Nataka niache advance PCB nahisi imenishinda

Nataka niache advance PCB nahisi imenishinda

Tushukuru Mungu kwa Yote.

Japo umejifunza unaweza sasa kumpa ushauri mtu wa kwenda advance au chuo....
Me ilikuwa hivii, nilichaguliwa pcb o level nilipiga B physics, B chemistry na A biology, nimefika tu advance shule ya serikali, hamna waalimu,hamna viti na meza, hamna vitanda watu wanalala kwa shift, waalimu hawafundishi halaf unakuja kupewa paper tu, nilikuwa na score marks za umri wa Serengeti boys (below 18)... Kuna mda nilikuwa narudi nyumbani tu bila sababu niliwaambia wanihamishe au niende chuo, lakini mungu alinitia nguvu ya kutokata tamaa, na hapo ninapata 16 physics sio kwamba sisomi, nlikuwa nakula msuli nahisi mkoa mzima mm ndio nilikuwa nakua wa mwisho kulala....Ila mda huo nimepata 16, kuna mdau nalala nae bweni moja alikuwa anapiga 80+, nikawa nafanya nae discussion za kutosha, na kuadopt mfumo anaotumia kusoma mtihani uliofata nilipiga 72, hivohivo mpk mwisho wa siku necta nimepiga div1.7, nimeshaapply vyuo vinne, nasubiri matokeo ya first round yanatoka mwezi huu trh25...
 
Since nimeingia advance sijawahi kupata zaidi ya 50marks kwenye chem&phys zaidi napataga kwa bios isitoshe mtihani wangu wa annul form five nimepata zero ffs respectively kwa PCB sasa nimekata tamaa kabisa na kuona hakuna ninachofanya zaidi ya kwenda kuzungusha form six 2018. Hivyo rasmi nahitaji kuongea na wazazi nitafute alternative ways ya kwenda collage nikachuke course nyingine

N.B sio kwamba sisomi nasoma tena sana ila sielewi kwanini inakuwa hivi

Pia o level nilifaulu vizuri tu kwa CCA in PCB

==========

MREJESHO(2023)

Wakuu kwa sasa nimerudi baada ya miaka kadhaa naomba nilete mrejesho.

Kiukweli sikuweza kuendelea na advance PCB nikaamua kwenda diploma ya afya kwa course ya Nursing and Midwifery, nikagraduate mwaka 2020.

Baada ya hapo nimeweza kufanya kazi hospital mbili moja dispensary Dar na nyingine mkoani Iringa hospitali ya mkoa.

Kwa sasa Tangu mwaka jana niko moja ya shirika kubwa la afya nikifanya kazi mbalimbali katika project zinazohusiana na research.

Hivyo sijajutia uamuzi nilioufanya kama itampendeza Mungu mwaka huu nitarudi kusoma bachelor ya physiotherapy Muhas au natafuta scholarship nikasome Public health bachelor nje.

Asanteni sana.

Narudi kwenye id yangu mpya...

Achana nayo, kuna watu wamesoma HKL na sasa ni ma diplomat wazuri! Hayo madudu magumu sio guarantee ya mafanikio.

Unasoma kwa ajili yako, na ukifeli utafeli kwa lawama zako, usisikilize watu, fanya jambo unaloweza.

Wazazi wa Kibongo wakati mwingine wanatesa sana watoto wao ili wakajivune vijiweni, piga chini haraka.
 
Me ilikuwa hivii, nilichaguliwa pcb o level nilipiga B physics, B chemistry na A biology, nimefika tu advance shule ya serikali, hamna waalimu,hamna viti na meza, hamna vitanda watu wanalala kwa shift, waalimu hawafundishi halaf unakuja kupewa paper tu, nilikuwa na score marks za umri wa Serengeti boys (below 18)... Kuna mda nilikuwa narudi nyumbani tu bila sababu niliwaambia wanihamishe au niende chuo, lakini mungu alinitia nguvu ya kutokata tamaa, na hapo ninapata 16 physics sio kwamba sisomi, nlikuwa nakula msuli nahisi mkoa mzima mm ndio nilikuwa nakua wa mwisho kulala....Ila mda huo nimepata 16, kuna mdau nalala nae bweni moja alikuwa anapiga 80+, nikawa nafanya nae discussion za kutosha, na kuadopt mfumo anaotumia kusoma mtihani uliofata nilipiga 72, hivohivo mpk mwisho wa siku necta nimepiga div1.7, nimeshaapply vyuo vinne, nasubiri matokeo ya first round yanatoka mwezi huu trh25...
Shule gani hiyo haina viti wala meza...aisee ccm wametuweza
 
Halafu matokeo yakitoka shule za serikali zina PCB point 3 kibao, lazima kuna namna.
Shule nliosoma simu zilikuwa kama zinaruhisiwa tu tuseme, robo tatu ya wanafunzi walikuwa na smartphone na wanazitumia hadharani hamna kujificha, kwahiy tulikuwa tunaconnection na shule nyingine kubwa kama mazinde,mzumbe,kuna wanangu walikuwa na simu ilboru, tabora boys nk, na tulikuwa tunatumiwa kila mtihani uliofanyika katika hizo shule kuanzia mwezi wa pili mpk may, trust me guys, kila paper!!! Nimesolve yoote mpk kuna paper nlikuwa nazo zimetoka feza inasemekana ndio necta code 1 zote nmesolve, necta haivuji wakuu, hakuna mtihani uliokuja vile vile, hakuna, hakuna lakini kuna maswali yamejirudia, of course ukisolve sana lazima ukutane na maswali ushawahi kuyasolve, kila somo kuna maswali nlikuwa nshayapiga, Ila mengi ni mapya
 
Back
Top Bottom