Mgahawa wa kwanza wenye uwezo kamili wa kujiendesha kwa kutumia Akili Mnemba (AI) wafunguliwa

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Roboti zimefika... huko Pasadena, Kusini mwa California.

Mwishoni mwa Desemba 2023, CaliExpress ilifungulia Mgahawa wa kwanza kabisa duniani wenye uwezo kamili wa kujiendesha kwa kutumia AI - Artificial Intelligence (Akili Mnemba). Mteja anatakiwa kutoa oda yake mapema ili kupata huduma ya chakula. Mgahawa huo ni wakutengenza chakula aina baga (Burger).

Mgahawa hutumia baadhi ya teknolojia zenye ubunifu zaidi inayopatikana kwa sasa ili kujiendesha katika vituo vyote vya kupika na kukaanga. Wageni wanaweza kuona roboti wote wanapoandaa chakula kwa maagizo yao maalum.

Teknolojia hizi mbalimbali za kuunda mgahawa wa kujiendesha (automated) zaidi duniani ni mwisho wa miaka mingi ya utafiti, maendeleo, na uwekezaji. Teknolojia inayotumia AI, na utaratibu wa kuagiza na kupika kwa kutumia roboti, inawezesha minyororo mikubwa inayowalisha watu wa Marekani kuboresha sana ubora, ufanisi, na kasi.

 
Back
Top Bottom