Natafuta kazi Usalama wa Taifa,hata leo naomba mnipe tena naomba mnipe mapema
Nahitaji kazi ambayo nitaifanya kwa malipo madogo ila kwa ajili ya wanajamii
Nataka kuwasaidia kuwajua kwa undani wale waliochukua Pesa za EPA ili wajulikane
Nataka niajiliwe ili nionane na Rais na nimwambie yaliyo moyoni mwa watanzania
Nataka kazi usalama ili na mie nichukue pesa za EPA na niwagawie watanzania Masikini
Nataka tu sababu najua nikiwaomba pesa kwa njia ya kawaida hawatanipa.
Nafuta kazi ili niwape watanzania habari wanazotaka kujua
Niko tayari kufanya nao kazi kwa masharti ya uwazi na ukweli
Nataka Rais Ajue kwamba watu wanafanya ufisadi wa khali ya juu kwasababu ni rafikize
Nataka nimwambie Rais jinsi wachache wanavyowadharau walio wengi
Nataka nimwambie Rais ni watu wangapi mpaka sasa ni mafisadi wakubwa
Nataka kazi usalama ili nimjue vizuri rais wetu na tabia yake ya maamuzi
Nataka kazi usalama ili nifanye uchunguzi kuhusu BOT,
Nataka nimjue mmiliki wa Kagoda alipewa shilingi ngapi ?
Nataka niwajue waliorudisha Pesa za EPA mpaka sasa
Nataka kazi Usalama ili niwaambie watanzania ukweli ni wapi alipo Balali
Nataka kazi Usalama wa taifa ili nitoe majibu kuhusu Chenge
Natafuta kazi usalama ili niwaambie jinsi Dili ya RDC ilivyosukwa
Natafuta kazi ili nijue je Rais anawachukuliaje walihsuika na Richmond
Nataka kujua ni kwanini serikali hawatoi majibu ya Ripoti ya Richmons na EPA
Natafuta kazi siyo kwa ajili ya kumlinda Kada wa CCM wala kiongozi
Natafuta kazi ili kulisnda heshima ya nchi yetu
Natafuta kazi ili nchi hii iwathamini wafanyakazi na wakulima
Niko tayari kwa mshahara mdogo ila niwe huru kuwaambia wananchi
Ndiyo nataka Kazi Usalama wa Taifa na nataka Nafasi ya Ukurugenzi ndiyo ninayo itaka
Mpaka hapo ushapoteza sifa tayari.
wakuu heshima mbele sana
kwa mnaojua,nisaidieni kunipatia vigezo ambavyo vinaweza kumfanya mtanzania kufanya kazi usalama wa taifa.mtaani nimesikia wakisema hizi kazi huwa unachaguliwa tangia ukiwa shule ya msingi au sekondari huwezi kujipeleka mwenyewe kuomba hizi kazi.je ni kweli?je ni kweli ni lazima upitie mafunzo ya kijeshi kabla ya kujiunga usalama wa taifa?
mimi napenda sana kufanya kazi na usalama wa taifa je siwezi kujiunga uko baada ya miaka 2 nikimaliza masomo yangu(nina miaka 28,nafanya masters sasa).
mods naomba muiache kidogo halafu mnaweza kuiamisha panapostahili.
Unaweza kumwona MH.HASSI KITINE,ATAKUAMBIA MENGI ILA INAONEKANA WEWE NI MWOGA WA MAFUNZO YA KIJESHI AU UNA MTIZAMO HASI NA JESHI.
Basic training for (TISS) is nine months which comprises of "military"training,how to secure info and to protect it against un authorized personnel + much more to keep you fit for the job.
Habari za mtaani ulizosikia zaweza kuwa na ukweli fulani. Nafahamu jamaa mmoja anafanya kazi usalama wa taifa. Process yake alifuatiliwa long time tokea anasoma Tabora boys na watu hawa waliokuwa wanamfuatilia walikuwa makini; maana hata alipotoka nje ya Dar walimfuatilia pia. Ila jamaa alikuwa Scout na alifanya vyema alivyokuwa Scout. Suala la Jeshini sikujui.
Ila kwa siku kila kitu hela, system ilishaoza; kama una hela mbona kila sehemu unapenya bwerere tu. Ndio maana kwa sasa Bongo wafanyakazi asilimia kubwa hawana sifa ya kufanya hizo kazi; sababu wamezipata kwa hongo na ndio maana uvurundo kila siku. But keep trying; u never know what happens and u gotta nothing to loose though!
Mkuu jipe moyo tu kila kitu kinawezekana ni wewe tu kujitahidi na kuwa na nia na kitu unachotaka kufanya ni hivyo tu!!
Shaycas,
Unamaanisha watu wanaotaka kazi Usalama wa Taifa Tanzania wakapange mstari nyumbani kwa mstaafu Mkurugenzi wa Usalama, Hassi Kitine, kwa mazungumzo ya faragha, ndio wewe ulivyopata kazi hivyo huko Usalama? Na kama mtu hamjui Kitine akamwone nani, Apson? Hakuna utaratibu rasmi, sio?
Mjomba, usifikiri kila mwananchi ana access na the Apson's and the Kitine's of the world. Hivi mbona watu wengine wako so out of touch?
Eti unafundishwa "how to secure info and to protect it against un authorized personnel"!
Ndio ukachero huo uliofundishwa huko?
huo ndiyo ukweli wenyewe.kama wazee wako hawana jina basi kuwaona hao wakulu ni ndoto.
Nakubali.
Lakini sister brother p53, hata kama ungekuwa na jina la Baba wa matawi ya juu, au mtoto wa masikini, hutakiwi kukubali kupitia kwa watu maarufu, the Apson's and the Kitine's of the world, ili upate kazi sehemu kama Usalama wa Taifa. Ndio ufisadi wenyewe huo. Kwamba, my point is, p53, mambo ya connection connection na kujuana juana haya nishai. Mimi hapa nilipo sitaki kujuana na Kitine au Apson hata kama ningekuwa na access nao, hata kama wao ndio the go-to guys wa kukutafutia kazi Usalama. Sitaki, sitaki kuwajua. Wakae na ukuu wao na utajiri na umaarufu wao, waanze mbele!
Kwa nini tusijenge nchi ambayo sio lazima uka kiss ass kwa Kitine ili akuunganishie kazi Usalama wa Taifa? Yani mimi siwezi, siwezi, sijui ni kiburi cha kutotaka kuuza utu wangu, lakini sitaki.
Huyu Shycass anaweza kuwa na Kitine au jamaa yake fulani ambae anaweza kumuunganishia mahala akapeta, lakini ambacho hakijui ni kwamba mtoto wake Shycass akija baadae anaweza kuwa hamjui mtu, kwa hiyo yeye, kizazi cha baadae, atapata shida, kwa hiyo tusipojenga mazingira ambayo hayajitaji kujuana kwa kweli si poa kwa nchi yetu.
So, to hell with kujuana na the Hassi Kitine's of the world. Screw that!
how and why?
...unaona sasa, ushapoteza sifa ya pili hiyo kwa hilo swali lako...
duu mkuu kama nyie ndiyo ma interviewer wenyewe basi kazi ipo!