Nataka niache advance PCB nahisi imenishinda

Nataka niache advance PCB nahisi imenishinda

Pole sana mdogo wangu. Brother wako hapa kilinikuta kitu hicho hicho! Nimetoka o'level vizur sana (division two point 18) nikiwa nmetandaza B kwenye kombi ya PCB, hivyo kama kawaida nikaona advance nikasome PCB.
Nilipofika kule (nilisoma Mtwara tech) mambo hayakuwa kama nilivyotarajia..! Mambo yalikuwa magumu sana! Kwa mwanzo somo nililokuwa nalielewa vizur lilikuwa ni Biology pekee! Chemistry na Physics mambo hayakuwa mazuri kabisa! Yaani mambo yalikuwa yana-vapour kwa haraka mpaka nikaanza kuhisi nmerogwa (ingawa imani hizo siziamini!)
Ilifika kipindi form five ilikuwa nikisoma chemistry or physics ndani ya saa moja nmeshasahau kila kila kitu! Yaani mpaka definition haikai kichwani..! Nilichanganyikiwa kwakweli!

Bahati nzuri nilikuwa napenda kujichanganya na mabrother wa form six and so nikashare nao tatizo langu! Jamaa walinicheka sana (cause nao walipitia issue kama hizo) but walinisaidia kufanya utatuzi wa tatzo langu ingawa bado haikuwa the best solution..!

Namkumbuka bro wangu anaitwa boaz alisema "Ubavu, angalia dogo, chuo wanataka principal mbili tu.! (kwa kipindi kile principal ilikuwa E) so chakalika upate E ya biology na chemistry then off you go to the university"
Kwa kipindi kile niliona hiyo ndo ilikuwa solution and so nikalikacha rasmi somo la physics..! Nikaamia kwa chemistry! Na kweli, muulize mtu yeyote aliyesoma PCMB (phy, chem, bios, or math) advance atakwambia.. Kuwa chemistry ndio somo la kukutoa cause huwa halikatai mtu!

Fortunately, necta ya form six nilipita kwenye tundu ya sindano kwa kutumia formula ya brother boaz kwani nilipata div three (ndipo pcb wengi wanapoangukia hapa) ya point 15 meaning nilikuwa nna D mbili za bios and chem! Hivi sasa nmemaliza chuo na nmepata kajikazi kakujishikiza!
Turudi kwako, mara nyingi sipendi kumpa mtu ushaur mmoja! Huwa napenda kumchambulia mtu pros and Con's za kila option ili mwenyewe ajue wapi ni kuzuri zaidi!
Moja, unaweza kutumia njia yangu ambayo baadae ilinikosti kwa vile physics nilikuja kupata F ila nikaenda chuo! Na sikuweza kufikia malengo ya wanaPCB wengi ya kusoma MD!, hapa unatakiwa pia uchague topics za kusoma pia..! Kwenye chemistry pitia sana physical chemisry, Inorganic chemistry pamoja na General chemisry... Hizi ndio mkombozi wako... Maana kama ukizikazia huwa hazichomoi! Hapa tafuta kitabu cha last papers kutoka mwaka 1987 mpaka 2006! Hiki ndio awe rafiki yako..!maswali yote ya topics hizo nilizokwambia inabidi uwe unayajua ndani nje..! Kuanzia data mpaka solutions! Organic chemistry! Asee huyu mdudu anavitu vingi sana.! Halafu maswali yake huwa hayatabiriki..! Zile conversion inatakuwa kuanzia temperature, catalyst mpaka pressure inayotakiwa ili reaction itake place! Kwa mm niliacha nayo! Ila kama unajiamini unaiweza.. Ukiweza kuimaster hii A ya chemistry inanukia cause organic chemisry hubeba 60%ya maksi zote kwa paper one na two..!
Biology yote inatakiwa iwe at the fingertip of your hand! Meaning swali lolote la topic yoyote inatakiwa usilifikilie zaidi ya dk moja..! Yaani ukishamaliza kulisom swali hakuna muda wa kurudia.. Inatakiwa uwe umeshajua muulizaji anataka nn kwenye swali hilo..! Pia ni muhimu kufupisha jibu lako kuwa fupi ila lenye ujazo wa haja.. Msahihishaji huwa analess than one minute kusahihisha swali moja so hawezi kuhangaika kutafuta jibu katikati ya essay lako! Majibu yawe in bulletin way hata kama swali ni la assay form! Kama ni swali la kudescribe ni lazima uchore mchoro! Kama ni explain ni lazima isizid mistari mitano ya jibu lako! (hapa kuna mengi ambayo siwezi kuyaandika yote so unaweza kuja pm nikupe namba tuongee..). Or

Mbili, unaweza kukaza zaidi! Tafuta likizo hata ya week moja, tulia fikilia ni kwann mambo yamekufika hapo ulipo?! Je ni strategy or materials yanayokufanya ushindwe kuperfom..? Mara nyingi huwa ni strategy..! Kwa maana shule za govt kwa advance ni msuli yatima (meaning unakomaa na materials wewe mwenyewe mpaka kinaeleweka!) so huwa inakuwa how you study and for how long ndicho kinacho-determine ufaulu wako..! Kuna jamaa yangu tulikuwa room moja, alikuwa anastrategy za ajabu sana..! Yeye alikuwa anasema, "Ubavu advance mambo ni mengi sana and so unatakiwa urudie rudie kusoma hizi mambo mara nyingi iwezekanavyo..!" akandelea kusema "inatakiwa uwe umeimaliza syllabus yote ya advance tena ya masomo yote ndani ya week moja..!" wakati huohuo fahamu idadi na uzito wa vitabu vyiiliyopo advance! Mimi ilinishinda njia hii kwakweli"
Hapa nataka niseme neno kidogo!. Hii ndio njia ninayoona at least itakusaidia.. Baada ya kumaliza form six nilikuja kuelewa ni kwann hii ndio njia nzuri! Unajua mtu anavyotoka o'level huwa anaexpectation kusema kuwa "kama nmetoka kwenye masomo tisa na nikafaulu kwann nisifaulu nikiwa na masomo matatu tu!" thats totally wrong! Yaani advance sio ya kuifikilia kihivyo kabisa..! Mimi nilikuwa ni mmoja ya watu wanaoisema serikali kuwa wamekosea kwa kuruhusu watu walioferi form six kuruhusiwa kufundisha o"level kama amesoma deploma ya ualimu..! Ila kwa sasa nmeona ndio option nzuri, kwann nasema hivyo..! Advance mara nyingi mtu huwa afeli kwasababu ya kuto kusoma..! Bali huwa anafeli kwasababu ya kutokujua jinsi ya kulijibu swali la mtihani effectively..! Jamaa aliyepata div four ya advance ukimwambia akufundishe topic moja wapo... Utashangaa jinsi anavyoijua ndani nje... Tena mpaka na mifano..! But ndo hivyo unakuta necta anatoka na four...! Mtu huyu vitu anavijua sema jinsi ya kuviweka kwenye pepa ndo shida...! Unakuta anabeat around the bush mpaka muda unaisha..!
Sasa basi! Jaribu kufanya maswali mengi iwezekanavyo.. Tena sio ya vitabuni peke yake... Fanya mitihani mingi iwezekanavyo! Hapo utajihakikishia kufaulu!

Tatu, kama umeona kuwa hutoweza kutoka kwa njia hii ya advance, unaweza pia kuomba vyuo vya diploma vya afya na ukaacha hiyo advance kiroho safi tu! Tena ndo zinakaribia kufunguliwa sasa..! Njia hii ni nzuri kwa kuwa unakuwa na uhakika wa kutoka... Chuo kufeli ni kutaka mwenyewe tu.. Labda ukushike ugonjwa wa ajabu.. Wakati wa mtihani!

All in all! Advance sio sehemu ya kwenda kujaribu..! Inataka constant discipline ya muda..! Kuanzia unaingia siku ya kwanza mpaka unatioka siku ya mwisho! Elius kiyombo TO wa mwaka 2006 anamisemo yake..! Huwa anasema.. "Ukiwa advanve hakuna rangi utaacha ona" pia husema "siku ya kwanza kuingia form five wote huwa mnakuwa na div one ya point tatu, but huwa inapungua kulingana na aina ya maisha utakayoyaendesha mpaka necta inakufikia.. So inawezekana mwezi mmoja kabla ya necta ukawa umebaki na div one ile ile or umebaki na zero..!
Pia wakati unasoma jaribu kujifananisha na watu wa misuli mirefu..! Jaribu kukaa nao karibu cause watakupa changamoto ya kuongeza msuli wako...! Pamoja na usongo..! Kama unasoma boarding! (tena hapa ndio muhimu) na ngoja niandike kwa herufi kubwa ACHANA NA RATIBA YA SHULE, USIIFATISHE KABISA HII...! NI MBAYA NA HATARI KWA AFYA YAKO YA KUSOMA! Mi ratiba yangu ili kuwa ni kama ifuatavyo..! Naamka saa moja na nusu..! Mbili kamili nipo room kwenye meza yangu naanza misuli ya bios..! Mpaka saa nne muda wa uji nakuwa nmeshapitia topic mbili za bios pekee..! Kuanzia saa tano mpaka saa nane kamiri nakuwa nmeshapitia topic tatu za phy chemistry! Baada ya msosi nalala kuanzia saa kumi mpka saa kumi na mbili..! Then nakula msosi wa jioni..! Napiga story mpaka saa moja na nusu...! Mbili kamili nipo mezani kwenye room yangu misuli inaanza tena (kwa advance hasa watu wa pcbm usiku ndio unatakiwa uwe muda wa kusoma sana..! Unless otherwise usingizi uwe unakushinda nguvu) hapo ntasoma mpaka saa tano na dk 45 (huu ndo muda wa usingizi kuanza kusumbua..) nalala kwa saa moja mpaka saa sita na dk 45 nikiamka nnanguvu mpya..! Kuanzia saa saba kamili mpaka saa kumi na nusu alfajir ni mwendo wa kusoma tu..! Then nalala naamka saa moja tena kazi inaanza tena... Hii ni toka mwezi wa sita wa form five mpaka mwezi wa pili (kipindi chetu ndo papers zilikuwa zinafanywa muda huu) wakati wa necta
Na mwisho kabisa.. Jipatie muda mwingi wa kupumzika.. Ikiwezekana chagua jumamosi (kama wasabato) or jumapili kama waroma nk) or hata ijumaa (kwa waislamu) kuwa ni siku ya mapumziko ukikusanya nguvu..!
Mimi binafsi nilichagua ijumaa kwasababu huwa ni siku fupi sana..! And so ilikuwa ndo siku ya kulala..!
Kama we niwa day..! Uliza wengine...

Ubavu!
risala
 
Kaza Uzi advance ndivyo ilivyo hvyo mambo yanasaulika fasta,kikubwa usipanic kwa kua umeshajua kasoro ifanyie Nazi.yangu hayo ndgu
 
Ushauri wa kuendelea na pcb hapa hautasaidia...mentality yako imeshajitune kushindwa!kama una ndoto za kua kweye field ya afya,hujachelewa kujiunga na vyuo vya CO's!
Kwa pcb advance izo ndio alama zake..mimi o'level pcb nlikua na DBC,ila advance nikapata BAD!!!sitakuja kusahau msuli YATIMA niliopiga those days!!
Sasa ni Medical Doctor,since 2013
Hongera sana mkuu!!
 
Kumbe hizo marks unazopata ndio size yako has a ukizingatia high school uzito wa masomo unaongezeka. CCA maana take Physics ulipata 41, Chemistry 41 na Biology 81. Kwa hiyo usilalamike.
 
Ubavu kiongozi nimekuelewa Sana kijana ni Wa kiume pia hana kabisa mambo ya kijingajinga ya kupoteza muda. Ulimaliza mwaka gani hapo mtwara Tech? maana mpaka sasa naona memory yote ipo kichwani Kama vile bado unasoma hapo. Na vp kuhusu facilities Kama vitabu vya biology, physics na chemistry vinapatikana hapo shuleni au nipe list ya vitabu vizuri nimnunulie aende navyo. All in all natanguliza shukrani Sana kwa ushauri wako nitaufanyia kazi kwa uwezo Wa Mungu.
 
Wewe jikaze acha uoga. Mimi mwenyewe nilsoma pcb, ingawa chuo nlienda somea ktu kngne. Wewe malza hapo ingawa pcb ni ngum, itakusaidia mbeleni vtu vngne utakua unaviona rahsi
 
Ubavu kiongozi nimekuelewa Sana kijana ni Wa kiume pia hana kabisa mambo ya kijingajinga ya kupoteza muda. Ulimaliza mwaka gani hapo mtwara Tech? maana mpaka sasa naona memory yote ipo kichwani Kama vile bado unasoma hapo. Na vp kuhusu facilities Kama vitabu vya biology, physics na chemistry vinapatikana hapo shuleni au nipe list ya vitabu vizuri nimnunulie aende navyo. All in all natanguliza shukrani Sana kwa ushauri wako nitaufanyia kazi kwa uwezo Wa Mungu.
Mimi nmemaliza hapo mwaka 2013. Nakumbuka mengi kwasababu ya good memories nyingi sana nilizotengeneza hapo..! Nakumbuka vitu vingi pia kwa vile nnauwezo mkubwa wa kutunza kumbukumbu. Bi mkubwa huwa anashangaa sana hasa nnapomkumbusha vitu vya zamani kipindi nnamiaka mitano..!

Turudi kwenye issue msingi..! Dogo wa pcb kwanza ni lazima awe na BS (Biological Science) yenyewe ni nyekundu..! Kama akiweza kumeza BS vizur pekee basi anaweza pata B ya necta! Kama familia inajiweza unaweza kuongezea UNDERSTANDING BIOLOGY hii haija jaa sana ila ninarecomend apatiwe CHANDY YA BIOLOGY! Hapo biology tunasema at least anaweza kucompete na syllabus ya baraza! Pia usisahau kupitia posta or mlimani city kwenye vitabu vya ANATOMY AND PHYSIOLOGY (kama unataka dogo awe BEN CARSON )

Kwa chemistry unaweza kumpatia CHANDY ya chemistry... Unaweza kumnunulia ile ya form five.. Then akirud likizo unamalizia iliyobakia (ya form six) kama unataka awe nondo kwenye inorganic na organic kuna vile vitabu vya baraza (actually hivi ni must have books) vinakuaga two volumes each! Kama unataka aelewe zaidi muongezee na RAYMOND CHANG! (a very good book on inorganic and general chemistry)

Physics lazma kwanza awe na CHANDY zote mbili! Kama mpunga anao unamuongezea na ROGER MUNCASTER kwaajili ya ELECTRICITY & ELECTRONICS, bila ya kusahau NELKON &PARKER (swali tata za necta huwa wanazichomoa huku)! kama unataka dogo awatishe wenzie mtafutie na UP (UNIVERSITY PHYSICS)

HAPO JUU NMEWEKA VITABU VYOTE HIVYO KAMA HOME MPUNGA UPO. ILA KAMA NI MAJALALA BASI FANYA HIVI!

ATAFUTE VITINI VYA SUREBOY MANDIA PAMOJA NA MBUGA (FOR BIOLOGY) ! HIVI VIKO PALE MCHIKICHINI! PIA APATE VITINI VYA SIR UNGA VYA PHYSICAL CHEMISTRY BILA YA KUSAHAU NOTES ZA PHYSICS ZA... Ayaaa nmesahau! Nani yulee daaah! Sio muddy physics.! Wala sio mtata de mtatuzi.! Daaah jamaa nmemsahau..! Labda kwa vile sijawahi kusoma kwake..!

BIOLOGY:
-BS (35000-40000) na
-ANATOMY & PHYSIOLOGY (hivi huwa wanauza jamaa wa pale posta kwenye vitabu vya mtumba vya kizungu bei huwa mpaka 35,000)
Mpende mdogo wako mpatie na GIFTED HANDS apate mzuka wa shule!

CHEMISTRY
CHANDY ZOTE MBILI AND VITABU VYA ORGANIC NA INORGANIC CHEMSTRY VYA BARAZA (VOL I &II)

PHYSICS
APATE CHANDY ZOTE MBILI NA NELKON & PARKER!
VINGINE ATAPATA KWA WENZIE...

PIA MWAMBIE AWE ANAINGIAGA PALE COMPUTER LAB. PALE KUNA ENCYCLOPEDIA BRITANNICA AMBAYO HUWA NA MAMBO MAZURI SANA YANAYOWEZA KUMSAIDIA...! (nilifumaga ORNITHINE CYCLE LA KIBABE PALE)!

Kuhusu Library ya mtwara tech nisikufiche mkuu pale hakuna vitabu vya advance.. Mi nilikuwa naenda kuazima vitabu vya Novel za watoto pamoja na VITABU VYA UJAMAA NA KUJITEGEMEA (shule ya ccm ile ) PAMOJA NA HISTORIA ZA MAKOMREDI WA RED ARMY WALIOFANYA HEROIC DEEDS DURING THE WAR! (very socialistic of mwal. Nyerere )

VITABU VYOTE HIVYO INABIDI AVIPITIE INSIDE OUT! NYUMA MBELE! Hapo atakuwa na chance ya kufika anapopataka!

Ubavu!
 
Niliamua kujiita hivyo..
I know you know why Nilikuuliza hilo swali!! Angalia User ID yako kisha angalia hili jibu ulilonipa mwanzo!!
Kinachonipa uoga nasoma sana na nina elewa na maswali nasolve mpaka nafurahia but since nikifika point ya mtihani duuuh...naishiwa nguvu hapa may nimepifa mock form five nimetoka na div 4 ya mwisho sasa naogopa kupotea form six
Now look... User ID yako, Thread yako na majibu yako VYOTE ni FEAR! FEAR! FEAR!!

Nimekuuliza kwanini umejiita hilo jina, umesema uliamua tu...! YES, ni rahisi sana kuamini kwamba ULIAMUA tu but trust me, you're filled with FEAR na matokeo yake inakukosesha confidence! Unaogopa KUPOTEA Form VI... another FEAR! Utapotea vipi Form VI?! Utapotea au UTAFELI?!

And let's assume umefeli... SO WHAT?! Wewe utakuwa ndo wa kwanza kufeli? Ina maana ukifeli ndo utakuwa UMEPOTEA?! How?!

Take that FEAR shit out of you!! Una miezi 9 at your disposal. Una Jumamosi na Jumapili 72 at your disposal... which means, una at least FULL 2 months za kujisomea!!! I repeat, you don't have luxury time... katika hizo Jumamosi na Jumapili 72 una angalau 720 hours!!!

Hapo sijaweka time after school hours Jumatatu - Ijumaa!!! Hivi unafahamu ulivyo na muda wa kutosha kufanya kile ambacho unadhani huwezi tena kufanya simply because you're filled with FEAR?!

Ipe muda wa kutosha Chemistry & Biology... trust me, UTAFAULU tu!! Ondoa uoga uliojaza nafsi yako hadi unafikia kujiita muoga wa jf huku mwenyewe ukidhani umejipa tu hilo jina kumbe in fact, the jina reflects the inner part of you!!

Ukiwa mwoga utasoma with tension... utakuwa unasoma hiki unaacha, unasoma kile unaacha kwa sababu, kila utakapokuwa unasoma utakuwa unafikiria topic XYZ ndio itakayotoka kwenye mitihani... kwahiyo utakuwa unaacha unachosoma na kukimbiia Topic XYZ!!! Ukiwa na fear utakuwa unaingia kwenye paper ukiwa sio wewe!!

FEAR leads to NERVOUS leads PANIC leads to RESTLESS MIND leads to FAILURE kwa sababu, hayo yakitokea you'll never ever be able to fully remember nini ulisoma!!!

Ukishaondoa FEAR utatawaliwa na CONFIDENCE! Ukishakuwa na confidence, huwezi kuwa nervous and so no panic!! Matokeo yake utakuwa na SETTLED MIND itakayokufanya uwe na uwezo wa kukumbuka mengi ya yale uliyosoma and then BINGO!!
 
Bora uende chuo, maana ukimaliza six km matokeo sio mazuri changamoto kupata kozi unayoitaka maana mnachaguliwa so ukute kozi moja chaguo la wengi ingawa vyuo vinaongezeka
 
Mimi nmemaliza hapo mwaka 2013. Nakumbuka mengi kwasababu ya good memories nyingi sana nilizotengeneza hapo..! Nakumbuka vitu vingi pia kwa vile nnauwezo mkubwa wa kutunza kumbukumbu. Bi mkubwa huwa anashangaa sana hasa nnapomkumbusha vitu vya zamani kipindi nnamiaka mitano..!

Turudi kwenye issue msingi..! Dogo wa pcb kwanza ni lazima awe na BS (Biological Science) yenyewe ni nyekundu..! Kama akiweza kumeza BS vizur pekee basi anaweza pata B ya necta! Kama familia inajiweza unaweza kuongezea UNDERSTANDING BIOLOGY hii haija jaa sana ila ninarecomend apatiwe CHANDY YA BIOLOGY! Hapo biology tunasema at least anaweza kucompete na syllabus ya baraza! Pia usisahau kupitia posta or mlimani city kwenye vitabu vya ANATOMY AND PHYSIOLOGY (kama unataka dogo awe BEN CARSON )

Kwa chemistry unaweza kumpatia CHANDY ya chemistry... Unaweza kumnunulia ile ya form five.. Then akirud likizo unamalizia iliyobakia (ya form six) kama unataka awe nondo kwenye inorganic na organic kuna vile vitabu vya baraza (actually hivi ni must have books) vinakuaga two volumes each! Kama unataka aelewe zaidi muongezee na RAYMOND CHANG! (a very good book on inorganic and general chemistry)

Physics lazma kwanza awe na CHANDY zote mbili! Kama mpunga anao unamuongezea na ROGER MUNCASTER kwaajili ya ELECTRICITY & ELECTRONICS, bila ya kusahau NELKON &PARKER (swali tata za necta huwa wanazichomoa huku)! kama unataka dogo awatishe wenzie mtafutie na UP (UNIVERSITY PHYSICS)

HAPO JUU NMEWEKA VITABU VYOTE HIVYO KAMA HOME MPUNGA UPO. ILA KAMA NI MAJALALA BASI FANYA HIVI!

ATAFUTE VITINI VYA SUREBOY MANDIA PAMOJA NA MBUGA (FOR BIOLOGY) ! HIVI VIKO PALE MCHIKICHINI! PIA APATE VITINI VYA SIR UNGA VYA PHYSICAL CHEMISTRY BILA YA KUSAHAU NOTES ZA PHYSICS ZA... Ayaaa nmesahau! Nani yulee daaah! Sio muddy physics.! Wala sio mtata de mtatuzi.! Daaah jamaa nmemsahau..! Labda kwa vile sijawahi kusoma kwake..!

BIOLOGY:
-BS (35000-40000) na
-ANATOMY & PHYSIOLOGY (hivi huwa wanauza jamaa wa pale posta kwenye vitabu vya mtumba vya kizungu bei huwa mpaka 35,000)
Mpende mdogo wako mpatie na GIFTED HANDS apate mzuka wa shule!

CHEMISTRY
CHANDY ZOTE MBILI AND VITABU VYA ORGANIC NA INORGANIC CHEMSTRY VYA BARAZA (VOL I &II)

PHYSICS
APATE CHANDY ZOTE MBILI NA NELKON & PARKER!
VINGINE ATAPATA KWA WENZIE...

PIA MWAMBIE AWE ANAINGIAGA PALE COMPUTER LAB. PALE KUNA ENCYCLOPEDIA BRITANNICA AMBAYO HUWA NA MAMBO MAZURI SANA YANAYOWEZA KUMSAIDIA...! (nilifumaga ORNITHINE CYCLE LA KIBABE PALE)!

Kuhusu Library ya mtwara tech nisikufiche mkuu pale hakuna vitabu vya advance.. Mi nilikuwa naenda kuazima vitabu vya Novel za watoto pamoja na VITABU VYA UJAMAA NA KUJITEGEMEA (shule ya ccm ile ) PAMOJA NA HISTORIA ZA MAKOMREDI WA RED ARMY WALIOFANYA HEROIC DEEDS DURING THE WAR! (very socialistic of mwal. Nyerere )

VITABU VYOTE HIVYO INABIDI AVIPITIE INSIDE OUT! NYUMA MBELE! Hapo atakuwa na chance ya kufika anapopataka!

Ubavu!
Mkuu etii naomba kujua kwa mtu anaepata division 4 form VI anaweza pata kozi yoyote chuo chochote
 
Ni wangapi Form VI wanapata ZERO?! Unataka kusema wote hao waliiba au kufanyiwa mitihani?!
uspanic br. madhara ya spoon feeding hayo. kama u-mtabe wa prac basi na a level komaa nazo pracs!
 
uspanic br. madhara ya spoon feeding hayo. kama u-mtabe wa prac basi na a level komaa nazo pracs!
Sasa na wewe ndo unaongea nini?! Ni-panic kwa sababu zipi?!
 
Mkuu etii naomba kujua kwa mtu anaepata division 4 form VI anaweza pata kozi yoyote chuo chochote
Kwanini usome kozi yoyote ("bora twende") kwavile tu unadhani huna jinsi wakati Form IV ulifaulu?!
 
Hata Mimi niliponea kwenye tundu la sindano 2 ya mwisho ashukuliwe Mungu sasa hivi ni MD
 
Unaweza ukapata AAA lakini bado ukawa na msingi mbaya. Kufaulu pekee hakumaanidhi una msingi mzuri.

Je. Ni kweli wote wanaofaulu huwa wanaelewa somo husika? Nitakupa mfano.

Nina zaidi ya miaka 16 tangia nipate degree yangu ya kwanza. Majuzi walikuja vijana kazini kufanya mafunzo kwa vitendo wakiwa mwaka wa pili wa degree yao ambayo ni sawa na ya kwangu.

Nilishindwa kuwaelewa pale nilipokuwa nawafafanulia uhusiano wa kazi na kile walicho kisoma. Tena niliwaambia hii ni application ya FARADAYS LAW. nikaona hawajanielewa. Nikawauliza kama wamewahi kuisoma hiyo kitu wakakubli. Lakini wakasema WAMESAHAHU INAHUSU NINI.....

Hii ni kwamba wamesoma na kufaulu lakini hawakuelewa. Tulioelewa huwa hatusahahu. Na huu ni mmoja wapo wa MISINGI YA KISOMA inayotokana na aina ya walimu pamoja na aina ya mazingira uliyosomea.

Ukifundishwa na mwalimu kilaza anayekariri usitegemee kuelewa. Tegemea kufaulu kwa kukariri. Lkini huko mbeleni lazima aliyeelewa atofautiane na aliyekariri au aliyeibia mtihani. Huwa haijifichi.

Kifupi tunao waajiriwa wa aina ya wanafunzi niliowataja hapo juu. Hawawezi kazi isipokuwa majungu wizi fitna na uchawi.
Hakika umenena mkuu....ni ukweli mtupu!!!!!
 
Mkuu etii naomba kujua kwa mtu anaepata division 4 form VI anaweza pata kozi yoyote chuo chochote
Mkuu ili uchaguliwe inabd uwe na at least principal pass mbili..! Ili upate division four ni lazima upate principal pass moja....! Or ukose kabisa.. ! So in whatever scenario.. Kama umepata four degree hauendi..! Unless otherwise ukasome diploma..! Na ndio option iliyobakia..!
 
Back
Top Bottom