Nataka kuhama Dsm, nishauri niende Mkoa gani?

Lagertha

Senior Member
Joined
Mar 1, 2023
Posts
116
Reaction score
326
Salaam wanajamvi,

Naombeni ushauri wa kina, nataka kuhama jiji la Dsm je niende mkoa gani?

Wenye maisha rahisi, vyakula vya kutosha, niweze kufanya biashara pia kwa maana ya mzunguko wa pesa upo,

Tafadhalini mnishauri kwa upendo, nina vidonda vya tumbo.
 
Wewe ni mwanamke ? Je una mtaji kiasi gani ? Je una ujuzi upi nipe hayo majibu ila zaidi kama ni mwanamke pole sana na vidonda vya tumbo ,mimi ni daktari naaweza kukutibu kama hautajali uje kwanza mbeya nikutibu vidonda vya tumbo alafu ndiyo tuone utaenda mkoa gani badaye .
 
Utuambie kwanza unajishughulisha na nini/taaluma yako.
Mfano kama ni mkulima wa mazao ya kawaida au ya bustani mikoa ya nyanza za juu kusini itakufaa. Kama ni mvuvi nenda Mtwara, Tanga, Kagera, Kigoma, Katavi, Zanzibar n.k, kama ni fundi ujenzi,welding, selemala, plumbing n.k. mji unaojengeka kwa kasi hadi mafundi wanaringia kazi ni Dodoma, mmachinga nenda Mwanza, Mbeya, Arusha au baki tu Dar, kama wewe ni mjanja wa masoko, masuala ya Internet, kazi za mikono au utalii nenda Moshi/Arusha/Manyara/Morogoro.
Nyoosha maelezo ushauriwe. Kila raheli
 
Ni mama wa nyumbani anayetaka kuanza maisha mkoa mwengine tofauti na Dsm, anayeweza kufanya biashara ndogo ndogo kujiingizia kipato
 
Back
Top Bottom