Nataka kufungua ofisi ya kuuza na kununua pikipiki amabazo zimeishatumika

dicloppa

JF-Expert Member
Jan 9, 2016
278
400
Wakuu habari! bila ya kupoteza wakati niende kwenye maada husika wazo langu ni kufungua ofisi ya kuuza na kununua pikipiki amabazo zimeishatumika mtaani(used)

Ili ofisi iwe imekamilika kwa upande vibali ni taratibu zipi napaswa kuzifuata ili kupata vibali na pia ni vibali gani napaswa kuwa navyo?

Mwenye kufahamu hilo naomba anifahamishe. Natanguliza shukrani
 
Ungefupisha na kuandika pikipiki used.
 
Jifunze kwanza uchunguzi mkali wa piki piki zilizotumika.

Usije ukaenda jela kwa kesi ya uhalifu.

Piki piki zinaibiwa sana. Usije ukauziwa piki piki za wizi
Kununua pikipiki ya wizi maana yake unakuwa umenunua pikipiki ambayo haina nyaraka nadhan nimeeleweka vyema

Ni upumbavu kiwango cha lami kununua pikipiki isiyo na nyaraka
 
Leseni ya biashara ndio utahitaji.
Maswala ya OSHA , na Zimamoto kibongo bongo naona kama bado kwa biashara hiyo. So hapo cha msingi lipia tu fire extinguishers, endelea na kazi.
 
Unao mtaji wa kutosha nikuelekeze kampuni ambayo unaweza kununua PIKI piki used. Hadi ukachoka na pikipiki zao zipo full documents maana ni kampuni inayotambulika na serikali...!
 
Kununua pikipiki ya wizi maana yake unakuwa umenunua pikipiki ambayo haina nyaraka nadhan nimeeleweka vyema

Ni upumbavu kiwango cha lami kununua pikipiki isiyo na nyaraka
Wewe una mashine ya kutofautisha kati ya nyaraka feki na halali?maana kuna wezi wana uwezo wa kufoji nyaraka.
 
Ingia anza biashara.
Utahitaji Fundi wa Kukagua kiwango cha uimara wa pikipiki ili isaidir bei ya Kununua na kuuza.
Usipoteze muda mwingi na ushauri kuna watu wataponda kila kitu.Ukishaa za Changamoto utazitatua huku unaendelea.
Anza kazi
 
Back
Top Bottom