Jamii yaaswa kuongeza juhudi katika shughuli za maendeleo ikiwemo kampeni ya ujenzi wa nyumba bora

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

JAMII YAASWA KUONGEZA JUHUDI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO IKIWEMO KAMPENI YA UJENZI WA NYUMBA BORA

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mwanaidi Ali Khamis ameiasa Jamii kuongeza juhudi za kushiriki kwenye shughuli za maendeleo ikiwemo kampeni ya ujenzi wa nyumba bora za makazi ili kuchochea maendeleo endelevu nchini.

Mfumo wa Jamii kushirikiana katika kujenga nyumba bora za makazi umewezesha kujengwa kwa nyumba 165 katika kata za Jinjimili, Sukuma, Ng’aya na Kabila wilayani magu mkoani Mwanza.

Mfumo unaolenga kuhamasisha jamii kujenga nyumba bora za makazi umebuniwa na shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la Kivulini.

Naibu waziri Khamis amesema kuwa dhamira ya serikali ni kuhakikisha mfumo huo unatekelezwa kote nchini.

Kampeni ya ujenzi wa nyumba bora ilianza kuekelezwa nchini Julai mwaka 2020 ambapo mpaka sasa nyumba bora 5,732 zimejengwa nchini.

IMG-20230917-WA0131-1024x768.jpg
 
"Unaihasa jamii kuongeza juhudi kujenga nyumba Bora" Maana yake ni ni ni? Kuna, mwananchi anasubili ambiwe na serikali umuhimu wa nyumba Bora? Haya, ni matamko ya, kipuuzi Sana, kwa sababu hayomuoneshi, mwananchi asiye na kipato cha kutosha atajengaje nyumba! Ingekuwa kuna mikopo nafuu, au tekinoljia ya ujenzi nafuu, harafu huu ushauri ukatolewa, ingeleta maana, bila hivyo ni maneno matamko ya kipuuzi ya kisiasa, yanasemwa ili mradi tu! Mwanasiasa ajisikie amesema, kitu,
 
Back
Top Bottom