Shehe: Asiyetambua Juhudi Anazofanya Rais Samia Anasukumwa na Roho Mbaya.

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,109
49,812
Shehe Kisq amesema wale ambao hawatambui juhudi zilizofanywa na zinazofanywa na Rais Samia kimsingi wanasukimwa na Roho mbaya na sio uhalisia wa mambo.

---
Kiongozi mmoja wa madhehebu ya Kiislamu nchini Sheikh NURDEEN KISHQ amezungumzia umuhimu wa Watanzania kutambua na kupongeza juhudi zinazofanywa na Rais @samia_suluhu_hassan katika kuleta maendeleo endelevu nchini.

Akizungumza jijini DAR ES SALAAM katika hafla ya wanawake kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kuwa kinara wa nishati safi ya kupikia, mazingira na afya ya mama na mtoto iliyohudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kiongozi huyo ambaye taasisi yake ya Alhikma Foundation imeandaa mashindano ya makubwa ya kimataifa ya usomaji QURAN Tukufu tarehe 24 mwezi huu amesema kila mmoja kuanzia ngazi ya familia, taifa, bara la AFRIKA na dunia kwa jumla wanatambua mchango wa uongozi wake Dkt SAMIA SULUHU HASSAN.


View: https://www.instagram.com/reel/C4VsxyhMoJC/?igsh=MTB2NGNoOW12ZHhwMg==

My Take
Naunga mkono hoja ya Sheikh.

Toka Tanzania imepata Uhuru hakuna Rais aliyewahi mwaga mabilioni Kwa mabilioni kila sekta ya Nchi hii kushinda Samia.

View: https://www.instagram.com/p/C4QnwpMt_ju/?igsh=MXVoM2x2aGUwZ2E2ag==
 
Kwa nini lazima iwe roho mbaya na si tofauti za kisiasa au kifalsafa tu?
Mapicha picha yashaanza 2025 imekaribia...
Vyote vinahusika japo Kwa sehemu kubwa watu wa Bara hawataki Mzanzibari Atawale,tena Mwanamke ambae ni Muislamu ndio maana wanaleta fitina nk.

Mwingine aliwahi niambia kwamba hata Ajenge Barabara zote Kwa tiles hatumpendi nikajua eeh hapo Sasa hoja sio uchapakazi Bali ni mambo ya kijinga ya roho mbaya kama anavyosema bwana Shekh hapo Juu.

View: https://www.instagram.com/p/C4QnwpMt_ju/?igsh=MXVoM2x2aGUwZ2E2ag==
 
Vyote vinahusika japo Kwa sehemu kubwa watu wa Bara hawataki Mzanzibari Atawale,tena Mwanamke ambae ni Muislamu ndio maana wanaleta fitina nk.

Mwingine aliwahi niambia kwamba hata Ajenge Barabara zote Kwa tiles hatumpendi nikajua eeh hapo Sasa hoja sio uchapakazi Bali ni mambo ya kijinga ya roho mbaya kama anavyosema bwana Shekh hapo Juu.

View: https://www.instagram.com/p/C4QnwpMt_ju/?igsh=MXVoM2x2aGUwZ2E2ag==

Hiyo kaull ya Sheokh ni ya kishamba sana.

Na bora kaisema Sheikh, si mtu msomi. Sheikh anahitaji ilmu dunia.

Anasema haiwezekani kutotambua jitihada za rais Samia kwa sababu za Kifalsafa.

Usipotambua tu, basi una roho mbaya.

Sheikh kashahitimisha watu wana roho mbaya tu kabla hata hajawasikiliza hoja zao.

That is basically saying "I don't give a fvck what you have to say, If you don't recognize Samia you are just a hater".
 
Angesema kinyume chake angeambiwa anachanganya dini na siasa au kupewa jina la sheikh wa chadema. Basi huyo ni sheikh wa ccm ambako kwao ni ruksa kuchanganya dini na siasa.
 
Huo ndio ukomo wa fikra zao.

Daima siasa na dini havikai chungu kimoja.
Africa watu wengi sana kama huyu Sheikh hawawezi fikra dhahania.

Hawawezi kufanya siasa za kushindanisha falsafa za, kwa mfano, ubepari na ujamaa, kushindanisha vyama, kusema huyu Samia anapingwa si kwa sababu yeye Samia, bali kwa sababu anawakilisha sera za CCM, sera, labda, za kijamaa, au sera zinazojipinga zenyewe hazijijui ni za kijamaa au kibepari, sera zilizopitwa na wakati, na kuna watu wanampinga si kwa sababu yeye ni Samia, bali kwa sababu anawakilisha CCM, anawakilisha sera zilizochoka etc.

Yani watu kama huyu Sheikh lazima waweke personality ya mtu kwenye siasa. Siasa za kukosoa sera hawawezi.

Mtu akija na kusema Samia anaangushwa na sera kwa sababu CCM haina ugatuzi wa madaraka mikoani, hilo suala halihusiani chochote na Samia wala chuki, hilo ni suala la sera za chama na tofauti za kifalsafa.

Sasa Sheikh anaelewa tofauti hizo za kifalsafa kati ya watu wanaotaka ugatuzi wa madaraka mikoani na kwenye serikali za mitaa na wasiotaka?

Sheikh anaelewa nini kuhusu political economy na economy?

Au anabwabwaja maneno ovyo tu?
 
Sheikh hyo kaongea kiuchawa,kujipendekeza
Uzuri kila kitu kina muda wako

Ova
 
Back
Top Bottom