Since nimeingia advance sijawahi kupata zaidi ya 50marks kwenye chem&phys zaid napataga kwa bios isitoshe mtihani wangu wa annul form five nimepata zero ffs respectively kwa pcb sasa nimekata tamaa kabisa nakuona hakuna ninachofanya zaidi ys kwenda kuzungusha form six 2018..hivyo rasmi nahitaji kuongea ba wazazi nitafute alternative ways ya kwenda collage nikachuke course nyingine
N.B sio kwamba sisomi nasoma tena sana ila sielewi kwanini inakuwa hivi
-pia o level nilifaulu vizuri tu kwa CCA in PCB
Pole sana mdogo wangu. Brother wako hapa kilinikuta kitu hicho hicho! Nimetoka o'level vizur sana (division two point 18) nikiwa nmetandaza B kwenye kombi ya PCB, hivyo kama kawaida nikaona advance nikasome PCB.
Nilipofika kule (nilisoma Mtwara tech) mambo hayakuwa kama nilivyotarajia..! Mambo yalikuwa magumu sana! Kwa mwanzo somo nililokuwa nalielewa vizur lilikuwa ni Biology pekee! Chemistry na Physics mambo hayakuwa mazuri kabisa! Yaani mambo yalikuwa yana-vapour kwa haraka mpaka nikaanza kuhisi nmerogwa (ingawa imani hizo siziamini!)
Ilifika kipindi form five ilikuwa nikisoma chemistry or physics ndani ya saa moja nmeshasahau kila kila kitu! Yaani mpaka definition haikai kichwani..! Nilichanganyikiwa kwakweli!
Bahati nzuri nilikuwa napenda kujichanganya na mabrother wa form six and so nikashare nao tatizo langu! Jamaa walinicheka sana (cause nao walipitia issue kama hizo) but walinisaidia kufanya utatuzi wa tatzo langu ingawa bado haikuwa the best solution..!
Namkumbuka bro wangu anaitwa boaz alisema "
Ubavu, angalia dogo, chuo wanataka principal mbili tu.! (kwa kipindi kile principal ilikuwa E) so chakalika upate E ya biology na chemistry then off you go to the university"
Kwa kipindi kile niliona hiyo ndo ilikuwa solution and so nikalikacha rasmi somo la physics..! Nikaamia kwa chemistry! Na kweli, muulize mtu yeyote aliyesoma PCMB (phy, chem, bios, or math) advance atakwambia.. Kuwa chemistry ndio somo la kukutoa cause huwa halikatai mtu!
Fortunately, necta ya form six nilipita kwenye tundu ya sindano kwa kutumia formula ya brother boaz kwani nilipata div three (ndipo pcb wengi wanapoangukia hapa) ya point 15 meaning nilikuwa nna D mbili za bios and chem! Hivi sasa nmemaliza chuo na nmepata kajikazi kakujishikiza!
Turudi kwako, mara nyingi sipendi kumpa mtu ushaur mmoja! Huwa napenda kumchambulia mtu pros and Con's za kila option ili mwenyewe ajue wapi ni kuzuri zaidi!
Moja, unaweza kutumia njia yangu ambayo baadae ilinikosti kwa vile physics nilikuja kupata F ila nikaenda chuo! Na sikuweza kufikia malengo ya wanaPCB wengi ya kusoma MD!, hapa unatakiwa pia uchague topics za kusoma pia..! Kwenye chemistry pitia sana physical chemisry, Inorganic chemistry pamoja na General chemisry... Hizi ndio mkombozi wako... Maana kama ukizikazia huwa hazichomoi! Hapa tafuta kitabu cha last papers kutoka mwaka 1987 mpaka 2006! Hiki ndio awe rafiki yako..!maswali yote ya topics hizo nilizokwambia inabidi uwe unayajua ndani nje..! Kuanzia data mpaka solutions! Organic chemistry! Asee huyu mdudu anavitu vingi sana.! Halafu maswali yake huwa hayatabiriki..! Zile conversion inatakuwa kuanzia temperature, catalyst mpaka pressure inayotakiwa ili reaction itake place! Kwa mm niliacha nayo! Ila kama unajiamini unaiweza.. Ukiweza kuimaster hii A ya chemistry inanukia cause organic chemisry hubeba 60%ya maksi zote kwa paper one na two..!
Biology yote inatakiwa iwe at the fingertip of your hand! Meaning swali lolote la topic yoyote inatakiwa usilifikilie zaidi ya dk moja..! Yaani ukishamaliza kulisom swali hakuna muda wa kurudia.. Inatakiwa uwe umeshajua muulizaji anataka nn kwenye swali hilo..! Pia ni muhimu kufupisha jibu lako kuwa fupi ila lenye ujazo wa haja.. Msahihishaji huwa analess than one minute kusahihisha swali moja so hawezi kuhangaika kutafuta jibu katikati ya essay lako! Majibu yawe in bulletin way hata kama swali ni la assay form! Kama ni swali la kudescribe ni lazima uchore mchoro! Kama ni explain ni lazima isizid mistari mitano ya jibu lako! (hapa kuna mengi ambayo siwezi kuyaandika yote so unaweza kuja pm nikupe namba tuongee..). Or
Mbili, unaweza kukaza zaidi! Tafuta likizo hata ya week moja, tulia fikilia ni kwann mambo yamekufika hapo ulipo?! Je ni strategy or materials yanayokufanya ushindwe kuperfom..? Mara nyingi huwa ni strategy..! Kwa maana shule za govt kwa advance ni msuli yatima (meaning unakomaa na materials wewe mwenyewe mpaka kinaeleweka!) so huwa inakuwa how you study and for how long ndicho kinacho-determine ufaulu wako..! Kuna jamaa yangu tulikuwa room moja, alikuwa anastrategy za ajabu sana..! Yeye alikuwa anasema, "
Ubavu advance mambo ni mengi sana and so unatakiwa urudie rudie kusoma hizi mambo mara nyingi iwezekanavyo..!" akandelea kusema "inatakiwa uwe umeimaliza syllabus yote ya advance tena ya masomo yote ndani ya week moja..!" wakati huohuo fahamu idadi na uzito wa vitabu vyiiliyopo advance! Mimi ilinishinda njia hii kwakweli"
Hapa nataka niseme neno kidogo!. Hii ndio njia ninayoona at least itakusaidia.. Baada ya kumaliza form six nilikuja kuelewa ni kwann hii ndio njia nzuri! Unajua mtu anavyotoka o'level huwa anaexpectation kusema kuwa "kama nmetoka kwenye masomo tisa na nikafaulu kwann nisifaulu nikiwa na masomo matatu tu!" thats totally wrong! Yaani advance sio ya kuifikilia kihivyo kabisa..! Mimi nilikuwa ni mmoja ya watu wanaoisema serikali kuwa wamekosea kwa kuruhusu watu walioferi form six kuruhusiwa kufundisha o"level kama amesoma deploma ya ualimu..! Ila kwa sasa nmeona ndio option nzuri, kwann nasema hivyo..! Advance mara nyingi mtu huwa afeli kwasababu ya kuto kusoma..! Bali huwa anafeli kwasababu ya kutokujua jinsi ya kulijibu swali la mtihani effectively..! Jamaa aliyepata div four ya advance ukimwambia akufundishe topic moja wapo... Utashangaa jinsi anavyoijua ndani nje... Tena mpaka na mifano..! But ndo hivyo unakuta necta anatoka na four...! Mtu huyu vitu anavijua sema jinsi ya kuviweka kwenye pepa ndo shida...! Unakuta anabeat around the bush mpaka muda unaisha..!
Sasa basi! Jaribu kufanya maswali mengi iwezekanavyo.. Tena sio ya vitabuni peke yake... Fanya mitihani mingi iwezekanavyo! Hapo utajihakikishia kufaulu!
Tatu, kama umeona kuwa hutoweza kutoka kwa njia hii ya advance, unaweza pia kuomba vyuo vya diploma vya afya na ukaacha hiyo advance kiroho safi tu! Tena ndo zinakaribia kufunguliwa sasa..! Njia hii ni nzuri kwa kuwa unakuwa na uhakika wa kutoka... Chuo kufeli ni kutaka mwenyewe tu.. Labda ukushike ugonjwa wa ajabu.. Wakati wa mtihani!
All in all! Advance sio sehemu ya kwenda kujaribu..! Inataka constant discipline ya muda..! Kuanzia unaingia siku ya kwanza mpaka unatioka siku ya mwisho! Elius kiyombo TO wa mwaka 2006 anamisemo yake..! Huwa anasema.. "Ukiwa advanve hakuna rangi utaacha ona" pia husema "siku ya kwanza kuingia form five wote huwa mnakuwa na div one ya point tatu, but huwa inapungua kulingana na aina ya maisha utakayoyaendesha mpaka necta inakufikia.. So inawezekana mwezi mmoja kabla ya necta ukawa umebaki na div one ile ile or umebaki na zero..!
Pia wakati unasoma jaribu kujifananisha na watu wa misuli mirefu..! Jaribu kukaa nao karibu cause watakupa changamoto ya kuongeza msuli wako...! Pamoja na usongo..! Kama unasoma boarding! (tena hapa ndio muhimu) na ngoja niandike kwa herufi kubwa ACHANA NA RATIBA YA SHULE, USIIFATISHE KABISA HII...! NI MBAYA NA HATARI KWA AFYA YAKO YA KUSOMA! Mi ratiba yangu ili kuwa ni kama ifuatavyo..! Naamka saa moja na nusu..! Mbili kamili nipo room kwenye meza yangu naanza misuli ya bios..! Mpaka saa nne muda wa uji nakuwa nmeshapitia topic mbili za bios pekee..! Kuanzia saa tano mpaka saa nane kamiri nakuwa nmeshapitia topic tatu za phy chemistry! Baada ya msosi nalala kuanzia saa kumi mpka saa kumi na mbili..! Then nakula msosi wa jioni..! Napiga story mpaka saa moja na nusu...! Mbili kamili nipo mezani kwenye room yangu misuli inaanza tena (kwa advance hasa watu wa pcbm usiku ndio unatakiwa uwe muda wa kusoma sana..! Unless otherwise usingizi uwe unakushinda nguvu) hapo ntasoma mpaka saa tano na dk 45 (huu ndo muda wa usingizi kuanza kusumbua..) nalala kwa saa moja mpaka saa sita na dk 45 nikiamka nnanguvu mpya..! Kuanzia saa saba kamili mpaka saa kumi na nusu alfajir ni mwendo wa kusoma tu..! Then nalala naamka saa moja tena kazi inaanza tena... Hii ni toka mwezi wa sita wa form five mpaka mwezi wa pili (kipindi chetu ndo papers zilikuwa zinafanywa muda huu) wakati wa necta
Na mwisho kabisa.. Jipatie muda mwingi wa kupumzika.. Ikiwezekana chagua jumamosi (kama wasabato) or jumapili kama waroma nk) or hata ijumaa (kwa waislamu) kuwa ni siku ya mapumziko ukikusanya nguvu..!
Mimi binafsi nilichagua ijumaa kwasababu huwa ni siku fupi sana..! And so ilikuwa ndo siku ya kulala..!
Kama we niwa day..! Uliza wengine...
Ubavu!