Albedo, kitendo cha kukubali Dr naye ni binadamu, kimetosha kunifanya nikubaliane na wewe.
Nape namfahamu fika, ni kijana makini na ana very bright future kwa siasa za bongo, mimi nilimweka kwenda kundi la Magogoni type 2025.
Kitendo cha kumshambulia Dr wa ukweli, kutazidi kuicost CCM kuchukiwa zaidi badala ya kuinyanyua. Anachotakiwa kufanya Nape, awe na washauri tena wengine wawe wa nje ya chama chake ili wampe trends zimekaaje ili azizidi kuharibu.
CCM BADO ina watu makini ambao kamwe hutakaa usikie wakimbeza Dr wa ukweli. Watu kama Prof. Mark Mwandosya, Samweli Sitta au Dr. Harison Mwakiembe huwezi wasikia wakiibeza Chadema au kumbeza Dr wa ukweli. Naamini Nape sio msema ovyo, sio Tambwe Hiza type, he is better than that, kosa lake ni moja tuu, kumwendekeza ******. NAadhani ****** kamtuma tukibezwa na nyinyi jibuni. Ni katika kumu impress ******, matokeo yake anataka kugeuka mropokaji Makamba na Tambwe Hiza ni afadhali.
Naomba tufike mahali tuaje kuwajadili watu wa aina hii, huku ni kuwapandisha chati zaidi kwa kuwapa faraja kuwa kumbe sindano wanazoidunga Chadema, zimewaingia sawasawa ndio maana jf (ya chadema!), wanamshukia kwa hasira!.