Wakazi wa Dar hasa wenye vipato vya chini na tunaoishi kwenye nyumba za kupanga

kangesa

JF-Expert Member
Jul 3, 2023
551
1,048
Habari za usiku huu ndugu watanzania?

Moja kwa moja niende kwenye mada iliyonifanya nifikirie kushare mawazo yangu.

Wakazi wa dar,hasa sisi wenye vipato vya chini na tunaoishi kwenye nyumba za kupanga huwa tunahaha sana msimu wa mvua ukianza. Hapa nazungumzia kuanzia mwezi wa 12 mpaka mwezi wa tano ya mwaka unaofuata.

Msimu wa mvua ukianza kwa sisi ambao hupata ujira wetu kwa siku,yaani kama mafundi ujenzi pamoja na wasaidizi wao,baadhi ya wafanya biashara ambao hutegemea jua kwa kiasi kikubwa kupata wateja na wengine ambao likiwaka jua kwao linaleta ahuweni ya upatikanaji wa pesa kwaajili ya kulipa kodi za nyumba tulizopanga,kununua chakula kwaajili ya familia,kwaajili ya kulipa ada na kwaajili pia ya matumizi madogo madogo huwa tunatafutana sana kwaajili ya kukidhi mahitaji hayo yote kwa kipindi chote(kuanzianmwezi wa 12 mpaka mwezi wa 5 wa mwaka unaofuata).

pia katika kipindi chankuanzia mwezi wa 12 mpaka mwezi wa tano kwa utafiti wangu ni kipindi ambacho ndoa nyingi sana hasa za sisi walala hoi huvunjika kutokana na kukosekana kwa mahitaji muhimu kwenye familia;kama kodi za nyumba,chakula na huwa inafikia kipindi mwanaume ambae hutegemewa na familia kwa kipindi chote huamua kukimbia kabisa na mwisho ndoa zenyewe huvunjika.

Katika kipindi cha kuanzia mwezi wa 6 mpaka mwezi wa 11 au wa 12 kwa dar es salaam syo rahisi usikie mtu anaefanya kazi yoyote halali nankwa bidii ukute analalamika hali ngum ya maisha kwasababu katika kipindi hicho chote huwa kuna kuwa na upatikanaji wa uhakika wa pesa hata kwa sisi watu wa vipato vya chini kwa kiasi kikubwa sana.

Katika kipindi hicho cha upatikanaji wa pesa kutokana na shughuli au vibarua kuwa vingi baadhi ya sisi walala hoi huwa tunajisahau na kubadili kabisa mfumo wa maisha.

yaani ni kawaida kwa mtu aliyekuwa anakula dagaa kila siku katika kipindi cha kuanzia mwezi wa 12 mapaka mwezi wa 5 ukute katika kipindi cha kuanzia mwezi wa 6 mapaka mwezi 12 anakula maini kila iitwayo leo na kusahau kabisa kama huwa kuna kipindi anakosa kabisa hata hela ya kodi,hela ya chakula mpaka kufikia hatua ya kuanza kusumbua wazazi na ndugu vijijini wafanye mpango wa kuagiza mahindi kwaajili ya kujikimu na familia yake.

Katika kipindi hiki cha upatikanaji wa pesa karibu kila mtu ambaye alikuwa halewi ataanza kulewa,ambaye alikuwa hajui hata kutongoza ataanza kutongoza,ambaye alikuwa hajui hata sehemunmoja ya starehe atafanya juu chini azijue zote kwa hapa dar.

USHAURI:

Kipindi ambacho unapata pesa nyingi hasa pesa ambayo inazidi matumizi,jenga utaratibu wa namna yoyote wa kuitunza.

Unaweza kuhifadhi bank,au ukiwa nayo pesa nyingi zaidi najua wake wa mafundi wengi na sisi wengine wenye vipato vya chini wake zetu wengi kwa asilimia kubwa huwa wanacheza vikoba na michezo mingine,kwahyo unaiweka huko au unaweza kumuanzishia biashara yoyote hata ya kuuza genge. Hapo kwenye kumuanzishia biashar mkeo inatakiwa uangalie na aina mtu wako kwa maana ya uaminifu wake kwako.

Lengo la kuhifadhi hyo pesa ni nini hasa?

Lengo kubwa zaidi ni kufanya recovery ya pesa itakayopelea katika kukidhi mahitaji yako hasa katika kipindi hiki cha mvua zinapoanza kutokana na kwamba huwa kuna kuwa na ufinyu wa upatikanaji wa pesa katika kipindi hiki.

Ahsanteni ...🙏🙏
 
Mwaka wa fedha unaanza mwez. Wa 6 mzunguko unakuwa mkubwaa baada ya miez 6 ya mwanza hushuka
 
Back
Top Bottom