafsi (APHFTA) na mashirika ya dini (CSSC na BAKWATA) pamoja na Chama cha Madaktari (MAT);

Kufanya mapitio ya nyaraka za mapendekezo ya bei katika kitita cha mafao kilichoboreshwa yaliyowasilishwa na Mfuko pamoja na watoa huduma wa sekta binafsi na mashirika ya dini;

Kufanya tathmini ya hali halisi ya bei ya bidhaa za afya katika soko kwa Mkoa wa Dar es Salaam kwa baadhi ya dawa zilizokuwa zimelalamikiwa;

Kufanya uchambuzi wa uzoefu kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi katika maeneo ya kudhibiti gharama ikiwemo co-payment; na
  • Kufanya uchambuzi wa gharama halisi (actual costing) katika maeneo ya
procedure na vipimo.

TAARIFA YA KAMATI YA WATAALAM KUHUSU MABORESHO YA KITITA CHA MAFAO CHA NHIF CHA MWAKA 2023
Baada ya kukamilika kwa jukumu iliyopewa, Kamati ya Wataalam iliwasilisha taarifa ya mapendekezo yake kuhusu Kitita cha Mafao kwa Mheshimiwa Waziri wa Afya tarehe 06 Februari 2024. Aidha, kuanzia tarehe 7 hadi 8 Februari 2024, taarifa hiyo iliwasilisha katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI.
Taarifa ya Kamati ya Wataalam ilifanya mapitio ya maboresho ya Kitita cha Mafao cha mwaka 2023 cha NHIF kwa kuwashirikisha wadau ambao ni APHFTA, MAT, CSSC, BAKWATA na NHIF. Baada ya majadiliano ya kina, Kamati na wadau walikubaliana katika vigezo vitakavyotumika katika mapendekezo ya bei ya huduma za dawa, upasuaji na vipimo katika kitita kinachopendekezwa. Vigezo hivyo ni kama ifuatavyo:-
Kwa huduma za dawa kuzingatia bei ya jumla ya soko ya dawa kutoka kwenye walau maduka 10 yanayotambulika na kutumia bei ya kati (median);

Gharama za uendeshaji na kiwango cha faida kufuata vigezo vya huduma zinazotumika sana, wastani na taratibu ambapo kwa upande wa dawa gharama za uendeshaji kuwa kati ya asilimia 20 hadi 30 na kiwango cha faida kuwa asilimia 10 hadi 20; na

Kwa huduma za upasuaji kuzingatia bei ya jumla ya soko katika ununuzi wa vifaa na vitendanishi; idadi ya vifaa na vitendanishi vinavyohitajika; rasilimali watu inayohitajika na muda unaotumika kutoa huduma husika; kiwango cha uchakavu wa vifaa vinavyotumika; gharama za uendeshaji na kiwango cha wastani wa faida.

Ndugu wanahabari

Matokeo ya uchambuzi uliofanywa na Kamati ya Wataalam

Kwa kuzingatia vigezo vya uchambuzi vya Kamati na katika kuhakikisha Mfuko unaendelea kuwa stahimilivu, Kamati imefanya maboresho katika kitita cha mfao cha mwaka 2023 ambapo matokeo ni kama ifuatavyo:-

Kati ya dawa 722 kama zilivyobainishwa katika kitita cha mafao cha mwaka 2023, bei ya dawa 237 zimeongezeka, bei ya dawa 239 zimepungua na 246 zimebaki kama zilivyopendekezwa awali;

Katika huduma za upasuaji na vipimo baadhi ya bei za huduma zimepungua, kuongezeka na kubaki kama ilivvyopendekeza awali;

Katika viwango vya ada ya ushauri na kumuona daktari ikilinganishwa na mapendekezo yaliyowasilishwa katika kitita kipya cha mafao cha mwaka 2023, baadhi ya ada kwa kuzingatia ngazi ya aina ya utaalam viwango vimeongezeka, vimepungua na baadhi kubaki kama ilivyokuwa awali.

Endapo Mfuko ungelipa madai kwa kutumia mahudhurio ya mwaka 2022-23 kwa kuzingatia bei iliyopendekezwa na Mfuko katika kitita cha 2023, madai ya shilingi bilioni 585.07 yangelipwa sawa na punguzo la asilimia 17 ikilinganishwa na kitita cha mwaka 2016. Aidha, endapo mapendekezo ya bei ya Kamati yatatumika Mfuko utalipa kiasi cha shilingi bilioni 577.45 sawa na punguzo la asilimia 18 ikilinganishwa na kitita cha mwaka 2016.

Mapendekezo ya Kamati ya Wataalam ni pamoja na:
Kuanza kutumika kwa Kitita cha Mafao cha mwaka 2023 pamoja na maboresho yaliyopendekezwa na kamati katika sehemu ya ada ya ushauri na kumuona daktari, huduma za dawa, upasuaji na vipimo;

Kitita cha mafao cha NHIF kifanyiwe mapitio ya bei za huduma kila baada ya miaka miwili ili kuwezesha mabadiliko ya bei kuzingatiwa kwa

wakati kama inavyotekelezwa na taasisi mbalimbali kama vile Bohari Kuu ya Dawa (MSD);

Kujumuisha kifungu Na. 7 cha Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote Na. 13 ya mwaka 2023 kinachoipa TIRA jukumu la usimamizi na udhibiti wa mfumo wa bima ya afya kuwa kati ya vifungu vinavyoanza kutekelezwa;

Wizara isimamie utaratibu wa rufaa katika upatikanaji wa huduma za afya ili kudhibiti huduma ambazo sio za dharura na zinapatikana katika ngazi ya msingi ya utoaji wa huduma;

Kutekelezwa kwa utaratibu wa mwanachama kuchangia gharama za huduma (co-payment) kama ilivyopendekezwa katika baadhi ya huduma za kitita kipya cha mafao;

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuimarisha utaratibu wa ushirikishwaji wa wadau wakati wa mapitio ya vitita kwa kuweka utaratibu utakaojenga uelewa wa pamoja mathalani kuwa na vikundi kazi vya kitaalam (Technical working group).

MREJESHO WA MAPENDEKEZO YA KAMATI YA WATAALAM
Mnamo tarehe 19 Februari, 2024, Mheshimiwa Waziri wa Afya aliitisha kikao kilichohudhuriwa na wadau wakiwemo NHIF, APHFTA, CSSC, BAKWATA na MAT kwa lengo la kutoa mrejesho wa mapendekezo ya Kamati ya Wataalam.Katika kikao hicho, wadau walipitishwa katika taarifa ya Kamati ya Wataalam, ambapo kwa pamoja waliridhia na kuipongeza Wizara na Kamati katika maeneo yafuatayo:

Kuweka vigezo vitakavyotumika katika mapendekezo ya bei ya huduma za dawa, upasuaji na vipimo;
Kuzingatia mapendekezo yaliyotolewa ya viwango vya ada ya ushauri na Kumuona daktari kwa kigezo cha ubobezi wa daktari (speciality) badala ya ngazi ya kituo cha kutolea huduma; na

Wizara kufanya utafiti ili Serikali iweze kutoa msamaha kwa baadhi ya kodi au ruzuku kama ilivyo sasa kwa baadhi ya sekta pamoja na kuwezesha watoa huduma katika sekta binafsi kupata fursa ya mitaji nafuu.

Maazimio ya kikao hicho ni pamoja na yafuatayo:

Mheshimiwa Waziri wa Afya aliridhia kitita kilichoboreshwa na Kamati ya Wataalam kianze kutumika;

NHIF kuendelea na taratibu za kuanza kutumia kitita hicho; na

Wadau kupewa kitita cha mafao kilichoboreshwa kwa kuzingatia mapendekezo ya Kamati ya Wataalam ili kuwa na uelewa wa bei zilizopendekezwa.

HITIMISHO
Kufuatia matamko yaliyotolewa na watoa huduma za afya wa sekta binafsi APHFTA, Kamati inapenda kutoa msimamo wake wa kitaalam kwamba Wizara kupitia NHIF iendelee na utekelezaji wa kitita cha mafao kilichoboreshwa cha NHIF cha mwaka 2023 kama ilivyoshauliwa na Kamati.

Aidha ieleweke kwamba Kamati hii iliundwa na Waziri wa afya kwa ajili ya kumshauri masuala ya kitaalamu kuhusu namna bora ya kuandaa na kutekelezeza kitita cha mafao kilichoboreshwa cha mwaka 2023.

Ahsante kwa kunisikiliza.

………………………………….
Dkt. Baghayo A. Saqware

MWENYEKITI WA KAMATI YA KUPITIA KITITA CHA MAFAO CHA NHIF 2023​

Wao waendelee na hivyo vitita vyao na waliovikataa waendelee kukaza.

It's business, siyo lazima wawe wabia kama hawaoni maslahi kufanya kazi na nyinyi.
 
Huu ni uharibifu sio maboresho,tunaoumia ni sisi watu wa chini,shupazeni shingo kabisa ili wateja wenu wafe tuone mtaendesha vipi hicho kitaasisi chenu,ubabe kwenye
biashara haufai,kamati imekuja kwenye mazungumzo ikiwa na majibu yake.

Wao kama kamati hawawezi kuhisi maumivu tunayopitia watu wa chini,maana wao wanapesa na muda wowote wakiugua wanaenda kutibiwa ng'ambo.

Baba yangu wa huku mpigamiti ambaye anaishi kwa kutegemea mshahara wangu wa shilingi 200,000 atkuwa na uwezo wa kufika muhimbili kwenye hospitali nzuri au za rufaa kweli ikiwa private hospital hawatampokea?

NHIFTZ tuueni kabisa ili mfaidi michango yetu
 
Kama ndivyo
Sasa haya malalamiko ya watoa huduma za afya yanatoka wapi?

Serikali kupitia kamati iache kupotosha umma. Irudi kwenye meza ya mazungumzo maana Kamati ilipaswa kuwasilisha taarifa kwa Wizara kisha wao ndo waje na hizi kauli. NHIF imeingia kwenye mikwaruzano kadhaa na watoa huduma hususan kwa kuchelewesha malipo kwa muda mrefu

Hapa kuna jambo linafichwa, au Ummy anatafuta kichaka cha kujiokoa na lawama kwa kuwasukuma NHIF waje kulisemea jambo linalohitaji Wizara ilifanyie utatuzi wa dharura.
 
Back
Top Bottom