Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,011
- Thread starter
- #41
MKJJ: Nafikiri the proper heading should have been: Nasitisha..., well, if that's what you meant!
Kusitisha kitu ni sawa kwa kadiri ya kwamba unachositisha si wewe mwenyewe. Ningetaka kusema nasitisha makala zangu ingekuwa sawa kwani ninachositisha ni "makala" yaani kitu kingine. Mtu anasitisha kitu kilicho nje yake.
k.m. Mkuu wa Polisi amesitisha kuendelea kwa mkutano wa vyama vya Upinzani.
lakini twaweza kusema:
Mkuu wa Polisi amesita kwenda kwenye mkutano wa vyama vya upinzani. Kwa maana ya kwamba hatowekwenda, kwamba alikuwa na mpango au alionekana anaelekea huko lakini akakoma.
Katika yote mawili - kusita na kusitisha - maana yake ni wazo nayo ni kukomesha kuendelea kwa kitu fulani kuendelea kufanyika. Neno kusitisha ni kinyume kidogo na neno kuzuia. Unasitisha kitu ambacho tayari kimeanza kufanyika au kiko katika hatua za kufanyika. Wakati kuzuia ni kufanya kitu hata kisianze kufanyika.
Hivyo nimesema "Nasita (yaani mimi) nakoma, nasimamisha, sitoandika n.k..