Natafuta Kazi Usalama Wa taifa

Natafuta Kazi Usalama Wa taifa

Status
Not open for further replies.
P53 unataka ufanye kazi usalama wa taifa kuna nini?...Una Ajenda gani? kuna lipa au? au unapenda kuwa shushu? kama una akili zako Timamu tafuta kazi ingine ya kufanya na si ya kazi ya kuchunguza watu. ni kazi ambayo at the end hutokuwa na raha nayo.

Pili moja ya ABC za kutaka kazi sehem ni kujua sehem au kampuni hio inadeal na nini...then vema ukaanza kujiandaa mapema incase for interview.

Nakubaliana na Kuhani, huu utaratibu usio rasmi ambao tumejijengea ya kuwa huwezi pata kazi sehem hadi ujuane na mtu si utaratibu mzuri na sie watafuta kazi tunajijengea mazingira ya kutojiamini ya kuwa unaweza pata kazi pasina connections.

Kama alivyosema shy, kila ukiona kazi Gazetini au Mtandaoni au kwa juhud zako binafsi za kupita maofisini na kuacha CV yako, nafikiri unaweza jikuta unaitwa na Hao the so called usalama wa Taifa. Wala kuingia Usalama hapahitaji connections...kwa utaratibu mpya wa sasa Usalama wengi huajiriwa kama wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani, from there then wanakuita kukuuliza kuwa kama unaweza fanya kazi nao, ukikubali watakufanyia uchunguzi wao, ukipita ajira umepata, na Hasa hizi kwa Proffessionals kama wewe unaefanya masters...

hao unaosikia mtaani, ni usalama wasio na elimu(wengi wao huishia form 4 au 6) au wale ambao ndugu zao au Jamaa zao wapo huko then wao ndio wanaakuuunganisha, kwani kazi ya kuchunguza inakuwa rahisi kwao, kwani tayari yeye na familia na rafiki wote washachunguzwa....

Bahati Mbaya wenzetu nchi zilizoendelea wanachukua wasomi na vipanga, sie tunachukua vijana walioishia ,F4 au F6 kuogopa kuhojiwa mara kwa mara na wasomi, maana tushazoea YES kila mara. huu ni kwa uzoefu wangu wa baadhi ya watu ambao walikuwa wakisemwa usalama wa taifa then wengi wao wanaishia F4/F6.

chuma umenipa mwanga wa kutosha mkuu.kuhusu swali lako:ukweli ni uzalendo ndiyo unaonituma kuitaka kazi hii na si maslahi.kama ni maslahi basi ningetafuta kazi ambayo inaendana na taaluma yangu ambayo naamini isingekuwa shida sana kuipata.
ila sikuelewi unaposema kama nina akili zangu timamu basi nitafute kazi nyingine.una maana wanaofanya kazi usalama akili zao siyo timamu au akili zangu siyo timamu ndiyo maana natafuta kazi usalama wa taifa?labda swali lingine,je kwa mfano napata kazi uko usalama wa taifa,siwezi kupangiwa kitengo kulingana na taaluma niliyosomea?
 
Mdogo wangu huna sifa. Hii kazi kama unataka hutakiwi kuji publish. Hutaweza kutunza hutayoshuhudia au kuyaona. Kuna kitengo cha research na recruitment kama una access nao poa tu. Mara nyingi hizi kazi kama ni kuapply huwa taarifa zinatoka ndani na huwa hazitoki magazetini. ndo maana wanopata kazi ni wale ambao wana ndugu au marafiki huko. kwa hiyo kama una mjomba yeye ndo hapo hapo. na pia ukishafanya interview wanaweza wakakuchukua hapo hapo au wakakaa kimya hata miaka minnee mitano siku wanakuja kukushtukiza wakati ulishasahau. Kama una ndugu yoyote huko mwambie upo interested then baada ya muda nafasi zikitoka atakustua. lakini usipende kuongea kwa watu kama unataka hiyo kazi sababu hutoipata. unaoongea nao hao ndo baadhi yao ni ma informer. ndo watakao kurecommend kama unafaa au laa. good luck.


sawa mkubwa wangu lakini dont judge a book by its cover!
ushauri wako mwingine nitauzingatia.
 
..PINDA ALIINGIA ALIPOKUWA MWAKA WA KWANZA MLIMANI....AKAAZA KWA ASSIGNMENT KUPELEKA PELEKA REPORTS MSASANI...BAADA YA KUMALIZA PALE AKAAPELEKWA MOJA KWA MOJA IKULU....AKIFANYA KAZI ZOTE HADI YA KUMPELEKEA MZEE KAHAWA HADI KUWA CLERK WA BARAZA LA MAWAZIRI etc....
 
Hana sifa kivipi wakati katumia jina bandia? Akienda kuomba hiyo kazi kutumia jina lake la serikali watajuaje yeye ndiye ajiitaye p53 kule Jamiiforums?

Unless kwenye cheti chake cha kuzaliwa jina lililopo ni p53, mimi sidhani kama hana sifa. And for all we know, he could be one of them already....

ndiyo hapo ninaposhindwa kushangaa yaani p53 wa jamiiforums kudhaniwa ndiye yuleyule atakayekwenda usalama kuomba kazi!!
mkuu ngabu,bado sijawa mmoja wao ila ningependa kuwa mmojawao.
 
we hujasoma text yake vizuri. huoni ameshajifanyia kitu kinaitwa profiling.
na pia hatakuwa amshawaambia na marafiki zake before kaja hapa. Based on the profile unaweza kumjua. current masters student, age 28, interest: Usalama, Dislikes: Military Training. Atakuwa kishamuambia one of his/her friends au watu anaofahamiana nao sasa huoni kam hiyo ni profile.

bado hazijawa specifics mkuu.wangapi wanafanya masters at 28?wangapi hawapendi military training?halafu sijasema kwamba sipendi military training kwahiyo hizi ni hisia zako tu ambazo si za kweli.
 
Zamani Usalama wa Taifa walikuwa wanapita katika shule za Sekondari wanafanya recruting.
Usalama wa Taifa ni kazi nzuri. Ukitaka kuingia Usalama wa Taifa,lazima utakuwepo ushindani,kwa sababu watu wengi watakuwa wanaitaka hiyo kazi,wengine kwa ajili ya uzalendo,na wengine kwa ajili tu wanatafuta kazi yoyote ile waifanye. Kwa hiyo kuonana na wahusika will be only the first step.
I suggest,uende Kijitonyama,Karibu na Makumbusho kwenye Makao Makuu yao,na uingie mule ndani,uende pale reception,uwaeleze shida yako. I mean kama ukitaka kujiunga na Jeshi si utakwenda Ngome? Kwa hiyo,my suggestion is that you should just walk into their HQ,halafu utapata maelekezo pale.

sawa mkuu nitafuatilia huko
 
Wrong!! Kijitonyama sio makao makuu, makao makuu yako karibia na St. Peters, kama anataka information aende ofisi za pale Stesheni au pale Ocean Road karibia na uwanja wa basketball wale ndio wanaweza kumsaidia. Kama hayuko Dar Es Salaam aende kwenye ofisi za wilaya au mkoa.

haya ndiyo maneno mkuu siyo kuni disqualify tehe tehe tehe!
 
mkuu kabla sijajibu embu fafanua kuwa kwenye field na kuwa kwenye desk manake nini?

Haha, bado unaendelea kupoteza sifa tuu za kuwa uko unakotaka kwenda kufanya kazi(PSYKE)

Since mnawazungumzia akina James Bond and them, nitatumia mfano wa kwenye sinema.

**Jason Bourne ni field agent or Intelligence Operative/Officer
**Alex Conklin au M ni Desk officers.

Sasa since umesema hutaki military training basi wewe utakuwa unataka kuwa desk officer, mind you lazima upitie basic training ambayo ina;
-hand to hand combat(self defence etc)
-jinsi ya kutumia silaha kama bastola na bunduki
-jinsi ya kuinterrogate.
-etc etc
kama instructor wako atakuona unafaa kuwa IO mzuri atakutrain kuwa field agent, hapa ndio utapewa paramilitary training etc etc.

**Majina ya Jason Bourne na Alex Conklin ni kutoka kwenye Filamu ya Bourne Identity
M ni kutoka kwenye filamu za 007-James Bond
 
tatizo vijana wa siku hizi wanataka kazi ya usalama ili wafanye mbwembwe...kuliko kazi....,ukikaa nao wanavojionesha utajua tu..akishakunywa vibia viwili basi tena anaaza kutapika maneno..ovyo kabisa..tunawaangalia tu!!

zamani hata mtoto alikuwa hajui kama baba yake anafanya kazi huko...kuna mzee mmoja alifariki karibuni ..alikuwa huko ,that old man was very desplined [kama mfano tu]....hakuna siku amepata hata kutamka,hata walevi wenzake walikuwa wakijuwa yeye ni shoe shiner style mission town...siku anazikwa ndio wakaaza kushangaa ...alaa kumbe naye huyu alikuwa na mwajiri [pale mc alipotangaza wafanyakazi wenzake ..bila kutaja wa taasisi gani waje waweke shada la maua]

lakini mnajuwa hili linatokana na ukosefu wa ajira ..so watu hata wasiokuwa na uwezo wanaona kuajiriwa pale ndio njia pekee ya kuukata..bila kuwa mustakabali wa uzalendo wao kwanza...

miaka ya 90 up serikali ilipozuia ajira tatizo hili pia lilikomaa majeshini. hadi watu wakawa wanahonga ili tu waajiriwe jeshini[wanaojua hii kitu wanakumbuka ile kashfa ya ajira jeshini]..kwani ndio taasisi pekee iliyokuwa ikiajiri...matokeo vijana wengi waliingia jeshini bila kuwa na wito zaidi ya kutaka ajira..matokeo baada ya sekta binafsi kuanza kuchanua miaka ya 2000 na ajira serikalini kufunguliwa ....askari wa aina hiyo walianza kuomba kusraafishwa au walitoroka ...

nadhani sehemu nzuri ya mtu anayetaka kuajiriwa kwenye vyombo vyetu polisi,usalama,jeshi ,magereza etc...iwe JKT [kwa kujitolea]....if you are really serious jitolee kwenda jkt...ukasote mwaka mmoja .....then ajira zote za vyombo zipelekwa huko!!!....na msiwakatishe tamaa wale vijana wanaojitolea kwenda jkt kwa kuwanyima umuhimu wa kwanza pale vyombo vinapoajiri....kwani kwa sasa ukiona mtu anamaliza form six...anaacha oppoertunity nyingine anaamua kujitolea kwenda jkt mwaka mzima basi ujuwe ni mzalendo kuliko yule anayengojea ajira ya jeshi au chombo kingine kwa kushikwa mkono....TUWEKE UTARATIBU KAMA KUNA NAFASI 1000 TUNAAZA NA WALE VIJANA WALIOJITOLEA ..ZIKIBAKI NDIO WENGINE WAFIKIRIWE!!!!!
 
Nafurahi nji hii bado inawatu wenye ujasiri wa kuchagua kazi ... tehetehe ...

Waisikuchanganye mwanetu, Go p35 ... go p35 ... go
 
Haha, bado unaendelea kupoteza sifa tuu za kuwa uko unakotaka kwenda kufanya kazi(PSYKE)

Since mnawazungumzia akina James Bond and them, nitatumia mfano wa kwenye sinema.

**Jason Bourne ni field agent or Intelligence Operative/Officer
**Alex Conklin au M ni Desk officers.

Sasa since umesema hutaki military training basi wewe utakuwa unataka kuwa desk officer, mind you lazima upitie basic training ambayo ina;
-hand to hand combat(self defence etc)
-jinsi ya kutumia silaha kama bastola na bunduki
-jinsi ya kuinterrogate.
-etc etc
kama instructor wako atakuona unafaa kuwa IO mzuri atakutrain kuwa field agent, hapa ndio utapewa paramilitary training etc etc.

**Majina ya Jason Bourne na Alex Conklin ni kutoka kwenye Filamu ya Bourne Identity
M ni kutoka kwenye filamu za 007-James Bond



sawa mkuu.kwahiyo all in all itategemea na uamuzi wa instructor wangu kuwa na fit wapi.
sasa mkuu icadon na wale wa kwenye msafara wa viongozi nao inakuwaje?ndiyo hao desk au field?
 
Huyo anayefikiria kila mtu anayefanya kazi kwenye Intel Org ni SPY aka James Bond.

Icadon,

Huyo aliyedhani kwamba mtu yeyote anaefanya kazi Intel body aweza itwa spy hajakosea. Sio wote wa Usalama wanafanya clock and dagger operations lakini kimsingi kazi zao ni kazi za kificho, za kijasusi, u-spy.

Ndio maana hata mkuu wa intelligence organization ya nchi mara nyingi anaitwa "Spy Chief," japo, again, sio kila mtu anaefanya kazi huko anahusika moja kwa moja na clock and dagger functions.

Again, msingi wa kazi yao ni u-spy.

Associated Press: Pakistan spy chief seen as tough on militants: Pakistan's new intelligence chief is seen as likely to strengthen the fight against al-Qaida and the Taliban, but takes the job amid U.S. concerns that elements in the country's spy agency are helping extremists. His appointment as head of the powerful Inter-Services Intelligence, the country's main spy agency, was...

Spiegel International: Germany Spy Chief under Pressure: The head of Germany's foreign intelligence agency has come under fire over admissions his employees monitored e-mails exchanged between a minister in the Afghan government and a SPIEGEL journalist. Chief spy Ernst Uhrlau will likely keep his job, but the scandal is...

NY Times: Global Economy Top Thread to US., Spy Chief Says: The new director of national intelligence warned Congress yesterday that the global economic crisis poses a graver and more immediate threat to the US than international terror, the New York Times reports.
 
sawa mkuu.kwahiyo all in all itategemea na uamuzi wa instructor wangu kuwa na fit wapi.
sasa mkuu icadon na wale wa kwenye msafara wa viongozi nao inakuwaje?ndiyo hao desk au field?


Inategemea wewe unataka kuwa wapi(interview ya pili), ukienda kwenye basic training ukionekana wewe una uwezo wa kuwa field agent mzuri basi instructor atakwambia na kukuuliza kama uko interested.

Wale ni bodyguards lol.

something is not right kwenye hii thread.
 
1984 nikiwa JKT pale Ruvu walikuja kuli cruit watu waliopenda kujiunga na taasisi hiyo na vijana wengi waliokuwa wamemaliza form 6 walikwenda kwenye interview na walichaguliwa watu wasiopungua kama 6 tu kati ya umati wa watu kama 200 hivi.
Huwezi kujua viwango wanavyotaka p53. Hiyo siku zote ni siri yao. Ingawa maswala ya elimu ni priority kwao kwani wanataka wasomi siku hizi, lakini si rahisi kujua nini wanahitaji hata uchaguliwe hata kama ungefanya interview na wewe ni msomi. Wasomi wangapi wana hata PHD na hawako huko?
Natambua kuwa hapo hapo chuo kikuu mlimani ni recruiting center yao watu wa UWT na wanawa target wasomi sijui katika vyuo vingine. Wakikuhitaji sawa kama hawajakuhitaji, achana nao ziko kazi nyingi za kujenga taifa tena zenye heshima kuliko hiyo.
Wewe komalia kazi unayofanya achana na kazi zisizoeleweka na zinazoweza kukuweka katika risk maishani mwako. Unajua nasema nini?
 
Hivi kwanza big deal ya kuwa spy ni nini? kubeba kibastola kila uendako na kujisikia wewe ni superman au superwoman au?

Kwa muono wangu, mtu ukiwa ktk mambo hayo hata maisha huwezi kuyafurahia kwa sana. But to each his own....
 
Inategemea wewe unataka kuwa wapi(interview ya pili), ukienda kwenye basic training ukionekana wewe una uwezo wa kuwa field agent mzuri basi instructor atakwambia na kukuuliza kama uko interested.

Wale ni bodyguards lol.

something is not right kwenye hii thread.


ukiacha bodyguards ina maana hakuna shushushu kwenye misafara ya viongozi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom