Natafuta Kazi Usalama Wa taifa

Natafuta Kazi Usalama Wa taifa

Status
Not open for further replies.
Well, kwanza hao sio "wenzetu" katika masuala ya Usalama tunayokabiliana nayo. Kuiga kunya kwa tembo kutakuwepo kama tutajifanya tunahitaji hizo idara zote.

Nitajie a couple credible national security threats Tanzania, zaidi ya kulinda Kikwete asipigwe mawe tena vijijini usiku.

Mkuu nimekupata fika ! Na kwa hilo UWT idumuuuu...

UWT ni kurugenzi iliyochini ya Katibu Mkuu ofisi ya Rais,katibu mkuu ofisi ya rais ndiye mwajiri.Peleka maombi yako ikulu,kama utafaa au wanakuhitaji watakuchukua.
 
Kama walitangaza wafanyakazi wenzake bila kutaja taasisi, kwanini watu wasijue ni Shoe shiners wenzake na wahisi ni usalama wakati Marehemu alikuwa shoe shiner. Nadhani hata huyo Mzee alikuwa anajulikana ni Usalama.

Kuweka utaratibu wa kujitolea ndio watu waajiriwe, basi kila mtu atajitolea, manake huko kujitolea ndio kutakuwa chanzo cha kazi.

Mkuu p53, kwani kazi unayotaka ni usalama tu?,kwanini usitafute na kazi nyingine?. Kutokea kwa hiyo kazi nyingine dhamira,utendaji na ulivyo inaweza kuwa sababu ya kuja kuwa usalama. Manake hawa jamaa wako kila kona, wakikuona unafaa watakupendekeza.

..nilikuwa namaanisha baadhi ya usalama orijinal walivyo wasiri!!!...walisema mwajiri wake .., na watumishi wenzake..,siunajuwa shoeshiners hana mwajiri anajiajiri ...plus mimi kama mtu mzima nilikuwa najuwa ...through my own sources...
 
Usitoke nje ya mada bro/sister.Jamaa ana uliza atapataje hiyo kazi na kama kozi zao zina mambo ya kijeshi(mafunzo).
Kwa kuwa jamaa inaonekana anaipenda hiyo kazi,namshauri aweke mawasiliano yake hadharani (sio username yake ya hapa JF)ili wanaohusika wamtafute na naamini akiwa trainned atakuwa mzuri kwa sababu anaipenda toka moyoni na kama ana dhamira ya kweli aweke sababu walao tano za kutaka kufanya kazi hiyo ukiondoa anayosema anaipenda.
Akishindwa kufanya hivyo,kuna mambo mawili ama tayari ni USALAMA anataka kujua watu wanauchukuliaje au wanauelewaje usalama na au Anataka kujua 'wenzake' wako cautious vp kuhusu utoaje na utafutaji wa habari za kiusalama

sasa mkuu nikishaweka mawasiliano yangu hadharani huo hautakuwa usalama tena!
 
Kama kwa umri ulio nao hawajakutafuta ujue hawakuhitaji. Hivyo usipoteze muda wako kupeleka CV. Huwa wana usalama wana targets zao, and it seems you are not among their targets. Halafu huwa upo kindugundugu sana, je una nduguyo aliye msalama na ana record nzuri ya kazi yake hiyo??? Kwa sababu siku hizi hakuna JKT huwa wanatumia mbinu nyingine kuwapata vijana ambazo kwa maadili ya kazi si vema kuziweka hapa. Hata ukienda pale reception HQ Kijitonyama yule receptionsit hapaswi kukupa wewe details. Sana sana utaacha taarifa au barua zako pale na watakuambia utatafutwa au utajibiwa. Sidhani kama utaruhusiwa kuonana na ofisa pale kwa jambo hilo!!!

Lakini pia hebu weka motive yako hapa ya kutaka kuingia huko usalama!!!! That is ni msukumo gani unao hadi unataka ujiunge huko kabla wao hawajakutafuta????
 
sasa mkuu nikishaweka mawasiliano yangu hadharani huo hautakuwa usalama tena!

Nilisema kwamba tayari wewe ni usalama,kwani kuweka mawasiliano hapo na wakakutafuta ina shida gani lakini kwa kuwa wewe ni usalama itakusumbua kuweka namba zako hapa.teteheeee niambie mh.unafanyia kitengo kipi?
 
Nchi kama marekani kazi hizo hutangazwa na tangazo huwa hivi.

“This job is For the extraordinary individual who wants more than a job, this job will challenge the deepest resources of your intelligence, self-reliance, and responsibility.

It demands an adventurous spirit, a forceful personality, superior intellectual ability,toughness of mind and the highest degree of integrity.

It takes special skills and professional discipline with an excellent academic record to produce results. (Tanzania???mhhhh)

You will need to deal with fast-moving, ambiguous, and unstructured situations that will test your resourcefulness to the utmost.

All applicants must successfully complete a thorough medical and psychological exam, a polygraph interview, and an extensive background investigation.”

Idara hiyo hujulikana kama Intelligence maana yake ni sehemu ya watu wenye akili sana sio wajinga wajinga waliofeli masomo au ambao maisha yamewapiga mwereka sasa wanatafuta popote pa kujishika.Watu hao intelligent huwa wana akili kuanzia darasani hadi nje.Waweza kuwajaribu kama wakimbiaji wakakimbia sana.Ukawajaribu kama waimbaji wakaimba sana.Ukawaingiza darasani wakafaulu mno.Ni watu ambao karibu ukimweka kila eneo aweza fanya vizuri kushinda hata walio katika eneo hilo.Ni watu above avarages almost katika maeneo mengi.

Nchi zingine Ukiwa na mtoto kwa mfano ambaye anajiweza mno kimasomo na anaweza kuongoza mfano shuleni vizuri kama kiongozi wa darasa au shule ,na akanyakua zawadi shuleni nyingi kwenye maeneo mengi ya darasani na nje ya darasa mfano michezo,skauti,n.k kwa muda mrefu akiwa anaongoza darasani na nje yawezekana akafaa baadaye usalama wa Taifa mlee na umkuze vizuri kitabia n.k unatakiwa mzazi u- mshauri ajiunge na jeshi lolote baadaye akimaliza digrii zake vizuri na akapata pass nzuri.mengine waachie wengine watajuana naye mbele kwa mbele na si lazima arudi kukwambia kuwa sasa niko usalama wa taifa.

Wanaposema mtoto hutizamwa kuanzia akiwa mdogo ni kuwa mwenye akili sana anakuwa hivyo kuanzia mdogo na anaendelea hivyo (consistency) hadi utu uzima anapomaliza digrii zake.Na juhudi zake na kujituma hupimwa kuanzia mdogo hadi anamaliza digrii zake ndani na nje ya Darasa.Na tabia hutizamwa toka mdogo ndani na nje ya darasa kabla ya kufikia uamuzi wa kuona kweli afaa kuitwa intelligent anayeweza kuingizwa Intelligence unit baada ya kutizamwa vigezo vingine.

Nchi iwe na utaratibu wa kutangaza au ule wa siri lakini cha msingi vigezo hivyo hubidi vizingatiwe visipozingatiwa huwi na intelligence unit bali dull unit ambayo madude kama ya Richmond na dowans ni rahisi tu kupita sababu akina richmond wanakuwa na akili kuliko ma-dull yaliyoko usalama wa taifa yaliyoajiriwa bila vigezo vya intelligence.

Yoooote sawa sawa mkulu tena umepiga Gujarati, hasa hapo mwisho..
 
P53
Join Date: Wed Feb 2009
Posts: 58
Rep Power: 21

Thanks: 1
Thanked 12 Times in 9 Posts
Credits: 927,994

Naona kazi uliyotumwa unaelekea kuimaliza... nilichobakia ni kwenda kuripoti tu, I love you!!!
 
Today, 12:22 AM
Phillemon Mikael
This message has been deleted by Phillemon Mikael.

Miongoni mwa vitu vinavyoonekana kwenye hii thread.
 
Naona kazi uliyotumwa unaelekea kuimaliza... nilichobakia ni kwenda kuripoti tu, I love you!!!

kipimo chako feki.tangia 2006 naingia jf kama guest,sasa kwanini ugeni wangu ukushangaze?
 
Nilisema kwamba tayari wewe ni usalama,kwani kuweka mawasiliano hapo na wakakutafuta ina shida gani lakini kwa kuwa wewe ni usalama itakusumbua kuweka namba zako hapa.teteheeee niambie mh.unafanyia kitengo kipi?

tumia logic mkuu yaani unasema niweke mawasiliano yangu,nikishaweka si kila mtu atanijua?nikijulikana nani atanipa kazi ya usalama tena?mimi siko kwenye kitengo mkuu kama wewe uko huko nielekeze na mimi nitaingiaje,ndiyo shida yangu kubwa.
 
kipimo chako feki.tangia 2006 naingia jf kama guest,sasa kwanini ugeni wangu ukushangaze?

teh teh teh teh,

sasa assignment imekushinda, wakubwa wako wanakuangalia shauri yako!
 
...unamchongea mwenzako apelekwe Nachingwea!
 
Nilisema kwamba tayari wewe ni usalama,kwani kuweka mawasiliano hapo na wakakutafuta ina shida gani lakini kwa kuwa wewe ni usalama itakusumbua kuweka namba zako hapa.teteheeee niambie mh.unafanyia kitengo kipi?

Naona kazi uliyotumwa unaelekea kuimaliza... nilichobakia ni kwenda kuripoti tu, I love you!!!

Hahaha, uko nyuma nilisema something is not right about this thread!

-uuuuum uuum umm-
 
Hahaha, uko nyuma nilisema something is not right about this thread!

-uuuuum uuum umm-

...umeshtukia eeh?, 'codename' p53 😀, what a giveaway, ...kitengo tofauti na firearm specialists, kina C12...(?)
 
Tathmini yangu ni kwamba mjadala wa namna ya kupata kazi Usalama wa Taifa umekuwa na sura nyingi zenye kupingana. Baadhi ya masuala yanaonekana ni ya kufikirika zaidi. Kama alivyo P53 nami ningependa kupata kazi Usalama wa Taifa kwa sababu hizo hizo za uzalendo kwani naamini chombo hiki kina nafasi muhimu ya kujenga taifa. Miongoni mwa mikanganyiko niliyoipata ni kama ifauatavyo:-

SHY anasema Mtanzania ataajiriwa Usalama wa Taifa baada ya kutoa taarifa fulani fulani kuhusu mambo fulani au kuomba magazetini kisha atajikuta yuko Usalama wa Taifa.

SHAYCAS anatuambia kama unataka kazi huko kamwone au wasiliana na mtu anayefanya kazi au aliyewahi kufanya kazi huko.

CHUMA anatuaelekeza kuwa kuingia Usalama wa Taifa hakuhitaji ‘connections' kwa sababu utaratibu mpya wa sasa waombaji kazi Usalama wa Taifa huanza kwa kuajiriwa kama wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani.

DISSOFFICERREC anasema kazi za Usalama wa Taifa hazitoki magazetini.

PHILLEMON MIKAEL anatueleza kuwa Waziri Mkuu MIZENGO PINDA alipokuwa mwaka wa kwanza Mlimani ( chuo Kikuu cha Dar es salaam) alianza kwa ' assignment' kupeleka taarifa msasani na baada ya kumaliza chuo akapelekwa Ikulu. Hivi hizo ‘assigments' hazikuwa za siri kama utaratibu wa kazi za namna hiyo?

Kuna wanaotuambia ili kupata kazi Usalama wa Taifa tuwasiliane na kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama au Makamanda wa Polisi.

Yupo anayesema Usalama ni ya watu wa Ikulu pekee hapo hapo anatusihi tuombe kazi huko.

Lakini pia katika ya mjadala tunaambiwa kuwa kama shuleni ulikuwa mbumbumbu huwezi kuajiriwa na chombo cha intelijensia.

Vilevile katika mjadala huu imejitokeza kuwa Usalama wa Taifa wana ‘target' zao na kama wewe siyo lengo kamwe huwezi kuchukuliwa.

Katika maelezo mengine ni mchanganyiko wa hapa na pale!!! Hivi katika mjadala huu ni nani mkweli ili anisaidie na mimi kuingia huko?

KUKIRI KWAMBA JAMBO SILIFAHAMU SI UPUMBAVU BALI NI UKOMAVU WA AKILI.
 
Tathmini yangu ni kwamba mjadala wa namna ya kupata kazi Usalama wa Taifa umekuwa na sura nyingi zenye kupingana. Baadhi ya masuala yanaonekana ni ya kufikirika zaidi. Kama alivyo P53 nami ningependa kupata kazi Usalama wa Taifa kwa sababu hizo hizo za uzalendo kwani naamini chombo hiki kina nafasi muhimu ya kujenga taifa. Miongoni mwa mikanganyiko niliyoipata ni kama ifauatavyo:-

SHY anasema Mtanzania ataajiriwa Usalama wa Taifa baada ya kutoa taarifa fulani fulani kuhusu mambo fulani au kuomba magazetini kisha atajikuta yuko Usalama wa Taifa.

SHAYCAS anatuambia kama unataka kazi huko kamwone au wasiliana na mtu anayefanya kazi au aliyewahi kufanya kazi huko.

CHUMA anatuaelekeza kuwa kuingia Usalama wa Taifa hakuhitaji ‘connections’ kwa sababu utaratibu mpya wa sasa waombaji kazi Usalama wa Taifa huanza kwa kuajiriwa kama wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani.

DISSOFFICERREC anasema kazi za Usalama wa Taifa hazitoki magazetini.

PHILLEMON MIKAEL anatueleza kuwa Waziri Mkuu MIZENGO PINDA alipokuwa mwaka wa kwanza Mlimani ( chuo Kikuu cha Dar es salaam) alianza kwa ‘ assignment’ kupeleka taarifa msasani na baada ya kumaliza chuo akapelekwa Ikulu. Hivi hizo ‘assigments’ hazikuwa za siri kama utaratibu wa kazi za namna hiyo?

Kuna wanaotuambia ili kupata kazi Usalama wa Taifa tuwasiliane na kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama au Makamanda wa Polisi.

Yupo anayesema Usalama ni ya watu wa Ikulu pekee hapo hapo anatusihi tuombe kazi huko.

Lakini pia katika ya mjadala tunaambiwa kuwa kama shuleni ulikuwa mbumbumbu huwezi kuajiriwa na chombo cha intelijensia.

Vilevile katika mjadala huu imejitokeza kuwa Usalama wa Taifa wana ‘target’ zao na kama wewe siyo lengo kamwe huwezi kuchukuliwa.

Katika maelezo mengine ni mchanganyiko wa hapa na pale!!! Hivi katika mjadala huu ni nani mkweli ili anisaidie na mimi kuingia huko?

KUKIRI KWAMBA JAMBO SILIFAHAMU SI UPUMBAVU BALI NI UKOMAVU WA AKILI.

Nani mwenye sifa za kufanya kazi Usalama wa Taifa

Namuunga mkono FIKRA MBADALA

Natumani P53 pamoja na baadhi ya wenye nia ya dhati ya kufanya kazi Idara ya Usalama wa Taifa wameachwa njia panda ndani ya mjadala huu wenye majibu mengi yenye kuleta mkanganyiko. Wanajamiforums wenzangu kuna hoja nyingi za kupingana ambazo mimi nadhani tukiri kuwa inawezekana hatukifahamu chombo hiki vizuri pengine ni kwa sababu majukumu na wajibu wake kikatiba ni ya usiri uliopindukia sawa na vyombo vya namna hiyo duniani kote.

Mimi naona tuachane na majadiliano haya na tulenge kwenye mijadala ambayo ni ‘positive’ na yenye kuwasaidia wanajamii hasa maskini wanaoendelea kukandamizwa na serikali ya CCM.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom