Naunga mkono msimamo wa serikali juu ya kutoingilia bei ya chakula, tatizo ni kwamba katiba yetu bado inasema 'Tanzania ni nchi ya kijamaa'

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,605
Masuala ya bei ni masuala yanayohusu uchumi wa soko, yaani bei huwa inaamuliwa na nguvu za demand and supply au huwa tunaita 'Price mechanism'. Muasisi wa falsafa hii ni baba wa uchumi, na mwanafalsafa wa Uskochi Adam Smith kupitia kitabu chake kilichoandikwa zaidi ya miaka 240 iliyopita (1776).

Na kupitia dhana za Adam Smith, ndipo haswa ulaya na Marekani walijikuta wakipendelea zaidi kuwa na mifumo ya kiuchumi ambayo ime base kwenye falsafa za kiliberali ambazo zilimaanisha kwamba uchumi ulikuwa zaidi unamuliwa kwenye soko na watu binafsi na kunakuwa kuna 'minimum role from the government'.

Kwa maana hiyo, kwenye uchumi wa kiliberali na kibepari, maamuzi ya nini kizalishwe, kwa kiasi gani kizalishwe, kiasi gani kikauzwe n.k, yote haya yalikuwa ni maamuzi ya mtu binafsi pasipo kuingiliwa na serikali. Kwa maana hiyo hakuna namna yeyote serikali atakuwa anaingilia maamuzi ya mkulima kwenye kupanga bei kwasababu hakushiriki kwa namna yeyote kwenye kuamua nini cha kulima, ni wakati gani wa kulima, na wakati gani wa kuvuna n.k

Kwa nchi kama Tanzania ambayo tumezoea serikali kufanya kila kitu, na kwasababu pia katiba yetu bado inatamka kwamba Tanzania ni nchi ya kijamaa, wananchi wa Tanzania wengi wao bado wapo kwenye mtanziko wa kufikiri ya kwamba serikali inahusika moja kwa moja kwenye kufanya maamuzi ya bei kwenye uchumi kitu ambacho mimi naamini ni makosa makubwa sana.

Serikali haitakiwi kuwa na mkono wowote kwenye kuamua bei za vyakula, kwasababu bei za vyakula zinaamuliwa na forces of demand and supply. Kwasababu kama wakulima wamefungia mazao ndani na matokeo yake supply imepungua sokoni au kumetokea uhaba. Kusema kwamba serikali iwaingilie wakulima wauze mazao yao kwa nguvu, hilo litakuwa ni kosa la kisheria. Kwasababu aliyelima ni mkulima na sio serikali, sasa kwanini umuamulie wakati gani auze mazao yake na wakati gani asiuze, au wapi auze mazao yake - soko la ndani au soko la nje?

Serikali inachotakiwa kufanya ili ku regulate hizi bei za vyakula bila kuadhibu mkulima na mlaji, na ambacho naona sasa wameanza kukifanya ni haya yafuatayo.

1. Kuweka mipango ya kuongeza uzalishaji kwenye kilimo - hii maana yake itasababisha supply ya mazao iwe ni nyingi sokoni na ukishakuwa na supply kubwa maana yake automatically bei ya mazao lazima ishuke. Hapa kwenye mipango ya kuongeza uzalishaji kuna mambo kama

  • Mbolea ya ruzuku
  • Kuwawezesha mabwana shamba ili watoe elimu kwa wakulima
  • Kushawishi vijana kuingia kwenye kilimo, hili ni jambo zuri kwasababu ukiwagawia vijana mashamba na wakafanikiwa kulima lazima uzalishaji utaongezeka. Naunga mkono sera iliyoanzishwa na serikali kugawia vijana mashamba na kuanzisha block farms.

2. Serikali iwe na strategic food reserve kwa ajili ya kustabilize market - Hii nadhani pia ni kitu muhimu kiwepo, hii strategic food reserve, inatakiwa iwe ni ile akiba ya chakula ambayo itakuwa chini ya serikali kwa lengo la ku stabilze market.

Kiuchumi, kama wakulima wameficha mahindi ndani, na sisi tunajua kwamba wameficha, haina haja ya kutumia nguvu kushawishi wakulima kuuza mazao yao, serikali itachokifanya ni kutoa mahindi kwenye reserve yake na kuyauza kwa wingi sokoni, ukifanya hivo maana yake utaongeza kwa haraka supply ya mahindi sokoni, na kukiwa na supply kubwa ya mahindi sokoni, itapelekea bei ianze kushuka.

Sasa kwa upande wa mkulima, akianza kuona bei inashuka, huwa wana react kwa kuanza na wao kuuza mahindi yao, kitu ambacho kitapelekea supply izidi kuongezeka maradufu na bei kushuka kwa kasi. Na bei ikishuka kwa kasi, serikali wata 'Build up' ile reserve waliyoiuza ili wawe na supply kubwa zaidi ya kustabilize market siku za mbeleni.

Sasa hapa swali la kujiuliza ni kwamba, hiyo reserve kweli inatosha ama ndo tia maji tia maji?? Kama serikali haina food reserve ya ku stabilize market pale kwenye uhitaji, hilo sasa ndio litakuwa changamoto ambayo nadhani ni muhimu iwekwe kwenye sera ya nchi.

Kwa wanaofuatilia wenzetu dunia ya kwanza, hichi ndo kitu huwa mara kwa mara kinafanyika. Nchi ya marekani kwa mwaka jana, wakati bei ya mafuta inapanda kwa kasi, Rais Biden aliamuru 'strategic petroleum reserve iingizwe sokoni ili kuongeza supply kwenye uchumi.

Kwahiyo all in all, naunga mkono sana serikali ya Samia kwenye kushughulikia hili suala, na namuunga mkono sana Mh. Bashe kwa kulisimamia hili suala vizuri. Tatizo ni kwamba watanzania asilimia kubwa bado wana mitizamo ya kijamaa, ya kudhani kwamba serikali inatakiwa kufanya kila kitu. Na hili ndo baadhi ya masuala ambayo nataka kwenye katiba mpya, yawe amended kabisa kabisa.

Serikali haitakiwi ku own uchumi wala kupanga bei.

N.Mushi
 
Hakuna mkulima aliyefungia chakula ndani ni Wafanyabiashara, chakula kinasafirishwa nje kwa wingi ndomana bei zinapanda kila siku.
 
Tuna waziri kiazi si wengine ndugu zetu wakulima,yaani hapo anapiga kelele ila wakulima washauza chakula tokea mwaka jana.

Sasa hivi wenye hizo bidhaa ni walanguzi, eti anadai awamu yake wakulima ndio wanapiga pesa tatizo lake hana hata data,wakulime hali zao zipo vilevile wanaopiga pesa walanguzi
 
Hakuna mkulima aliyefungia chakula ndani ni Wafanyabiashara, chakula kinasafirishwa nje kwa wingi ndomana bei zinapanda kila siku.
Hata hilo sio tatizo mkuu, chakula kuuzwa nje ya nchi iwe kinauzwa na wafanyabiashara au iwe kinauzwa na wakulima, hilo sio tatizo, na wala hai justify serikali kutia mkono wake, kwasababu hizi ni shughuli za kuichumi za watu binafsi na sio serikali joseph1989
 
Hata hilo sio tatizo mkuu, chakula kuuzwa nje ya nchi iwe kinauzwa na wafanyabiashara au iwe kinauzwa na wakulima, hilo sio tatizo, na wala hai justify serikali kutia mkono wake, kwasababu hizi ni shughuli za kuichumi za watu binafsi na sio serikali joseph1989
Sasa kama kila mkulima ataweka focus auze nje ya nchi unafikiria hali itakuwaje humu ndani. Soon maharage yatafikia kuuzwa elfu 5
 
Back
Top Bottom