Wiki ya AZAKI: Kodi kubwa ni kikwazo katika maendeleo ya Dijitali

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
intro foto.jpg


Topic: Masterclass: Business and Human Rights in Digital Era.

Speakers: Jovina Mchunguzi, Godfrey Munisa and Maxence Melo (JamiiForums)

JamiiForums inashiriki katika CSO week inayofanyika Arusha ambayo inatarajiwa kuisha leo, Oktoba 27, 2023.

Siku ya leo, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo atakuwa mzungumzaji katika session ya Masterclass: Business and Human Rights in Digital Era. Ambayo inafanyika Simba Hall, AICC.

Wazungumzaji ni kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) ambao ni Jovina Mchunguzi na Godfrey Munisa, pamoja na Maxence Melo ambae ni discussant.

=====

20231027_093214.jpg

Godfrey Munisi - CHRAGG
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Tume hii ni idara huru ya serikali ambayo imeanzishwa kwa mujibu wa katiba. Ni idara huru kwa maana kwamba hailekezwi wala kupangiwa majukumu yake na serikali. Hii ni Tume ya Muungano. Ina ofisi na matawi maeneo mbalimbali nchini.

Muundo wa tume unaundwa na Kamshna 7 na Katibu Mtendaji ambao ni wateule wa Rais. Uteuzi wao ni uteuzi wa wazi ambao unachaguliwa na Kamati.

Tume ina idara mbalimbali ikiwemo Idara ya Sheria na Idara ya Haki.

Sisi tunapokea malalamiko mbalimbali ya kuhusu Utawala Bora na Haki za Binadamu na kufanya Uchunguzi. Pia tunafanya Tafiti na sisi ni Washauri Wakuu wa Rais kuhusu Haki za Binadamu na Utawala Bora. Pia tunashauri kuhusu Sheria na Utawala Bora, tuna jukumu pia la kufungua kesi inapokuwa kuna changamoto za utawala bora.

Sisi hatuko nyuma linapokuja suala la tecknolojia, tunafanya kazi kwa mfumo wa kidigitali. Mfumo kidigitali unaitwa Haki App ambapo tunashughulikia malalamiko, na pia tuna kurasa za mitandao ya kijamii ili kupokea malalamiko. Ttunatumia namba *152*00# kupokea malalamiko kwa simu za viswaswadu.

Tunafanyakazi kama Mahakama japo sisi si Mahakama. Tuna-issue summons nk. Hata hivyo kuna vitu ambavyo hatuwezi kufanya ikiwa ni pamoja na Kumchunguza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au Zanzibar, pia hatuwezi kuchunguza Mahusiano ya kimataifa.

20231027_093446.jpg

Jovina Muchunguzi - haki za binadamu na biashara

Tunafanya kazi na CSO nyingi katika kusisitiza agenda ya biashara na haki za binadamu.

Tanzania ni mdau mkubwa wa ajira. Katika hilo watu wanaajiriwa na kuwekeza katika miradi mbalimbali. Kupitia biashara watu hupata kipato na miundombinu inaboreshwa. Hizi ni athari chanya za biashara.

Shughuli za biashara zina upande mbaya pia ambayo ni pamoja na migogoro ya ardhi na uchafuzi wa mazingira. Aidha kuna usimamizi mbovu hasa kwenye viwanda. Pia kuna malalamiko ya haki za kazi ikiwemo kukosa mikataba, kukosa likizo na kuwa na unyanyasaji wa kingono kazini.

Tunajumuisha masuala yote haya jinsi yanavyoathiri Haki za Binadamu. Tunapoenda sasa ndio tunakutana na dijitali kama ambavyo inaendelea hivi sasa, hata bodaboda anahusika na mtandao kupitia Uber au Bolt, hata upande wa chakula nk. Katika huu mlolongo (value chain), tunaangalia kama hakuna kitu kinafanyika bila kutumia dijitali. Wengi mmezungumzia privacy, ni haki ya binadamu.

Kuna madhara mengine makubwa ambayo yanagusa makampuni yote. Kwa sababu hiyo tukaletewa Miongozo ya Umoja wa Mataifa kuhusu Biashara na Haki za Binadamu (UN guide of business and human rights), ambayo hii ina misingi mitatu ya kuhakikisha biashara na watu. Hii ni pamoja na:

1. Kuwa na kanuni za kusimamia sera na sheria za kusimamia biashara na haki za binadamu.

2. Msingi wa pili unaelekeza kila mfanya biashara au muwekezaji kuheshimu Haki za Binadamu.

3. Msingi wa tatu unazungumzia kuwa na mifumo ya kuweza kutatua migogoro na kusimamia haki. Ambazo ni pamoja na judicial, state based non-judical kama TIRA na NEMC, na pia watato ni non-state non-judical ambapo CSO zinaingia humo.

Tume ya Haki za binadamu tunaona mwanya katika maeneo mbalimbali ambapo ni pamoja na kukosa muongozo wa kusimamia biashara na haki za binadamu. Hakuna National Action plan ya biashara na haki za bianadamu.

Pia watu wengi hawana uelewa wa Miongozo hiyo ya UN. Watu hawajui kipi kiende Tume, Mahakamani au sehemu nyingine.

Pia jamii haihamasishwi kuhusu maendeleo na wawekezaji wenyewe wanaona shida kukaa siku nzima kujifunza vitu hivi. Aidha makundi yenye mahitaji maalum ni waathirika wakubwa.

Nani anatakiwa kutelekeza hizi haki za binadamu na biashara? CSO wana nafasi kubwa ya kutekeleza hili mbali na wadau wengi waliopo. Ambapo CSO wanaweza kuzungumza na kampuni na kuwaelewesha kuhusu haki za binadamu.

Tunaona kazi zenu mbalimbali kama haki rasilimali, haki madini nk, kwa hiyo hata hili la haki za binadamu na biashara twende nalo.

Tuna uhitaji mkubwa wa mpango wa haki za binadamu na biashara. Ili tuwe na mpango tunajua tutahakikisha uwajibikaji kwa wadau. Pia itakuwa inawawezesha wote waliochwa nyuma na uwekezaji na itakuwa na namna ya kuibua kesi nyingi zinazohusika uvunjwaji wa haki za binadamu.

Tume ya Haki za binadamu, imepeleka waraka serikalini kuhitaji Action Plan, kwa kuwa sisi tunaishauri serikali na leo tunafanya validation ya concept note ya haki za binadamu na biashara.

Kwa hiyo tumeonesha nia ya kwenda kuwa na mpango mkakati wa haki za binadamu na biashara.

Katika mpango huu tutakuwa na steering commitee, nk, tunatarajia kuwa na ushirikishwaji mkubwa wa CSO. Wengi wenu tuliwashirikisha mwaka 2017 lakini tutapitia upya mwaka huu kwa kuwa kuna mabadiliko mengi yametokea tangu 2017 ili tuje na vipaumbele vya kuwa navyo katika mpango wa kitaifa.

Tutafuata hatua zote kwa mapango kuwa shirikishi katika mchakato huu.

20231027_100208.jpg

Maxence Melo - Mkurugenzi Mtendaji JamiiForums
Hali ikoje kuhusu haki za binadamu na biashara

Katika mchakato huu wa kuwa na mpango ni muhimu kuingiza pia suala la uchafuzi wa kidijitali (digital pollution). Katika ulimwengu huu tumeingiziwa vitu vingi vya kidijitali lakini ni uchafu ambapo lazima kuwe na wataalamu watakaozungumzia kuondoa uchafu kwenye dijitali.

Jambo lingine ni suala la kodi, kuna kodi nyingi sana utadhani dijitali ni kitu pekee cha kukitoza kodi. Tumegeuzwa kuwa sehemu ya kutozwa zaidi.

Kuna uelewa mdogo wa masuala ya dijitali ambapo kuna ukusanyaji wa taarifa za watu binafsi za watu kupita kiasi; ni muhimu kuwa na Sera ya suala la Akili Bandia (AI policy). Hatuna utaratibu wa Kitanzania unaoeleweka ambayo inatufanya kuwa bidhaa katika ulimwengu wa kidigitali.

Aidha watu wenye ulemavu wana changamoto kubwa sana kwenye dijitali hivyo mchakato uwashirikishe, wasisemewe, waseme wenyewe nini wanatamani kiwemo.

Kumekuwa na tabia ya kuwa na 'wadau wa kimkakati' ambao wanatugharimu sana. Yaani mnafanya jambo halafu mnasema wadau walishirikishwa ambao wadau hao ni wa kimkakati sio wadau halisi.

Tunaenda kuwa na watu wengi mtandaoni lakini kutakuwa na namna ya kuminya uhuru wa watu mtandaoni. Tunategemea tume mtusaidie ikitokea hali kama hii.

Nadhani pia ni muhimu kupigania haki hata za mahakama maana kuna wakati nao wanakuwa na changamoto. Ni jukumu letu kulinda katiba yetu.

Sisi JamiiForums tupo tayari kutoa ushirikiano mkubwa katika suala zima la haki za faragha na taarifa binafsi za watanzania.

Kipindi cha Maswali na Majibu
Maswali
Mchango kutoka kwa Mabala;
Nimeona linapokuja suala la uwekezaji ni muhimu mtu awe na kiwango cha maisha aliyokuwa nayo badala ya kulipa ardhi kwa bei aliyonunulia. Mara nyingine wamenunua kwa bei kubwa zaidi. Wananchi huwa wanaonewa na wanatishwa kuwa marufuku kuita waandishi wa habari. Kwa hiyo ni muhimu kuhakikisha uwekezaji hauharibu maisha ya watu. Kuna wengine ni wazee ambao kwa fidia ndogo, wanashindwa kujenga nyumba nyingine.

Mchango kutoka kwa changiaji mwingine;
Tunafanya baishara na watu wenye elimu kubwa. Mfano, wafanyabiashara wa Mtwara wana elimu ndogo kuliko wanaonunua korosho. Hivyo kama tume mnafanyaje kuhakikisha elimu ya biashara inakuwa kwa wote.

Swali kutoka kwa mshiriki;
Tutegemee lini tutakuwa na mpango uliokamilika? Maana mchakato wa kuwa na mpango mkakati ulianza tangu 2017.

Swali jingine;

Ni kwa namna gani CHRAGG wanafanya ushikishwaji wa watu wenye ulemavu katika kutengeneza hiyo Action Plan?

Geofrey Julius;
Kuna mkakati gani wa kudhibiti mbegu zenye madhara za GMO ambazo zimeonesha katika biashara zinaathiri kwa kiasi kikubwa mambo kadhaa ikiwemo nguvu za kiume?

Majibu
Jovina;

Bado hatujawa na maeneo maalum yaliyopangwa kufanyiwa kazi. Hivyo hatuna suala la kujua kipi ni kipaumbele. Tukifanya ushirikishwaji tutajua kuwa tunahitaji nini kuhusu kilimo elimu nk.

Mchakato wa 2017 haukuwa Mpango bali ni kama vikao vya mara kwa mara vinavyokaliwa.

Kuhusu ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu, tumepokea na kutakuwa na ushirikishwaji.

Munisi;
Kuhusu alichozungumzia Mabala; sheria ziko wazi kuhusu fidia. Hata sisi tunajua kuwa viwango vya fidia ni vidogo. Kwa hiyo tumeshauri serikali kubadili viwango vya tozo mbalimbali na kodi ili wananchi wasiumie. Tunaendelea kushauri viwango vya fidia vibadilike ili vikidhi hali halisi ya maisha.

Maswali
Aidani Eyakuze;
Tunawezaje kuhakikisha tunashawishi Sera za Kimataifa kudhibiti Akili Bandia (AI) ili zifanye maamuzi bila kudhuru maisha ya binadamu?

Swali jingine;
Tume imesema inafanya tafiti, je ni kwa kiasi gani wanazitoa tafiti hizo kwa wengine?

Mchango;
Nadhani kwenye suala la uelimishaji, ni muhimu kuishirikisha vyombo vya habari kimkakati, sio kama ilivyo hivi sasa, vyombo vinashirikishwa kwenye makongamani na utoaji wa matamko. Ni muhimu vyombo vya habari vielimishwe na kushirikishwa kimkakati ili kusiaide kwenye kuelimisha umma.

Swali kutoka kwa Mariam Rashid;
Je, haki za binadamu zinamshirikishaje mfanyabaishara mdogo? Halmashauri nyingi hazifanyi ushirikishwaji kwa wafanyabaishara wadogo matokeo yake kunakuwa na ushuru mkubwa kwa wafanyabiashara ambao hawatengenezi faida. Unaenda sokoni mtu analipa kodi zaidi ya elfu 19 kwa mwezi wakati maparachichi yameoza. Ni vyema mshirikiane na halmashauri kujua wanapata shilingi ngapi ili kuweka tozo na kodi ambazo zinaendana na wanachokipata wafanyabiashara wadogo. Ushirikishwaji wa sasa kwa wafanyabiashara wadogo hauridhishi.

Majibu
Maxence Melo:

Suala la Akili Bandia (AI) alilouliza Aidan ni lazima tujue kuwa tunapoangalia dijitali kwa kuzingatia AI haifanyi kazi bila data lakini sheria na sera zetu haziangalii AI.

Aidha kwenye suala la uchafuzi wa kidijitali ni kuwa; mfano mmesikia iPhone 15 imetoka na unakuta mtu anauza iPhine 15 kwa shilingi laki nne na mnanunua lakini zile ni kopi, hazina viwango, ni takataka, kwa hiyo tunakuwa jalala. Mnatumia vifaa ambavyo mara nyingine vinapata moto, vinalipuka ni kwa kuwa havina viwango. Ni uchafu kidijitali na tunakuwa jalala kwa kuwa hatuna mpango wa kuzuia uchafu wa kidijitali.
 
Back
Top Bottom