Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi ya Shule afikishwa Mahakamani kwa kutaka kumhonga Afisa wa TAKUKURU

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Morogoro, imemkamata na kumfikisha mahakamani Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa shule, Suleiman Mwishehe kwa tuhuma za kujaribu kumhonga Afisa wa TAKUKURU kwa kutoa shilingi Milioni 3 ili asifikishwe mahakamani wakati wa uchunguzi kwa ubadhilifu wa shilingi milioni 90 za ujenzi kwenye Kijiji cha Mlilingwa wilayani Morogoro.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Morogoro, Manyama Tungaraza amesema hayo katika taarifa yake ya utekelezaji wa kazi kwa kipindi cha kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba 2023 ambapo amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa kwenye ofisi za TAKUKURU alipoenda kupeleka kiasi cha shilingi Milioni 3 kati ya tano alizoshawishi awali kuwa atampa ili asifikishwe mahakamani.

Tungaraza alisema mshtakiwa huyo ambaye pia ni Mlezi wa kikundi cha Bosi Kuku Group alikiri kosa na kutiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya shilingi laki tano ambapo alilipa faini huku fedha alizotoa kama hongo kutafishwa na kuwa mali ya Serikali.

Hivyo Mkuu huyo alitoa onyo kwa wananchi kutojaribu kushawishi au kutoa hongo kwa watumishi wa TAKUKURU mahali popote kwa lengo la kuharibu uchunguzi au ushahidi wa tuhuma zozote zinazochunguzwa na sababu hatua kali za kisheria zitachukuliwa kama ilivyokuwa kwa mtuhumiwa huyo.

Hata hivyo alisema mtuhumiwa huyo amefunguliwa jarada lingine mahakamani la kesi ya ubadhilifu wa Milioni 90 zilizoidhinishwa na kungizwa kwenye akaunti yake kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya walimu na chumba cha darasa ambao ulitakiwa kuwa umeshakamilika huku ukiwa bado haujakamilika.
 
Kwahio milion 90 za serikali ziliidhinishwa kuingia kwenye akaunti ya mtu binafsi?

Hapo kuna tatizo kubwa sana na sio peke yake
 
Hiyo hukumu nimeipenda miaka 2 gerezani au laki 5 !!,bora zingekuwa dollar za kimarekani ningejua kuwa hukumu zimepitwa na wakati.
 
Selemani wee seele! Seele! Seele! Mbona kama una laana Seele ooooh sele unaleta lawama seele aaaagh seleee
 
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Morogoro, imemkamata na kumfikisha mahakamani Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa shule, Suleiman Mwishehe kwa tuhuma za kujaribu kumhonga Afisa wa TAKUKURU kwa kutoa shilingi Milioni 3 ili asifikishwe mahakamani wakati wa uchunguzi kwa ubadhilifu wa shilingi milioni 90 za ujenzi kwenye Kijiji cha wilayani Morogoro.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Morogoro, Manyama Tungaraza amesema hayo katika taarifa yake ya utekelezaji wa kazi kwa kipindi cha kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba 2023 ambapo amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa kwenye ofisi za TAKUKURU alipoenda kupeleka kiasi cha shilingi Milioni 3 kati ya tano alizoshawishi awali kuwa atampa ili asifikishwe mahakamani.

Tungaraza alisema mshtakiwa huyo ambaye pia ni Mlezi wa kikundi cha Bosi Kuku Group alikiri kosa na kutiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya shilingi laki tano ambapo alilipa faini huku fedha alizotoa kama hongo kutafishwa na kuwa mali ya Serikali.

Hivyo Mkuu huyo alitoa onyo kwa wananchi kutojaribu kushawishi au kutoa hongo kwa watumishi wa TAKUKURU mahali popote kwa lengo la kuharibu uchunguzi au ushahidi wa tuhuma zozote zinazochunguzwa na sababu hatua kali za kisheria zitachukuliwa kama ilivyokuwa kwa mtuhumiwa huyo.

Hata hivyo alisema mtuhumiwa huyo amefunguliwa jarada lingine mahakamani la kesi ya ubadhilifu wa Milioni 90 zilizoidhinishwa na kungizwa kwenye akaunti yake kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya walimu na chumba cha darasa ambao ulitakiwa kuwa umeshakamilika huku ukiwa bado haujakamilika.
Mwenyekiti huyo pia ni Katibu wa Tawi la CCM Kijiji cha Mlilingwa
 
Kwahio milion 90 za serikali ziliidhinishwa kuingia kwenye akaunti ya mtu binafsi?

Hapo kuna tatizo kubwa sana na sio peke yake
Naunga mkono hoja kuna watu wapo nyuma yake huyu ni mbuzi wa kafara tu. Milioni 90 mwamba kawekewa kwenye akaunti hivihivi tu aaah hapana kwanini zisiingizwe kwenye akaunti ya shule?
 
Rc mmoja mkoa wa mwanza alifanya madudu kama hayo kukazimisha madiwani waingize fedha za ujenzi wa madarasa ya Uviko 19 kwenye account ya mtu binafsi. Nini kilimtokea
 
Tatizo na yeye ametoa dau dogo. Yaani ubadhirifu wa milioni 90 halafu unatoa hongo ya milioni 3 tu!!
 
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Morogoro, imemkamata na kumfikisha mahakamani Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa shule, Suleiman Mwishehe kwa tuhuma za kujaribu kumhonga Afisa wa TAKUKURU kwa kutoa shilingi Milioni 3 ili asifikishwe mahakamani wakati wa uchunguzi kwa ubadhilifu wa shilingi milioni 90 za ujenzi kwenye Kijiji cha Mlilingwa wilayani Morogoro.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Morogoro, Manyama Tungaraza amesema hayo katika taarifa yake ya utekelezaji wa kazi kwa kipindi cha kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba 2023 ambapo amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa kwenye ofisi za TAKUKURU alipoenda kupeleka kiasi cha shilingi Milioni 3 kati ya tano alizoshawishi awali kuwa atampa ili asifikishwe mahakamani.

Tungaraza alisema mshtakiwa huyo ambaye pia ni Mlezi wa kikundi cha Bosi Kuku Group alikiri kosa na kutiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya shilingi laki tano ambapo alilipa faini huku fedha alizotoa kama hongo kutafishwa na kuwa mali ya Serikali.

Hivyo Mkuu huyo alitoa onyo kwa wananchi kutojaribu kushawishi au kutoa hongo kwa watumishi wa TAKUKURU mahali popote kwa lengo la kuharibu uchunguzi au ushahidi wa tuhuma zozote zinazochunguzwa na sababu hatua kali za kisheria zitachukuliwa kama ilivyokuwa kwa mtuhumiwa huyo.

Hata hivyo alisema mtuhumiwa huyo amefunguliwa jarada lingine mahakamani la kesi ya ubadhilifu wa Milioni 90 zilizoidhinishwa na kungizwa kwenye akaunti yake kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya walimu na chumba cha darasa ambao ulitakiwa kuwa umeshakamilika huku ukiwa bado haujakamilika.
Kha sijaelewa hii hesabu.

Alitaka kutoa rushwa ya mil 3

Mahakama imempiga fine ya laki tano

Hiyo mil 2.5 imeenda wapi!?
 
Tungaraza alisema mshtakiwa huyo ambaye pia ni Mlezi wa kikundi cha Bosi Kuku Group alikiri kosa na kutiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya shilingi laki tano ambapo alilipa faini huku fedha alizotoa kama hongo kutafishwa na kuwa mali ya Serikali.
Tuwekewe hapa risiti ya malipo hayo
 
Back
Top Bottom