Natafura mfumo bora wa ukusanyaji kodi katika nyumba za kupanga

Chiumbe

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
561
816
Wakuu salamu.

Naomba niende kwenye point moja kwa moja.

Kama mnavyojua miaka inasogea na watoto wanakua na wakubwa wanazeeka. Na maisha yanasonga mbele na TOZO zinayoyoma. Pamoja na 10% inayopendekezwa na serikali ya CCM, kwenye nyumba za kupanga.

Sasa Mungu katubariki vijumba viwili vitatu tunapangisha. Na hali sasa ilivyokua tight hata ulipaji wa kodi umekua una ukakasi.

Kutokana na umri wa bi mkubwa umeenda sana ni kama ana kama 65 hivi. Nikataka kuja na wazo la jinsi ya ukusanyaji bora wa kodi pamoja na uwekaji wa kumbukumbu nzuri baina sisi wapangishaji na wao wapangishwaji, maana kuna utata wa tarehe ya kodi.

Nauliza hakuna system ambayo itanisaidia mimi ambaye napokea kijiti cha kupambana na wapangaji?

Mfano: nakingiza tarehe, kodi kiasi fulani na taarifa nyingine. Alafu baadae nakua napata updates kama nyumba flan kodi imeisha na namna kama hivyo.
naomba kuwasilisha​
 
Ukishindwa kumanage vitu vidogo kama hivi utaweza nini?

Hivi hata kazi ya diary hujui kweli? Basi kizazi hiki tumekula hasara na ada uliyolipiwa shule ni hasara tupu.
Diary naifahamu kazi yake, natafuta system ya kisasa
 
Modes naomba mbadilishe kwenye kichwa cha habari kutoka natafura- natafuta
 
Back
Top Bottom