Naunga mkono wazo la Mbunge kuweka Picha ya Rais Samia kwenye Sarafu ya Tanzania

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,051
49,735
Naunga mkono wazo la Mbunge kuweka Picha ya Rais Samia kwenye Sarafu ya Tanzania ili kutunza kumbukumbu na alama muhimu ya Maendeleo ya Nchi yetu.

BoT fanyeni haraka wazo hili.

===


Mhe. Waziri Mkuu mwaka 2006 Bunge hili lilipitisha sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya kuipa mamlaka benki hii kudizaini fedha kwa kuweka nembo na material mbalimbali, mwaka 2021 nchi hii imepata Rais wake wa kwanza mwanamke anayefanya kazi nzuri na anatambulika katika Bara la Afrika na duniani kama Rais madhubuti na wa mfano, je, serikali haioni sasa kwamba kuna haja ya kuweka kumbukumbu ya kudumu kwa Rais Samia Suluhi Hassan kwa kuweka picha yake katika fedha za nchi hii?" - Mbunge Ng'wasi Kamani.

 
Ndiyo wapiga kura walichowatuma ? Au kwa vile mliingizwa mjengoni kwa mabavu ya vyombo vya dola? Pumbavu kabisa hawa majizi ya kura
 
Hadi Sasa ameshindwa kabisa kudhibiti swala la kukatika kwa umeme halafu awekwe kwenye notikwa kifupi Hana maajabu
Changamoto ya kukatika Kwa umeme ni ndogo sana kulinganisha na aliyofanikiwa.

Wewe unaweza kudhibitiwa umeme usikatike?
 
Tukija kuona matunda ya Sera zake baada ya miaka 50 tutakumbuka kufanya hivyo, ila kwasasa ni mapema sana...watu wenye maono ni wale wanaoweka long term plan alafu zinatoa matokea chanya siyo wale wanalenga urefu wa pua yao.
Nashauri tu, mawazo ya mbunge yaheshimiwe ila asiseme mambo kwa pupa akiongozwa na ushabiki.
 
Back
Top Bottom