MALENGO NA MIPANGO

Richard mtao

JF-Expert Member
May 13, 2018
209
236
Habari ya wakati mwana jF.
Kama mjuavyo mwaka 2023 umebakiza masaa kadhaa ili uishe.

Watu wengi katika mitandao ya kijamii wanafurahia kuumaliza mwaka huu kwa namna tofauti tofauti, kuna waliotimiza mipango na malengo yao, kuna walioshindwa kutimiza malengo yao kwa namna mbalimbali, kuna wanaopitia magumu kiasi kwamba hata wamekosa maneno mazuri ya kuonesha kwamba nawao wapo na wanashukuru kwa kufika mpaka hatua hii.

Hoja yangu imejikita kwa haya makundi matatu ya watu niliowataja hapo juu kwa lengo la kukumbushana, kuhimizana na kutiana moyo, kwakua maisha ni fumbo ambalo linahitaji fikra pevu na hekima kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili kulifumbua.

KUNDI LA KWANZA:Waliotimiza mipango na malengo yao.
Kwanza kabisa nianze kwa kuwapongeza wote ambao kwa namna moja ama nyingine mmeweza kufikia malengo yenu kwa kiwango ambacho mlikitarajia, kwakua sio kila mmoja ameweza kutimiza malengo au mipango yake.
Ni wazi kwamba katika kufikia mafanikio yenu mlijinyima, mlijitoa, mlikubali kudharirika, mlikubali kuitwa majina ya ajabu ikiwemo mabahili na kadharika lakini hamkukata tamaa na ndio maana leo tunapoenda kuukamilisha mwaka 2023, Mpo na furaha zote kwakua malengo mlioyaweka wakati tunauanza mwaka huu yametimia.

Ujumbe wangu kwenu:- Kuyafikia malengo yenu kwa mwaka 2023 hakuwafanyi kuwa manabii( au watu wenye uwezo mkubwa kuliko watu wote) Hivyo mjitahidi kusimamia misimamo yenu lakini pia Muendelee kuweka mipango na malengo ya kimkakati ili kuendeleza mafanikio hayo na kuanzisha mambo mengine makubwa yatakayowafikisha mbali zaiid kuliko hapo mlipo hivi sasa.

KUNDI LA PILI: Walioshindwa kutimiza malengo.
Wakati tunauanza mwaka 2023 kuna watu tulijiwekea Malengo ya kuyafikia lakini kwasababu mbalimbali zilipelekea tushindwe kufikia malengo hayo.
Niseme tu wewe sio wa kwanza kushindwa kutimiza malengo yako kwa mwaka huu kuna wengi waliofanikiwa kwa Mwaka huu lakini walifululiza kufeli kwa miaka kadhaa iliyopita, Ninamaanisha kwamba kufeli kwako haijalishi ni mara ngapi hupaswi kuchoka wala kukata tamaa.
Unachopaswa kufanya kabla hujaweka malengo kwa mwaka 2024:-
Kwanza, Jiulize unataka nini?
Pili, rejea mpango wako wa mwaka uliopita ili ubaini nini kilikuwa kikwazo mpaka kupelekea kufeli.
Tatu, Weka malengo ambayo yanafikika na yanayoweza kupimika kwa mwaka 2024.
Nne, Andaa Muundo wa utelekezaji wa malengo yako na katika hili zingatia zaidi muda wa marejeo pamoja na usimamizi(plan review and monitoring) ili kubaini changamoto kwa wakati na kuzitatua.
Tano, Hakikisha unafanya maboresho ya mpango pale inapobidi kama kuna sababu za kufanya ivo.

Lakini kumbuka kila unapopanga Mipango yako, Shetani huwa yupo kukuharibia kwaiyo hakikisha kabla hujafanya chochote Mtangulize Mungu kwanza.

KUNDI LA TATU: Wanaopitia Magumu Maishani.
Kundi hili ni kubwa kuliko makundi yote kwakua kila mmoja katika maisha anapitia magumu yake.

Lakini kwa maana ya Makala hii, kundi hili ni la wale watu wenye Magonjwa Makubwa, Majanga Makubwa( kama wenzetu wa Hannag), Watu waliopata ulemavu wa kudumu, Watu waliokata tamaa, Wafungwa, Mayatima na watu wote wenye uhitaji maalum ambao kwao sio rahisi sana kuweka malengo au kuyafikia kabisa.

Nikweli yawezekana una jambo fulani ambalo kwa namna moja ama nyingine linakufanya ujione huna uwezo wa kufanya chochote lakini nakwambia hapana, nasema ivyo kwasababu kila kitu kinawezekana kama utakuwa tayari, kujitoa na kumtegemea Mungu.
Tazama(WAFILIPI 4:13)
Wafilipi 4:13
Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

Hili ni fungu kutoka katika biblia takatifu, Huu ni ushuhuda kwamba Mwenyezi Mungu anatambua Magumu yetu tunayopitia na yuko pamoja nasi katika kuyashinda yote hayo.
Wakati mwingine Mungu anaruhusu jaribu fulani katika maisha yako kwasababu, hivyo kwa wewe ndugu yangu ambae kwa namna moja ama nyingine umekata tamaa unaona huwezi Nakwambia sasa unaweza.
MUALIKE MUNGU katika maisha yako sasa, weka malengo yako kwa kuzingatia mazingira yako na uhitaji wako nae atafanya muujiza katikati ya juhudi zako.

Nasisitiza sana ndugu yqngu usikubali kwa vyovyote kukaa tu bila kuweka lengo.
Mfano wenzetu wagonjwa unaweza kujiwekea lengo la kupona haraka kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya na kujitunza ili upone haraka na kuweza kuendelea na shughuli zingine.
Yawezekana mfano huu usiwe halisia saana lqkini nachotaka uelewe ni kwamba Kila kitu kinawezekana kqma utaamua na kumshirikisha Mungu ili akufanikishie kwa pale utapoishia.

Mfano mwingine ni kwa Ndugu zetu walioathirika huko Hannag.
Nikweli ndugu zetu wamepatwa na janga kubwa sana na limewaathiri pakubwa sana kiasi kwamba hata kuelezea inaniwia vigumu sana lakini kwa maana ya kutiana moyo.

Napenda kuwapa pole waathirika wote, lakini pamoja na hayo nawatia moyo kwamba Mungu yupo na anaona magumu wanayopitia kwasasa hivyo ni jukumu la kila mmoja ambae ameathirika na janga hilo kuamka na kujipanga upya kwa kuweka malengo ili kufufua nuru ya maisha yao. Kwasababu tusipofanya ivo hatutakuwa tumefanya kitu kwajili ya vizazi vyetu au taifa letu.
Tupange, tuweke malengo na tuyatelekeze kwakua baraka za Mungu zinatusubili tuanze utekelezaji ili zitumiminikie.

HITIMISHO.
Baada ya kusema hayo nawashukuru wote kwa kusoma makala yangu hii yenye mmbaraka kwako na maisha kwa jumla.

Hakikisha unaweka malengo Mahususi,yanayopimika, yanayoweza kufikikika, halisia na kwa wakati maalumu. Lakini pia jitahid sana kuzingatia mahitaji ya moyo wako wakati unaunda malengo yako.

Mungu akubariki sana katika malengo yako kwa mwaka 2024.
 
Bless
 
Back
Top Bottom