muoga wa jf, what's your Plan B endapo utagonga mwamba kwa wazazi suala la ku-drop na kusoma alternative course?!
Kwangu mimi naona huo ndio uamuzi wa busara zaidi lakini ukigonga mwamba; vuta nguvu upya na sahau suala la kukata tamaa! When that happens; tenga muda mfupi sana kwa Physics manake itakupotezea muda wakati productivity ya huo muda inaweza kuwa very minimal. Kinyume chake, wekeza muda kwenye Chemistry na Biology. Trust me, Chemistry ni rahisi sana kufaulu kwa sababu watungaji wa mitihani hawana ubavu wa kwenda mbali sana na vitabu!
Hapo juu umezungumzia uwezo wako wa kukariri! Biology unaweza kukariri lakini Chemistry hata kama kukariri kunalipa (am not sure manake mimi kichwa changu ni kibovu kweli kweli linapokuja suala la kukariri) muhimu kwa Chemistry ni kuzielewa concepts mbalimbali. Chagua topics chache za kuanza nazo ambazo ni rahisi pia kuzielewa. Hizi ziwe zile ambazo zina-cover sehemu kubwa ya mitihani! Wekeza muda wako huko and trust me, hadi May 2018 unaweza kukuta unatoka na angalau FDD.
Ikiwa FDD itakukosesha kusoma Bachelor bado unaweza kwenda kusoma Diploma huku ukiwa na good Form VI results itakayokutofautisha na wenzako waliotoka FIV au waliofeli FVI. Hii good FVI results ndio mtaji wako wa baadae utakapo-apply bachelor with equivalent qualification.
NOTE: Don't give up kabla hujapata formal alternative!!
I repeat, ipunje muda Physics manake Physics haitambui kabisa jitihada za mtu especially kama mtu mwenyewe ni wa PCB!!
In addition, sijui una muda gani hapa JF! Kama hujaizoea sana JF basi at least for now till June 2018 na yenyewe ikalie mbali kama Physics!! JF ni Gogo Zembe! JF ni very addictive!! Though you can learn a lot through JF but for now you don't have luxury time for it!!
Don't say hukuambiwa utakapojikuta unalazimika ku-balance muda wako kwa masomo matatu-- Chemistry, Biology & JF huku JF likiwa ndiyo favorite subject linalohitaji more attention!!!