wakuu heshima mbele sana
kwa mnaojua,nisaidieni kunipatia vigezo ambavyo vinaweza kumfanya mtanzania kufanya kazi usalama wa taifa.mtaani nimesikia wakisema hizi kazi huwa unachaguliwa tangia ukiwa shule ya msingi au sekondari huwezi kujipeleka mwenyewe kuomba hizi kazi.je ni kweli?je ni kweli ni lazima upitie mafunzo ya kijeshi kabla ya kujiunga usalama wa taifa?
mimi napenda sana kufanya kazi na usalama wa taifa je siwezi kujiunga uko baada ya miaka 2 nikimaliza masomo yangu(nina miaka 28,nafanya masters sasa).
mods naomba muiache kidogo halafu mnaweza kuiamisha panapostahili.
Nchi kama marekani kazi hizo hutangazwa na tangazo huwa hivi.
This job is For the extraordinary individual who wants more than a job, this job will challenge the deepest resources of your intelligence, self-reliance, and responsibility.
It demands an adventurous spirit, a forceful personality, superior intellectual ability,toughness of mind and the highest degree of integrity.
It takes special skills and professional discipline with an excellent academic record to produce results. (Tanzania???mhhhh)
You will need to deal with fast-moving, ambiguous, and unstructured situations that will test your resourcefulness to the utmost.
All applicants must successfully complete a thorough medical and psychological exam, a polygraph interview, and an extensive background investigation.
Idara hiyo hujulikana kama Intelligence maana yake ni sehemu ya watu wenye akili sana sio wajinga wajinga waliofeli masomo au ambao maisha yamewapiga mwereka sasa wanatafuta popote pa kujishika.Watu hao intelligent huwa wana akili kuanzia darasani hadi nje.Waweza kuwajaribu kama wakimbiaji wakakimbia sana.Ukawajaribu kama waimbaji wakaimba sana.Ukawaingiza darasani wakafaulu mno.Ni watu ambao karibu ukimweka kila eneo aweza fanya vizuri kushinda hata walio katika eneo hilo.Ni watu above avarages almost katika maeneo mengi.
Nchi zingine Ukiwa na mtoto kwa mfano ambaye anajiweza mno kimasomo na anaweza kuongoza mfano shuleni vizuri kama kiongozi wa darasa au shule ,na akanyakua zawadi shuleni nyingi kwenye maeneo mengi ya darasani na nje ya darasa mfano michezo,skauti,n.k kwa muda mrefu akiwa anaongoza darasani na nje yawezekana akafaa baadaye usalama wa Taifa mlee na umkuze vizuri kitabia n.k unatakiwa mzazi u- mshauri ajiunge na jeshi lolote baadaye akimaliza digrii zake vizuri na akapata pass nzuri.mengine waachie wengine watajuana naye mbele kwa mbele na si lazima arudi kukwambia kuwa sasa niko usalama wa taifa.
Wanaposema mtoto hutizamwa kuanzia akiwa mdogo ni kuwa mwenye akili sana anakuwa hivyo kuanzia mdogo na anaendelea hivyo (consistency) hadi utu uzima anapomaliza digrii zake.Na juhudi zake na kujituma hupimwa kuanzia mdogo hadi anamaliza digrii zake ndani na nje ya Darasa.Na tabia hutizamwa toka mdogo ndani na nje ya darasa kabla ya kufikia uamuzi wa kuona kweli afaa kuitwa intelligent anayeweza kuingizwa Intelligence unit baada ya kutizamwa vigezo vingine.
Nchi iwe na utaratibu wa kutangaza au ule wa siri lakini cha msingi vigezo hivyo hubidi vizingatiwe visipozingatiwa huwi na intelligence unit bali dull unit ambayo madude kama ya Richmond na dowans ni rahisi tu kupita sababu akina richmond wanakuwa na akili kuliko ma-dull yaliyoko usalama wa taifa yaliyoajiriwa bila vigezo vya intelligence.