Natafuta Kazi Usalama Wa taifa

Natafuta Kazi Usalama Wa taifa

Status
Not open for further replies.
Ndugu Anfaal,

Nakubali kuwa suala la kujuana linaweza kuwepo (karibu kila idara TZ iko hivyo), ila nafikiri utaratibu wa haki pia upo. Lakini utaratibu wenyewe nafikiri ni sehemu pia ya "usalama wa Taifa" kwa hiyo si lazima wote tuufahamu ili kuepusha "infiltration of foreign agents". Nafikiri kuna information huwa zinakuwa released based on "need to know".

Kwa upande mwingine nakumbuka mwaka niliokuwepo Juni Kumi na Tano (JKT) kwa mujibu wa sheria, kwenye kambi yangu tulitangaziwa nafasi hizo kidizaini . Wote tukiwa parade, tukaambiwa form six leavers wabaki, wengine, waondoke. Baadaye, Tukaambiwa waliopata div.1 na 2 wabaki wengine waondoke. Ni kwenye hatua hii ndio wakachukua majina ya waliobaki. Hapo ndipo tukaambiwa wanaotaka kujiunga na UWT wabaki ambao hawataki waondoke na tulikatazwa kuongelea hilo swala baada ya kuondoka. Waliobaki walipelekwa kwenye ofisi ya No. 10 (Intelligence officer IO tulikuwa tunafupisha kama 10).

Wengi waliobaki nawakumbuka mpaka leo, japo sijui wako wapi kwa sasa na halikuwa suala la kujuana.
 
Ndugu Anfaal,

Nakubali kuwa suala la kujuana linaweza kuwepo (karibu kila idara TZ iko hivyo), ila nafikiri utaratibu wa haki pia upo. Lakini utaratibu wenyewe nafikiri ni sehemu pia ya "usalama wa Taifa" kwa hiyo si lazima wote tuufahamu ili kuepusha "infiltration of foreign agents". Nafikiri kuna information huwa zinakuwa released based on "need to know".
Tatizo langu ni hapo ambao si lazima wote wajue kwanini? Kwanini hatutaki kujifunza? Wale wanaotangaza kwenye website zao je inakuwaje? Infiltration ya foreign agents haiwezi kutokea kwa namna hiyo?
 
Usalama una aply polisi afu wao ndo wanamega baadhi kwenda mafunzo ya usalama wa taifa. Huwa sehemu tofaut na wanaofanya upolisi
Hii umeitoa wapi? Ninawafahamu wengi saaana ambao waliajiriwa kwa sababu tu baba zao au jamaa na rafiki wako kule. Hii ni mentality mbaya saana. Halafu kwanini wemegwe tofauti? Kazi hizi ni tofauti saana zilivyo na ndio maana hata wizara ni tofauti na namna ya utendaji ni tofauti. Mtu anaweza asiwe na interests na polisi lakini akawa na interests usalama na kinyume chake.

Tunaogopa nini kuifanya system ya rectruitment wazi halafu selection ikafichwa kama haja ni usiri?
 
Ndugu Anfaal,

Inawezekana kabisa kuwa umejaribu kutafuta kazi ukakosa au umeona kuwa kazi unazopata hazilipi. Ukiangalia neno 'Usalama wa Taifa' utadhani ni very sensitive job ila kazi hizi huunganisha kuanzia polisi, JWTZ, askari kanzu, wapelelezi n.k, Ukija kwenye kazi kama JWTZ, Polisi hawa kazi zao hutangazwa.

Ila linapokuja suala la upelelezi [Hapa nina maana siyo kupeleleza kesi na matukio ya jinai bali ni kupeleleza wananchi (informer/shushu, nusanusa, mnoko, umbeya n.k) ili kujua kama kuna njama zozote zile zinazoweza kuitia nchi katika msukosuko wa kiuongozi kama uasi, mapinduz i(japo siku hizi yamekosa msukumo baada ya jumuiya za kimaifa kuwatenga wapinduaji)] hapo kidogo inakuwa ni sensitive, maana ukishamjua mbeya huwezi ku-disclose issue yoyote nyeti kwa kuhofia kuwa atawapelekea watawala.

Hawa ni lazima wawe watu walio under cover. Na wengi wao huwa na kazi nyingine kabisa zaidi ya upashaji wa habari za kimbeya. Ila katika group hili wapo wa aina mbili kuna wale ambao ni permanently employed na wanajulikana kama analysts, wao kazi yao ni kukusanya habari toka kwa wapashaji na kuzianalyse na kuchukua genuine na kuzipeleka kwa baraza la usalama for action na mara nyingi hukabidhiwa rais. Hawa ma analyst hata ukiwajua haitasaidia kitu kwani wao si frontliners, watu ambao wapo kwenye risk zaidi ni frontliners ambao kama wakujulikana huweza hata kupoteza maisha na ndiyo maana wanalindwa kwa kuwa under cover.

Lakini ukiangalia historia ya usalama wa taifa utaona imeanzia Egypt kwa Filauni (Pharao) ambaye alipata habari ya kuja kwa nabii Mussa ambaye ataushinda utawala wake toka kwa mtabiri wake aliyemwamini sana. Filauni alipoona hivyo akaweka watu kuchunguza kila mtoto atakayezaliwa popote ajulikane na kama ni wa kiume auwawe kabla ya kuja kuwa adui wa utawala wake na kumuangusha, hapo ndipo chanzo cha usalama wa Taifa ulipoanzia.

Kwa nini wewe unataka kazi hii??
 
Asante kwa maelezo yako.

Sijatamka kuwa ninaitaka kazi hii sehemu yoyote hapo. Na si kwamba kazi yangu ni mbaya. Hapana, ni bora saana na ninaipenda na sijutii kuwa kwenye hii proffesional maana imenifikisha nilipo. Lakini ninachozungumzia ni uwazi wa recruitment naomba tuelewanae. Si selection wala namna wanavyofanya kazi. Kuna watu wangependa kuwa huko lakini kwa bahati mbaya mfumo mbovu wa utoaji kazi hizi haueleweki.

Hii kazi ni kama kazi yoyote vile. Leo unasikia fulani ni polisi bila kujua polisi wanapatikana vipi. Popote pale kwenye kificho ndio chanzo cha rushwa. nakumbuka miaka hiyo tumemaliza form 6 kuna mtu alikuwa anapita anawaambia watu wampe pesa atawaingiza usalama. Why?

Nimesema mwazoni kwanini iunganishwe na polisi au JWTZ. Historia ipo, yes, lakini iwe chanzo cha kutupeleka mbele sio kung'ang'ania utaratibu uliopo.
 
Mbona mimi ni mlinda Usalama wa Taifa na sijaajiriwa na mtu? nimejitolea kulinda Taifa langu.
 
Tatizo langu ni hapo ambao si lazima wote wajue kwanini? Kwanini hatutaki kujifunza? wale wanaotangaza kwenye website zao je inakuwaje? Infiltration ya foreign agents haiwezi kutokea kwa namna hiyo?

Nchi yetu huwezi kulinganisha na UK au USA au na nchi zingine nyingi tu zilizotuacha kimaendeleo.

Nchi za wenzetu, institutions zao nyingi ndani ya serikali, zipo kamili. Mtu una-apply hata kutoka kwenye website zao, lakini wanaweza wakakufahamu hata kabla hawajakuita. Sisi tupo nyuma sana, kiasi kwamba hata vitambulisho vya uraia hatuna, vitambulisho vya kazini na kupigia kura, hata asiye raia anaweza kuwa navyo, kwa namna hii, nafikiri utaratibu wetu inabidi uwe crude. Isitoshe, si ajabu wengi kwenye UWT hata level zao za IT zikawa chini, wakitumia websites labda hata vijana wa hapa jukwaani wanaweza ku-hack. Unaweza kukuta Mkurugenzi mwenyewe anatetemeka kushika mouse ya computer.

Nafikiri tuwape benefit of doubt, kwamba hata kama hatujui wanavyopeana kazi, basi wanapeana kwa kufuata misingi fulani ya haki, huku wakitunza siri za usalama wa nchi yetu.
 
Asante kwa maelezo yako.

Sijatamka kuwa ninaitaka kazi hii sehemu yoyote hapo. Na si kwamba kazi yangu ni mbaya. Hapana, ni bora saana na ninaipenda na sijutii kuwa kwenye hii proffesional maana imenifikisha nilipo. Lakini ninachozungumzia ni uwazi wa recruitment naomba tuelewanae. Si selection wala namna wanavyofanya kazi. Kuna watu wangependa kuwa huko lakini kwa bahati mbaya mfumo mbovu wa utoaji kazi hizi haueleweki.

Hii kazi ni kama kazi yoyote vile. Leo unasikia fulani ni polisi bila kujua polisi wanapatikana vipi. Popote pale kwenye kificho ndio chanzo cha rushwa. nakumbuka miaka hiyo tumemaliza form 6 kuna mtu alikuwa anapita anawaambia watu wampe pesa atawaingiza usalama. Why?

Nimesema mwazoni kwanini iunganishwe na polisi au JWTZ. Historia ipo, yes, lakini iwe chanzo cha kutupeleka mbele sio kung'ang'ania utaratibu uliopo.

Frontliners wa UWT hata siku moja hawawezi kutangazwa kama vile wanavyotangaziwa "state attorneys et al" Sababu kubwa ni kwamba wanatakiwa kufanya kazi under cover full stop, anaweza kuwa lecturer wako chuoni, manager wako kazini, katibu mkuu wako wizarani, katibu muhtasi wako kazini.

Recruitment ya watu hawa ni sensitive na unaweza fuatwa na mtu usimfahamu aka kushawishi, then utajikuta unatembelewa na strangers kukuchimba, bila kujua ndiyo usaili wenyewe huo, sasa wewe baada ya hapo unapelekwa kwenye mafunzo. Nchi nyingi duniani hutumia mfumo huu, lengo likiwa ni kuhakikisha informer abakia kuw under cover ili kumlinda yeye uwezo wake wa kupata habari. Mara nyingi akiisha julikana tu basi huwa ni mwisho wa kazi hiyo, au anahamishiwa sehemu isiyohitaji cover.

Jaribu hata kuwa unafuatilia hata sinema za kipelelezi basi mambo mengine ni common sense tu si lazima uwe huko.
 
Nchi yetu huwezi kulinganisha na UK au USA au na nchi zingine nyingi tu zilizotuacha kimaendeleo.

Nchi za wenzetu, institutions zao nyingi ndani ya serikali, zipo kamili. Mtu una-apply hata kutoka kwenye website zao, lakini wanaweza wakakufahamu hata kabla hawajakuita. Sisi tupo nyuma sana, kiasi kwamba hata vitambulisho vya uraia hatuna, vitambulisho vya kazini na kupigia kura, hata asiye raia anaweza kuwa navyo, kwa namna hii, nafikiri utaratibu wetu inabidi uwe crude. Isitoshe, si ajabu wengi kwenye UWT hata level zao za IT zikawa chini, wakitumia websites labda hata vijana wa hapa jukwaani wanaweza ku-hack. Unaweza kukuta Mkurugenzi mwenyewe anatetemeka kushika mouse ya computer.

Nafikiri tuwape benefit of doubt, kwamba hata kama hatujui wanavyopeana kazi, basi wanapeana kwa kufuata misingi fulani ya haki, huku wakitunza siri za usalama wa nchi yetu.
Hivi ni visingizio ambavyo vinakwamisha saana maendeleo yetu. Hivi unafaham kwamba wale wanaopelekwa na ndugu zao wanafanyiwa vetting tena wakati fulani huchukua hata miaka miwili. Sasa kama wanaweza kuwafanyia vetting hao kwanini wasifanye kwa wote.

Mapungufu mengi tunayoyaona kwenye serikali yetu wakati fulani inasababishwa na wataalamu waliopo kule. Kuna haja ya kufanya vitu kitaalam. Ukifanya Kitaalam, ufanisi utaongezeka kwa maana ya gharama kupungua kwa sababu utahitaji watu wachache kufanya kazi kubwa.

Tujifunze tuache kusingizia umasikini wetu.
 
Frontliners wa UWT hata siku moja hawawezi kutangazwa kama vile wanavyotangaziwa "state attorneys et al" Sababu kubwa ni kwamba wanatakiwa kufanya kazi under cover full stop, anaweza kuwa lecturer wako chuoni, manager wako kazini, katibu mkuu wako wizarani, katibu muhtasi wako kazini.

Recruitment ya watu hawa ni sensitive na unaweza fuatwa na mtu usimfahamu aka kushawishi, then utajikuta unatembelewa na strangers kukuchimba, bila kujua ndiyo usaili wenyewe huo, sasa wewe baada ya hapo unapelekwa kwenye mafunzo. Nchi nyingi duniani hutumia mfumo huu, lengo likiwa ni kuhakikisha informer abakia kuw under cover ili kumlinda yeye uwezo wake wa kupata habari. Mara nyingi akiisha julikana tu basi huwa ni mwisho wa kazi hiyo, au anahamishiwa sehemu isiyohitaji cover.

Jaribu hata kuwa unafuatilia hata sinema za kipelelezi basi mambo mengine ni common sense tu si lazima uwe huko.
Kwa bahati mbaya siongei nisilolifaham kama unavyotaka kuniaminisha. Hata wale top uwaonao wamefika pale mostly through promotion.

Najua kuna walimu et al. wanafanya kazi hiyo. Lakini swali ni kwamba, inakuwaje mtu atumike kumuidentify mtu kwa ajili ya kazi yenye maslahi kwa taifa? Anajuaje kwamba hawapo wenye qualification kubwa zaidi na wana interest na kazi hiyo?

Siku hizi dunia imebadilika saana. Sio mfumo wa kila sehem. Pitia baadhi ya websites za vitengo hivyo, unaweza kujifunza kitu. Naendelea kusema tena; informer atakuwa tu undercover lakini recruitment process iwe wazi alafu selection ndio iwe siri. Tatizo nini hapo? Unajua nchi yetu tuna dhana ya ajabu saana ya usalama ndio maana hata matapeli hujitangaza ni usalama.
 
Hili linategemea nchi na nchi.

Ziko nchi nyingine wanatangaza kabisa (soma hapa Vacancies in Intelligence Bureau Recruitment (Central Intelligence Officer) 2009 …….; https://www.cia.gov/careers/opportunities/cia-jobs/index.html).

Hata hapa kwetu wanatangaza ila huwezi kujua kama hizo ndizo kazi zenyewe. Kwa mfano ukishakubali kuajiriwa PCCB ujue ni UWT. Hata hivyo ishu ya usalama wa taifa ni "complex" maana kila sehemu wapo. Kwa mfano katika vyuo vikuu hawa wapo na ili kurahisisha wanakuwa ni wafanyakazi wa taasisi hiyo. Muda mwingine tax driver ambaye hajaenda hata shule wanafanya hiyo kazi wapo tunawajua. Hata mkeo anaweza kuwa shushushu wako na usijue.

Zamani enzi tukiwa shule ya msingi mwalimu mkuu alikuwa anapewa jukumu la kutafuta vijana safi kimaadili ambao baadaye walikuja kuwa UWT.
 
Hili linategemea nchi na nchi.

Ziko nchi nyingine wanatangaza kabisa (soma hapa Vacancies in Intelligence Bureau Recruitment (Central Intelligence Officer) 2009 …….; https://www.cia.gov/careers/opportun...obs/index.html).

Hata hapa kwetu wanatangaza ila huwezi kujua kama hizo ndizo kazi zenyewe. Kwa mfano ukishakubali kuajiriwa PCCB ujue ni UWT. Hata hivyo ishu ya usalama wa taifa ni "complex" maana kila sehemu wapo. Kwa mfano katika vyuo vikuu hawa wapo na ili kurahisisha wanakuwa ni wafanyakazi wa taasisi hiyo. Muda mwingine tax driver ambaye hajaenda hata shule wanafanya hiyo kazi wapo tunawajua. Hata mkeo anaweza kuwa shushushu wako na usijue.

Zamani enzi tukiwa shule ya msingi mwalimu mkuu alikuwa anapewa jukumu la kutafuta vijana safi kimaadili ambao baadaye walikuja kuwa UWT.

Mary Chatanda
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom