Nasimama na Rais Magufuli kwenye kuchukua tahadhari dhidi ya Corona na napinga matumizi ya chanjo inayopigiwa kampeni na dunia

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
19,760
35,205
Rais John Pombe Magufuli ametoa msimamo wa taifa kuhusiana na maambukizi ya Corona pamoja na chanjo inayopigiwa kampeni na dunia kwamba kila nchi lazima ipatiwe chanjo hiyo.

Watanzania wengi wamemuelewa Rais na wanachukua tahadhari na pia wameelewa msimamo wa Rais kuhusu chanjo ya Corona. Ila penye wa kuelewa na wakupinga hawakosekani, na kuna watanzania wengi haswa wenye itikadi tofauti za kisiasa wanampinga Rais tena wakitumia nguvu kubwa sana kuhamasisha watu wakachanjwe.

Mimi binafsi nina maswali machache kuhusu hiyo chanjo:

1. Imetumika wapi kama majaribio na matokeo yake ni yapi hadi tuje kuchomwa huku kwetu? Tusisahau mwaka Jana walisema kabisa chanjo ingepatikana ilitakiwa ianzie kutumika Africa wakatoa sababu eti kuna uhaba wa health facilities kwa hiyo kukinga ni bora kuliko kutibu, sasa wameona ngoma imegoma na waafrika hawajaathirika kwa kiasi kikubwa walivyotaka bado wanalazimisha, kulikoni?

2. Wakati UK wanareport wastani wa vifo 1000 kwa siku, USA wao wana wastani wa vifo 4000 kwa siku. Kwanini wasitoe hiyo chanjo kwenye hizi nchi zilizoathirika zaidi ili kuonyesha effectiveness ya chanjo na kutokomeza vifo kabla ya kuja Africa?

3. Wataalamu wa mfumo wa upumuaji wanasema hakuna chanjo inayoweza kupambana na virus vya mfumo wa upumuaji kwa 100%, wanasema kama kuna chanjo inaweza kuwa effective 50% 60% ila kikubwa wanachoshauri ni wanadamu kubadili mfumo wa maisha ikiwa ni pamoja na Kula, kunywa na kubadili tabia zinazoweza kuchochea maambukizi. Je, kwanini WHO hawatumii nguvu kubwa kutoa hii hamasa kwa dunia kama wanavyohamasisha chanjo?

4. Tumsikilize Mtanzania mwenzetu hapa chini na tutafakari huu upendo mkubwa hivi kwa mataifa yaliyoendelea wa kutaka kutulinda ili tusife wakati wao wanakufa kila siku tena kwa maelfu unasababishwa na nini?

I STAND WITH MY PRESIDENT JOHN POMBE MAGUFULI

Pongezi kwa serikali ya Zambia kwa kuvunja ukimya

MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRIKA🙏
 
Wanaopanga kupunguza waafrika billion3 ndio haohao watoa chanjo

RAIS MSTAAFU MZEE JAKAYA "Za kuambiwa changanya na zako"
 
Mi umeniambia, ngoja nichanganye na zangu ntaleta mlejesho. Ila mabeberu Mungu anawaona. Na safari hii yuko upande wetu ,tuendelee kuchukua tahadhari na taratibu za kiafya tunazoshauriwa.
 
Kweli hizi chanjo tuwe nazo makini siyo kukurupuka....hata mimi binafsi namuunga mkono Rais jinsi anavyo deal na hali ya Corona

Hebu ione na uiskilize vizuri hii video clip
mama D

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Kwanza africa hatufiki bil 3. Labda waue hadi kizazi cha 5.

Then kuuwa watu bil 3. Ni sawa umeua nusu au robo 3 kabsa ya dunia nzima.
Hiyo ni plan endelevu sio kuua kwa siku moja.
 
Kingine hyo kinga. Huwez kuletewa bila WHO kuthibitisha. Na hyo kinga itakuwa worldwide. Atake meza mjapan ndio utakao meza wewe.

Kingine chanjo sio lazima. Ni kama chanjo zingine tu. Ukitaka unachukua ukitaka huchukui.

Mpaka sasa chanjo ni nyingi. Lakini bado bado hawajathibitisha. Ipi itolewe kwa watu wote.
 
Kama ni hIvyo ni bora kutotumia vitu vyote vya nje ya Afrika.

Kama wakitaka kutua nazani kuna njia nyingi tu, mfano wanaweza kusitisha kutupa ARV.

Nazani tunapaswa kuangalia kwa jicho la 3 swala kama hlo.

Labda useme ni bora tusianze kutumia mpka mataifa mengine waanze kutumia.
Hiyo ni plan endelevu sio kuua kwa siku moja
 
Unaweza kuwa na hoja ya msingi kwenye hili, ila nilitegemea busara na uchambuzi wa kisayansi zaidi kama Nchi kwenye kupinga hii chanjo, tupende tusipende hili gonjwa lipo na linaua, suala la kutulazimisha sisi huku Africa tuchanjwe haliwezi kuepukika maana muingiliano baina ya Nchi na Nchi ni mkubwa sana, haitakuwa na maana wao wachanjwe halafu sisi tubaki kama tulivyo.

Nikija kwenye hii hoja kwamba wanataka kutumaliza, hoja kama hii haiajaanza leo, ilianza kipindi gonjwa la ukimwi lilipochachamaa, lakini kwa busara zao hao wanaotaka kutumaliza, wametuletea ARVs ambazo kwa kiasi kikubwa zimesaidia kutubakisha hai, leo iweje kwenye COVID 19 ndio watumalize?

Nikija kwenya malaria, hawa jamaa wametulete vyandarua, wametoa billions of money kwa ajili ya kampeni za kutokomeza malaria, japo inafahamika vyanzo vya mazalia ya mbu ni uchafu, kwanini kama kweli tuna shaka na tiba zao tusionyeshe hata mifano ya sisi kujikinga ili wasituingilie?

Africa ilipofikia kwa sasa, hakuna namna tutaruka maamuzi ya hawa jamaa, watakachotaka tutafanya, tupende tusipende.

COVID 19 Is real, tuchukue tahadhari wakuu.
 
Ukifuatilia sana hii ishu mfano pale Uingereza selikali iliingia kwenye mgogoro na kampuni inayotengeneza hii chanjo kwa madai ni kwa usalama wa taifa.

Baadae umoja wa Ulaya wakasema mazungumzo yanafanyika.

Mpaka sasa hivi haieleweki ni usalama upi uliosababisha huo mgongano.

Kama kawaida JPM atakuja kueleweka baadae sana.
 
Kingine hyo kinga. Huwez kuletewa bila WHO kuthibitisha. Na hyo kinga itakuwa worldwide. Atake meza mjapan ndio utakao meza wewe..

Kingine chanjo sio lazima. Ni kama chanjo zingine tu. Ukitaka unachukua ukitaka huchukui.

Mpaka sasa chanjo ni nyingi. Lakin bado bado hawajathibitisha.. Ipi itolewe kwa watu wote
Kuna ukoo nawajua huwa hawakubali chanjo yoyote. Wazee wao wananiambia walizaliwa miaka ya 1940s na wao hawajawahi pewa chanjo wala watoto wao, wala wajukuu, wala vitukuu. Sio chanjo ya ndui sijui surua wala TB.

Ukiangalia vizuri sio unaweza ukatamani kufanya uchunguzi zaidi sababu upo ukweli kwamba waliochanjwa chanjo ya TB bado wanaugua TB na wapo wasiochanjwa na hawaugui

Tusikubali chanjo kama fashion, tuhoji na kujiridhisha kwamba hizo chanjo zina faida au hasara na tuchague mbadala kama upo.
 
Kila kukicha mzungu hufikiri afanye nini apate Mali za bule kutoka Africa, Mwafrica Naye kila kukicha hufikiri ni kwa namna Ipi aweze kuomba cha kumsaidia Kutoka Kwa mzungu.

Mzungu anapotengeneza Jambo lake, Africa ijiandae kulikubali Kwa lazima, na hata asiyeumwa atameza tu dawa nakwambia!

Eti mtafungiwa kuingia nchi zao! Duh.
 
Kama ni hvyo ni bora.. Kutotumia vitu vyote vya nje ya africa.

Kama wakitaka kutua nazani kuna njia nyingi tu..mfano wanaweza kusitisha kutupa ARV

Nazani tunapaswa kuangalia kwa jicho la 3 swala kama hlo.

Labda useme ni bora tusianze kutumia mpka mataifa mengine waanze kutumia
Hoja ya msingi chief, hilo la ARV ndio hasa wangetupatia hapo, sema waafrika tuna gubu,shida zetu lakini maneno mengi.
 
Unaweza kuwa na hoja ya msingi kwenye hili, ila nilitegemea busara na uchambuzi wa kisayansi zaidi kama Nchi kwenye kupinga hii chanjo, tupende tusipende hili gonjwa lipo na linaua, suala la kutulazimisha sisi huku Africa tuchanjwe haliwezi kuepukika maana muingiliano baina ya Nchi na Nchi ni mkubwa sana, haitakuwa na maana wao wachanjwe halafu sisi tubaki kama tulivyo.

Nikija kwenye hii hoja kwamba wanataka kutumaliza, hoja kama hii haiajaanza leo, ilianza kipindi gonjwa la ukimwi lilipochachamaa, lakini kwa busara zao hao wanaotaka kutumaliza, wametuletea ARVs ambazo kwa kiasi kikubwa zimesaidia kutubakisha hai, leo iweje kwenye COVID 19 ndio watumalize?

Nikija kwenya malaria, hawa jamaa wametulete vyandarua, wametoa billions of money kwa ajili ya kampeni za kutokomeza malaria, japo inafahamika vyanzo vya mazalia ya mbu ni uchafu, kwanini kama kweli tuna shaka na tiba zao tusionyeshe hata mifano ya sisi kujikinga ili wasituingilie?

Africa ilipofikia kwa sasa, hakuna namna tutaruka maamuzi ya hawa jamaa, watakachotaka tutafanya, tupende tusipende.

COVID 19 Is real, tuchukue tahadhari wakuu.
Mkuu kwenye kipengele cha UKIMWI unahisi huu ugonjwa hautumalizi? Ulishawahi kujiuliza wakisitisha hizo dawa nini kitatokea?

Imefika hatua sasa hivi mfano maeneo ya vijijini watu wanaishi kwa madawa yani kuna vijiji robo tatu nzima wana ngoma na bila madawa hawaishi.

Mzungu kama aliweza kutucolonize kamwe hawezi kushuhudia ustawi wetu
 
Kama ni hvyo ni bora.. Kutotumia vitu vyote vya nje ya africa.

Kama wakitaka kutua nazani kuna njia nyingi tu..mfano wanaweza kusitisha kutupa ARV ..

Nazani tunapaswa kuangalia kwa jicho la 3 swala kama hlo..

Labda useme ni bora tusianze kutumia mpka mataifa mengine waanze kutumia
Wameanzia mbali sana hawa, tangu kwenye ukimwi, kutuletea mbegu za kisasa za mazao na kuua mbegu zetu za asili, kuhamasisha mapenzi na mahusiano ya jinsia moja ili tusizaliane, ila bado Mungu anatupigania
 
Hata Kwa bunduki sichanjwi! Na kama serikali itaagiza chanjo, kama Tanzania tuko 60M. Waagize pungufu ya mtu mmoja!

Wizara shikilia Hilo!
 
Back
Top Bottom