Nasita kuendelea kuandikia Gazeti

MKJJ: Nafikiri the proper heading should have been: Nasitisha..., well, if that's what you meant!

Kusitisha kitu ni sawa kwa kadiri ya kwamba unachositisha si wewe mwenyewe. Ningetaka kusema nasitisha makala zangu ingekuwa sawa kwani ninachositisha ni "makala" yaani kitu kingine. Mtu anasitisha kitu kilicho nje yake.

k.m. Mkuu wa Polisi amesitisha kuendelea kwa mkutano wa vyama vya Upinzani.

lakini twaweza kusema:

Mkuu wa Polisi amesita kwenda kwenye mkutano wa vyama vya upinzani. Kwa maana ya kwamba hatowekwenda, kwamba alikuwa na mpango au alionekana anaelekea huko lakini akakoma.

Katika yote mawili - kusita na kusitisha - maana yake ni wazo nayo ni kukomesha kuendelea kwa kitu fulani kuendelea kufanyika. Neno kusitisha ni kinyume kidogo na neno kuzuia. Unasitisha kitu ambacho tayari kimeanza kufanyika au kiko katika hatua za kufanyika. Wakati kuzuia ni kufanya kitu hata kisianze kufanyika.

Hivyo nimesema "Nasita (yaani mimi) nakoma, nasimamisha, sitoandika n.k..
 
Sawa lakini inaweza kuchanganywa kirahisi na maana ya kwanza ya kusita, i.e to hesitate.
 
Sawa lakini inaweza kuchanganywa kirahisi na maana ya kwanza ya kusita, i.e to hesitate.

sasa hiyo ni hoja tofauti na ninakubaliana nawe. Lakini kuna katika Kiswahili kucheza na maneno yale yale mara mbili na kuleta maana tofauti kabisa au inayokaribiana lakini ikiwa na msisitizo wa jambo jingine.

Utakutana na maneno kama haya yafuatayo ambayo yanacheza na neno moja mara mbili na kuleta tofauti ya maana:

Amesita - amesitasita
Amecheka - amechekacheka
Yuko Bara - Yuko barabara
Ameruka - Amerukaruka
Kinyume - kinyumenyume

Nadhani hili ni mojawapo ya utamu wa lugha yetu!
 
MMwnkjj

Are u sure si nguvu za ufisadi zinazokufanya kusitisha kuandika makala ktk hilo gazeti unalozungumzia????

MUNGU APISHIE MBALI!!!!
 
Mkuu niliposoma ujumbe nilipata mawazo tofautitofauti kama hivi:

1. Mwanakijiji eshahamia upande wa pili (kwa mafisadi), na tusubiri uteuzi wake tu. Au;
2.Tusubiri kipindi cha miezi sita halafu atatulisha kuwa anaoa-na tusubiri kumchangia- Au;
3.Kuna fisadi eshamuingiza kwenye payroll, na eshazibwa mdomo.Ama
4.Ameamua kuvalia njuga uandishi na anaandika kitabu cha riwaya.

Baada ya kutafakari sana nimehisia kuwa tusubiri tu tutajulishwa muda si mrefu sana kuwa anao!

Kwa wale wanaotatizwa ni kwamba kuna neno kusita na neno kusitasita. Yote yafanana ila siyo sawa. Mwanakijiji hajasitasita. Mwanakijiji amesita.

Labda kamwe hatutafahamu kilichosababisha asite kuandikia gazeti, ila kwa yale aliyokuwa ameweza kuandika nasi tukayasoma miye nasema ahsante mwanakijiji! Muda utakapokuwa muafaka usisite kuchukua kalamu au kiibodi na utujulishe ufikiriacho au kulikoni.
 
Mwanakijiji,

Naungana na mpaka kieleweke kuwa punguza kuandika. Pia punguza kuspin.

Ni heri kabisa upumzike maana wasomaji wameshakuzoea sana. Ila nakiri kuna kundi jipya la akina kubwa jinga ulikuwa bado umewashikaaaaa.

Mapumziko mema buddy.

Kama kawaida nothing personal, najua unanielewa.

FairPlayer
 
natingisha kiberiti huyo Mwanakijiji......kama mtu anasita kuandikia magazeti hayo na bado katuambia ameshachukua uamuzi huoni jamaa huyu anataka tumpigie magoti aendelee?

Mkuu kama kuacha acha tu kimya kimya......
 
Nadhani Mwanakijiji anaomba ushauri kinamna--

Kumuelewa Mwanakijiji haraka ni kazi sana... inabidi upige --the larger moja, kisha uvute tumbaku kidogo... alafu utulie mahali kwenye upepo baridi mwananaa kama kule Lushoto, karibu na kwa...

Otherwise waweza kurupuka tu kujaza kurasa hapa!

Lingine Mwanakijiji amekasirishwa na matatizo ya uongozi CHADEMA, amekosa pa kushikia... kwi kwi kwi
 
Lingine Mwanakijiji amekasirishwa na matatizo ya uongozi CHADEMA, amekosa pa kushikia... kwi kwi kwi
Ni mwanachama pale ? si agombee yeye....sijui kama katokea kaskazini
 
Mwanakijiji Wanatuuliza Kuna Fungu Limemwagwa???????????tugawane!!!!!
Teeehteeeh!!!!!!!!!!!!!!!!!
All Trhe Best Br
 
Mwanakijiji Wanatuuliza Kuna Fungu Limemwagwa???????????tugawane!!!!!
Teeehteeeh!!!!!!!!!!!!!!!!!
All Trhe Best Br
 
FREE MEDIA wamenunuliwa na nani au MWanakijiji ndiyo kanunuliwa?

Kamanda mkjj, mbona hawa jamaa wanakupeleka pabaya. si muda watakufananisha na mtikila. Hebu weka wazi, ututoe mashaka wapiganaji!!!
 
Katika haya mambo ya kuomba mikopo nadhani RA anaweza akawa mtu wa kusaidia. Naweza kuelewa predicament ya Mtikila. Anapambana lakini akiomba msaada wa kufanikisha mambo yake au kufanya anayoyafanya yawe rahisi hakuna anayejitokeza kumsaidia hata kama wanapenda anachofanya.

Sasa ametingwa na anahitaji msaada kwanini asiende kwa "Baniani mbaya"? I'm telling you kuna wakati mambo yanakuwa magumu na hakuna ujanja isipokuwa kupiga magoti kwa fisadi. Je mtu akifanya hivyo alaumiwe?

Wengi hapa tunaifurahia JF lakini ni wangapi wamekuwa wakijitolea kusaidia kwa namna yoyote ile ukiondoa watu wale wale kam 10 hivi kati ya 5000? Je wale wanaoisimamia wakiwa na shughuli zao na mambo yao binafsi yanakwama kwa sababu ya JF wakiomba msaada kwa fisadi waupokee? waukatae?

Ndio maana kuna mtu mmoja aliwahi kusema katika hali hiyo "Uzalendo unamshinda"!

akija RA au EL na kusema Mwanakjj nasikia mambo yako yanaenda kombo.. niko tayari kukusaidia 3000 grand, no strings attached mtanishauri nizikatae wakati mwanangu amelezwa hospitali na shemeji/wifi yenu mkubwa kibarua kimeota nyasi? are you kidding me?

I'm just saying... JF, KLH, kuandika na kupiga kelele can do you so much except feed your family and pay your bills!
 
Ol the best mzee na mipangilio yako mengine ya baadae...hope yote ni mema na yanalenga kulikomboa taifa letu
 
Ni jambo la kusikitisha lakini kila mtu ana maamuzi yake binafsi, na askari halazimishwi kubikaga anaweza kukugeuzia silaha au akawa mamruki!
Lakini kumbuka kuwa kuandika ktk JF sio wengi watapata ujumbu, hivyo kumbuka kuwa any means ambayo utatumia iwe na athari katika jamii ya wanyonge sababu ukitazama watu wengi wa JF mpo mamtoni sisi wanyumbani siunajuea tena kodi kubwa.
Kuna jamaa kaniambia RA offer yake kwako kuwa uchague jimbo lolote lile Tanzania utakuwa mbunge na uwaziri mkuu absolute garantee MMJ usituangushe ukiulamba uwazili mkuu nadhani utatusaidia sana maana tutaokoa hivi vijesenti vyetu tunavyo lipa katika mtandao na utakuwa mwisho wa JK na wanamtandao wote.
Nachukua fulsa hii kukutakia safari njema lakini silaha mkononi sio kibindoni!
 
"Wengi hapa tunaifurahia JF lakini ni wangapi wamekuwa wakijitolea kusaidia kwa namna yoyote ile ukiondoa watu wale wale kam 10 hivi kati ya 5000? Je wale wanaoisimamia wakiwa na shughuli zao na mambo yao binafsi yanakwama kwa sababu ya JF wakiomba msaada kwa fisadi waupokee? waukatae?"

NIMEGUSWA.
ASANTE KWA KUNIKUMBUSHA WAJIBU WANGU KABLA YA KUSEMA AU KUANDIKA.
INVISIBLE NAOMBA MUONGOZO WA KUCHANGIA DUNDULIZO LANGU.

OMUTWALE SSEBO
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom