Tathmini yangu ni kwamba mjadala wa namna ya kupata kazi Usalama wa Taifa umekuwa na sura nyingi zenye kupingana. Baadhi ya masuala yanaonekana ni ya kufikirika zaidi. Kama alivyo P53 nami ningependa kupata kazi Usalama wa Taifa kwa sababu hizo hizo za uzalendo kwani naamini chombo hiki kina nafasi muhimu ya kujenga taifa. Miongoni mwa mikanganyiko niliyoipata ni kama ifauatavyo:-
SHY anasema Mtanzania ataajiriwa Usalama wa Taifa baada ya kutoa taarifa fulani fulani kuhusu mambo fulani au kuomba magazetini kisha atajikuta yuko Usalama wa Taifa.
SHAYCAS anatuambia kama unataka kazi huko kamwone au wasiliana na mtu anayefanya kazi au aliyewahi kufanya kazi huko.
CHUMA anatuaelekeza kuwa kuingia Usalama wa Taifa hakuhitaji connections kwa sababu utaratibu mpya wa sasa waombaji kazi Usalama wa Taifa huanza kwa kuajiriwa kama wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani.
DISSOFFICERREC anasema kazi za Usalama wa Taifa hazitoki magazetini.
PHILLEMON MIKAEL anatueleza kuwa Waziri Mkuu MIZENGO PINDA alipokuwa mwaka wa kwanza Mlimani ( chuo Kikuu cha Dar es salaam) alianza kwa assignment kupeleka taarifa msasani na baada ya kumaliza chuo akapelekwa Ikulu. Hivi hizo assigments hazikuwa za siri kama utaratibu wa kazi za namna hiyo?
Kuna wanaotuambia ili kupata kazi Usalama wa Taifa tuwasiliane na kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama au Makamanda wa Polisi.
Yupo anayesema Usalama ni ya watu wa Ikulu pekee hapo hapo anatusihi tuombe kazi huko.
Lakini pia katika ya mjadala tunaambiwa kuwa kama shuleni ulikuwa mbumbumbu huwezi kuajiriwa na chombo cha intelijensia.
Vilevile katika mjadala huu imejitokeza kuwa Usalama wa Taifa wana target zao na kama wewe siyo lengo kamwe huwezi kuchukuliwa.
Katika maelezo mengine ni mchanganyiko wa hapa na pale!!! Hivi katika mjadala huu ni nani mkweli ili anisaidie na mimi kuingia huko?
KUKIRI KWAMBA JAMBO SILIFAHAMU SI UPUMBAVU BALI NI UKOMAVU WA AKILI.
WanajamiiF kazi hizi za usalama wa taifa zipo ila ni kwa nini wewe uone kazi ni usalama wa taifa tu......baba yangu ni mkulima wa mpunga na mahindi na yeye pia ni usalama wa taifa...''he is a national security officer to secure the nation from being affected by famine okey you can judge yourself under any aspect like my father as well as me myself I am a carpenter''....msing'ang'anie kazi huenda Mungu anataka kukuepusha na uuaji...because si wote wanashika peni wengine wanashika bastola kuwaua wema.
Mpaka hapo ushapoteza sifa tayari.
Nakubali.
Lakini sister brother p53, hata kama ungekuwa na jina la Baba wa matawi ya juu, au mtoto wa masikini, hutakiwi kukubali kupitia kwa watu maarufu, the Apson's and the Kitine's of the world, ili upate kazi sehemu kama Usalama wa Taifa. Ndio ufisadi wenyewe huo. Kwamba, my point is, p53, mambo ya connection connection na kujuana juana haya nishai. Mimi hapa nilipo sitaki kujuana na Kitine au Apson hata kama ningekuwa na access nao, hata kama wao ndio the go-to guys wa kukutafutia kazi Usalama. Sitaki, sitaki kuwajua. Wakae na ukuu wao na utajiri na umaarufu wao, waanze mbele!
Kwa nini tusijenge nchi ambayo sio lazima uka kiss ass kwa Kitine ili akuunganishie kazi Usalama wa Taifa? Yani mimi siwezi, siwezi, sijui ni kiburi cha kutotaka kuuza utu wangu, lakini sitaki.
Huyu Shycass anaweza kuwa na Kitine au jamaa yake fulani ambae anaweza kumuunganishia mahala akapeta, lakini ambacho hakijui ni kwamba mtoto wake Shycass akija baadae anaweza kuwa hamjui mtu, kwa hiyo yeye, kizazi cha baadae, atapata shida, kwa hiyo tusipojenga mazingira ambayo hayajitaji kujuana kwa kweli si poa kwa nchi yetu.
So, to hell with kujuana na the Hassi Kitine's of the world. Screw that!
Hata wewe unaweza kuwa usalama wa taifa unaweza kutumika sehemu fulani fulani kutoa taarifa fulani kuhusu mambo fulani mwanzo huwa ni hapo wakati mwingine ni hizi kazi za magazetini wewe apply tu utajiona siku dili na usalama wa taifa hilo limekuangukia
Mie mwenyewe nataman kufanya kaz usalama wa Taifa.sifa ninazo.nimewachunguza wapenz wangu wote mpaka kuwafumania wale wasiokuwa waaminifu.nimetunza siri za mahusiano yangu hakuna mpnz aliyegundua km nilizoea kumsaliti.ujuzi wa kujilinda ninao,sijawahi kuvamiwa na mwizi tangu nianze kuishi peke yangu.nahitaji kweli hii kazi ili kuokoa Taifa langu
how and why?