Siasa za Korosho Tanzania, serikali kupandisha bei bila ya kusema namna itadhibiti hujuma za walanguzi

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Katika ziara ya Rais Kanda ya Kusini, serikali imeripotiwa kupandisha bei ya korosho bila ya kusema namna gani itadhibiti hujuma za walanguzi ambazo zimekuwepo kwa miongo mingi.

Kwa tabia, hulka na utamaduni wa Tanzania, nina imani walanguzi watapindua ahadi ya serikali ya kupandisha bei ya korosho kwa sababu pia hao hao wenye dhamana za kusimamia sekta na matamko ya serikali ndiyo hao hao walioko ndani ya biashara ya korosho na hata mazao mengine.

Msimu ukifika, walanguzi hawa watawaambia wakulima kuwa bei imeshuka soko la nje wanakopeleka korosho, hivyo wakinunua kwa wakulima kwa bei mpya iliyopandishwa na serikali hawaendi kupata faida. Hivyo wakulima wachague moja kati ya mawili:

1. Washushe bei chini ya bei iliyopangwa (iliyoahidiwa) na serikali ili walanguzi waweze kumudu kununua.

2. Wabaki na korosho zao ziozee ndani kwa muda usiojulikana na baadaye huko zipungue ubora wake.

Walanguzi watawatishia wakulima kuwa wakichagua namba 2 hapo juu basi wao walanguzi wataenda kununua korosho Msumbiji.

Vipindi vya kuelekea chaguzi, serikali inakujaga na matamko mepesi yasiyotekelezeka ili tu kushawishi kura na kuhadaa wananchi; matamko yasiyowezekana kusimamiwa kwa tija.

This is not Tanganyika it is Danganyika.
 
Ndugu mleta mada naona kuna jambo hujalielewa vema kwenye haya mzao global.

Hakuna hata siku moja serikali inaweza ikapandisha bei labda inaweza kupunguza bei kwa wakulima kwa kuweka tozo nyingi kwa mnunuzi.

Bei ya korosho kuwa kubwa inategemea na bei ya soko.
 
Back
Top Bottom