Nataka kufungua mgahawa ambao utakuwa maalum kwa kuuza Biriani tu maeneo ya Kinondoni

Dec 13, 2012
67
352
Salaams wana jamvi.

Mimi ni mdau wa miaka mingi humu ila sio mara nyingi kuwa active lakini huwa napitia sana baadhi ya thread zinazohusu biashara na ujasiriamali.

Mimi naishi maeneo ya Kitunda relini na by profession ni Graphics designer ila tangu nikiwa kijana mdogo (teenager) miongoni mwa vitu napenda ni kupika.

Zaidi napenda sana na naenjoy kupika biriani na pilau. Nina kama miezi mitano sasa tangu nimeacha kazi kwa muhindi na kwa hiyari yangu, na sababu kubwa ni kutaka kuwa huru na kufanya mambo yangu binafsi bila mipaka ya muda wa kazi.

Nimefkiria kufanya biashara, na biashara ambayo imenijia kichwani ni biashara ya mgahawa ambayo itaspecify chakula cha biriani, au hata kama kutakuwa na nyongeza basi naweza kuongeza ila chakula kikuu kiwe ni biriani.

Nafahamu Kinondoni ina watu wengi wa “kishuwa” ambao biriani inaweza kuwa ni miongoni mwa vyakula wanavyopenda lakini nataka kufahamu zaidi je, availability ya chakula cha aina hiyo ipo? Na vipi kama nitaanza kufanya, inaweza kuwa yenye mafanikio kwangu?

Nakaribisha mawazo, fikra na hata uzoefu wa wadau waliopo maeneo hayo au hata recommendation ya maeneo gani yanaweza kuwa ni maeneo rafiki.

Naomba kuwasilisha na natanguliza shukrani zangu.
 
Mkuu wazo zuri, na nikupongeze kwa ujasiri wako wa kuacha ajira ili kujiajiri, pokea maua yako, ni wachache sana wanaweza hili...

Kwanza kuhusu mgahawa ku deal na aina mbili za vyakula ( Biriani na pilau ) Naona kijiwe( mgahawa) utafifia kwa namna fulani, kwasababu...

Biriani ni aina ya chakula chenye viungo vingi sana, huwezi kufululiza kula kila siku lazima tu utakinai... yaani vile viungo ndio vitakukinaisha au utapoteza hamu ya hiko chakula.

Chakula aina ya biriani kinafaa kuliwa mara moja moja sana kutokana na uwingi wa viungo vyake, kwaicho ukifululiza kuuza biriani kila siku, kuna asilimia nyingi za chakula kubaki.

Ushauri wangu, mgahawa wako usi base kwenye biriani na pilau tu, Weka vyakula vyakula vyote vya kiswahili na jitahidi kuwa m'bunifu.

Mfano : ugali unaweza kuweka na mboga kama dagaa, kisamvu cha karanga, matembele, maharage yaliyoungwa nazi, samaki / kuku / maini / nyama choma ( kimoja wapo kati ya hivyo ) bila kusahau na mrenda.

Wali mzuri wa mafuta uliotiwa nazi na mboga mboga nyengine zenye ladha.

Hivyo biriani na pilau ni extras tu maana hapa katikati ya week watu hawatakua na mzuka navyo kama nilivyokwambia biriani inakinaisha.

Zingatio : Jitahidi sana kua mbunifu jikoni, hakikisha kinatoka chakula chenye ladha / kitamu sana.

Mwisho : Ukitaka kufanikiwa kwenye hii biashara cheza sana na social media hasa Instagram, inabidi uwe mtundu hasa wa kuandaa contents, kuandika captions zenye mtiririko mzuri unaovutia na usio chosha n.k

Naamini utafanikiwa, kila la kheri kwenye safari yako. Kwakua mimi naishi kinondoni, nitakua mteja wako wa kudumu.
 
Mkuu wazo zuri, na nikupongeze kwa ujasiri wako wa kuacha ajira ili kujiajiri, pokea maua yako, ni wachache sana wanaweza hili...

Kwanza kuhusu mgahawa ku deal na aina mbili za vyakula ( Biriani na pilau ) Naona kijiwe( mgahawa) utafifia kwa namna fulani, kwasababu...

Biriani ni aina ya chakula chenye viungo vingi sana, huwezi kufululiza kula kila siku lazima tu utakinai... yaani vile viungo ndio vitakukinaisha au utapoteza hamu ya hiko chakula.

Chakula aina ya biriani kinafaa kuliwa mara moja moja sana kutokana na uwingi wa viungo vyake, kwaicho ukifululiza kuuza biriani kila siku, kuna asilimia nyingi za chakula kubaki.

Ushauri wangu, mgahawa wako usi base kwenye biriani na pilau tu, Weka vyakula vyakula vyote vya kiswahili na jitahidi kuwa m'bunifu.

Mfano : ugali unaweza kuweka na mboga kama dagaa, kisamvu cha karanga, matembele, maharage yaliyoungwa nazi, samaki / kuku / maini / nyama choma ( kimoja wapo kati ya hivyo ) bila kusahau na mrenda.

Wali mzuri wa mafuta uliitiwa nazi na mboga mboga byengine zenye ladha.

Hivyo biriani na pilau ni extras tu maana hapa katikati ya week watu hawatakua na mzuka navyo kama nikivyokwambia biriani inakinaisha.

Zingatio : Jitahidi sana kua mbunifu jikoni, hakikisha kinatoka chakula chenye ladha / kitamu sana.

Mwisho : Ukitaka kufanikiwa kwenye hii biashara cheza sana na social media hasa Instagram, inabidi uwe mtundu hasa wa kuandaa contents, kuandika captions zenye mtiririkk mzuri unaovutia na usio chosha n.k

Naamini utafanikiwa, kila la kheri kwenye safari yako. Kwakua mimi naishi kinondoni, nitakua mteja wako wa kudumu.
Asante sana kwa maua na pia kwa ushauri na nimekuelewa vyema. Nafkiria nikiweka huo mgahawa basi kitu “biriani” iwe ndio brand kwaiyo ningetamani iwepo siku zaidi ya moja, ikiwepo walau siku 3 ndani ya wiki (Ijumaa, Jumamosi na Jumapili) itakuwa safi zaidi. Kwa mfano Samaki Samaki ni brand lakini mbali na samaki, pia anauza kila kitu. Halkadhalika Cape Town Fish Market anauza hadi pork (Sina nia ya kuwa na kitimoto though) ingawa jina lake limejieleza lipo kisamaki zaidi. Kwenye hivyo vyakula vengine pia nazingatia mawazo yako.
Naendelea kupokea ushauri na I hope ndani ya wiki 2 nikafanye survey kwa sababu kwa mfano nyama choma almost kila pub/bar zinakuwepo kwaiyo nitajaribu kuangalia namna gani wanafanya ili nifanye kilicho bora zaidi. Halkadhalika kwenye vyakula vya kawaida kama ugali, wali na local foods nyengine.
Natanguliza shukrani.
 
Back
Top Bottom