kaka CIA ni kati ya mashirika bora kabisa ya kijasusi lakini tatizo la marekani INSIPIRATION ya kwanza ya mtu ku serve jeshini,CIA,FBI ets ni maslahi zaidi kuliko utaifa......UAJIRI HOLELA WA CIA ndio unaowasababishia matatizo ya siri zao kuvuja mara kwa mara[angalia taarifa mbali mbali na kufuatilia majarida]...na pia pamoja na kulipwa mshahara mkubwa imekuwa rahisi kwa mashirika ya russia na mengine kupemyeza watu wao...
Kila kitu ulichokisema hapo juu sio kweli.
Idara karibu zote za Serikali ya Marekani, ikiwemo CIA, siku zote zinabakia nyuma katika kushindania vipaji vya wataalam kwa sababu masilahi yake ni kiduchu kulinganisha na sekta binafsi. Malipo ya Serikali wanayaita karanga.
Mbili, kuvuja kwa siri - kule kunakohusisha wenye asili ya kigeni - hakutokani na "uajiri holela." Wachina wote wanaoingia CIA ni Raia wa Marekani, na Sheria yao hairuhusu kumnyima kazi awae yote kwa sababu babu yake alikuwa Mchina au Mhindi. Sheria hiyo, zaidi ya msingi wa uadilifu, ina mantiki nyingine. Marekani imejaa Wazungu wazawa ambao babu - na hata baba - zao walikuwa sio wa asili ya hapa. Isingewezekana kuchambua na kuwapata wale tu ambao ni vitukuu vya vitukuu vya wazawa wa Marekani. Sababu inayofanya Wamarekani wa Kichina tu wakose uaminifu wa Usalama ni kwa vile Mchina Mwekundu sasa hivi ana mwamko, ana ambition, ya kujenga Taifa Kubwa. Ndio maana unasikia wanaowacheza michezo ya siri mara nyingi ni Wachina, japo CIA na Serikali imejaa watoto wa Waitalia, Wajerumani, Wapotoriko, Wahindi Koko na Wagagagegegigikoko.
Tatu, hoja yako ya kwamba Warusi wanaweza kujipenyeza kuingia CIA kwa sababu CIA kuna maslahi, hicho kitu sio tu hakipo, ila pia, hata kama kingekuwepo, hakisaidii hoja yako. Kama ungesema maslahi ya CIA ni madogo ndio maana Warusi wanatumia hio kama tundu la kujipenyeza kwa kupenyeza ufisadi, hapo ungeleta mantiki zaidi.
Kuhusu recruiment za jeshi, nadhani, hayo yako nje ya mada.
Vitu ulivyoiitangazia dunia hapo juu vyote havipo!