Nape na madai ya uchagga ndani ya CHADEMA

Nape na madai ya uchagga ndani ya CHADEMA

Mzushi ni wewe Albedo kushadadia vitu visivyo na mashiko,inahitajika usome kwa kiwango kipi ujue kuwa Nape kajimaliza mwenyewe kukubali tena kwa njaa yake awe frontline apambane na risasi za cdm?ngoja kwanza ishu ya siku 90 za mafisadi wao zifike tuone atatokea wapi yeye si ndio msemaji wa chama cha magamba atatuambia.
Watu wengine mnaandika tu chochote kinachowajia kichwani mara mzushi ni Albedo within a second ukasema tena Nape kajimaliza then which is which, hapa inaonesha kwamba ukweli unaujua kuwa mwenye tazizo ni Nape lakini unalazimisha kuingiza neno uzushi kwa asiyehusika lakini wenye akili wamekuelewa.
 
Mkuu Nape amesema Hawezi Kujiunga CHADEMA kwa Sababu ni Chama cha Wachaga, Tafsiri yake ni Kwamba Kama CHADEMA kingekuwa ni Chama cha Wahehe Angejiunga

Sasa sijui unataka Tafsiri Gani

Ungeenda mbele zaidi ungeona kuwa alisema pia kuwa sio chama cha wachaga bali ni chama cha koo fulani, usingekuwa mkabila moyoni mwako usingeishia kwenye ukabila ungeenda mbele kidogo na kuona kumbe labda tatizo lake sio wachaga bali labda ni hizo koo, lakini ungeenda kwenye fikra pevu zaidi usingeiona kauli yake ile sio chuki yake kwa hizo koo bali ni lugha ya picha inayomaanisha kuwa kuna kikundi kidogo sana cha watu kinachohodhi chama, umeshindwa vipi kufikia hapo?

Kwanini uje kwenye tafsiri ya Nape ana Chuki na Wachaga?this is too low ndugu yangu, badilika!!
 
- Msemaji wa chama ni Katibu mwenezi, labda ungeorodhesha waliowahi kushika hiyo nafasi in the past na ndio hasa hoja ya Nape na ni valid, kwamba makatibu wenezi wa CCM waliopita wameiangusha sana CCM! I mean tungejuaje Mwenyekiti kukiuzia chama chake malori mabovu kwa hela zote hizo za ajabu sana kwa watetezi wa wanyonge?

FMEs!

Mkuu I can not thank you enough for this useful intervention. Tunazungumzia nafasi yake kama mwenezi halafu jamaa anafanya sampling ya viongozi wa nafasi tofauti ili kuleta uchochezi ili hao aliowataja wajione wamekashfiwa. Toa orodha ya Waenezi halafu tufanye ulinganisho ili tufikie hitimisho kuhusu kauli ya Nape na siyo kujichukulia tu watu ili kuptosha uzito wa mada ya Nape.

Hili la malori chakavu kwa kweli ni doa and we must face it!
 
Nataka muelewe kuwa haya maneno siyo ya Nape. Ukisikia mtoto anasema kitu nyeticha familia elewa kuwa mazungumzo hayo yalikuwa ya baba na mama. Sishangai hata kidogo. Nape amekuwa vuvuzela tu la kupigia mbiu na wala siyo yeye kamwe. CCM wanalijua hili fika! Na hata vyeo na madaraka wanavyopewa watu wa kabila hilo ni kuwahonga tu ili ionekane kuwa wako pamoja. Kiukweli wachaga wanaonekana tishio hata ndani ya CCM na wanawaogopa. Uoga huu sijui unatokana na nini ila historia inaweza kuwa imejirudia!
Mwalimu alilijua na aliwaheshimu wachaga kwa harakati! Wakati huo Nyerere aliwahi kukutana na Mangi Marealle UN akidai Uhuru wa wachaga! Nyerere alichukulia hili kama watu hatari sana! Sitoshangaa mbegu hii ikiendelea kuwepo CCM! Mwalimu ilibidi awe rafiki na Mangi Marealle! Nani asiyejua kuwa hata typewriter ya kwanza na secretary wa kwanza wa mwalimu alipewa na Mangi Marealle.
So taratibu wanaanza kuibua vile vi-genetic vilivyojengeka tangu zamani.
Nape ni muathirika wa wachaga na sipoangalia watammaliza maana vita aloanzisha hataimaliza dawa tu ni kuomba radhi kwa wachaga!

Nape kawashika pabaya CHADEMA niliwahi kutoa angalizo juu ya harufu ya Uchaga ndani ya CDM nikapuuzwa sasa hangaikeni nalo hilo ambalo ni Ukweli kabisa CDM bado inasumbuliwa na Uchaga!
 
Unachokionesha ni upindishaji wa mada kwa lengo la kueneza chuki za kikabila na kufitinisha watu, ni udhaifu mkubwa sana kwa mtu makini wa dunia ya leo.
Yupi kati ya Nape na Albedo anayeeneza chuki za kikabila and how be realistic please, inavyoonekana mnamjua anayeeneza ukabila kwa kiwango cha juu hadi katangazwa kwenye media lakini kwa sababu zenu mnajifanya hamuelewi.
 
Nitapindishaje Mada niliyoileta Mwenyewe?

Haujaileta mada yako bali umeleta jukwaani mada ya Nape kwa tafsiri potofu inayofitinisha jamii, hili ndilo tatizo langu hapa.
 
Ungeenda mbele zaidi ungeona kuwa alisema pia kuwa sio chama cha wachaga bali ni chama cha koo fulani, usingekuwa mkabila moyoni mwako usingeishia kwenye ukabila ungeenda mbele kidogo na kuona kumbe labda tatizo lake sio wachaga bali labda ni hizo koo, lakini ungeenda kwenye fikra pevu zaidi usingeiona kauli yake kama ni chuki yake kwa hizo koo bali ungeona kumbe ndani ya yale maneno anachomaanisha ni kuwa kuna kikundi kidogo sana cha watu kimekiodhi chama, umeshindwa vipi kufikia hapo?

Kwanini uje kwenye tafsiri ya Nape ana Chuki na Wachaga?this is too low ndugu yangu, badilika!!

Mkuu Nimeweka Full Statement inawezekana wewe Umeliona hilo la Ukoo! After all Chama ni lazima Kianzishwe na Mtuu. Utakuwa ni ufinnyu ( Au Kufikiri kwa Kiwango cha Nape) wa Kufikiri ikiwa Nitakuja Leo na Kusema kwamba Siwezi Kujiunga CCM kwa Sababu ni Chama cha Wazanaki na ni cha Ukoo wa Nyerere
 
Acheni upuuzi!
Chadema yenyewe si imeanza kujulikana kwenye uchaguzi uliopita baada ya kupata kampani ya KANISA!
Sasa huo mlolongo wote wa kazi gani?

Nyie watu wa Chadema mnatuletea zilezile za "zidumu fikra sahihi za mwenyekiti" kwa ajinsi mnavyom-venerate Bishop Slaa!
Ndio maana akipora mke wa mtu nyie mnashangilia tuu! Huo ni uzuzu mkubwa!



Hawezi kujenga taasisi ya taifa kama hana taasisi imara ya familia! Slaa ni muasi muovu!

Unajua ukiwa fanatic huwa unakosa objectivity. Jamaa ni fanatics na wanadhani huyu Slaa na kikundi chake ni malaika na kwa hiyo chochocte anachokifanya basi kiko sahihi kama gospel truth na yeyote anayewasaidia kukiangalia hicho kitu ukaribu na kuwaeleza dosari basi watamjia juu na kumuita majina kama vilification aliyofanyiwa Malaria Sugu. Najiuliza kama Presidential Aspirant wa CCM angefanya hivyo kina Marando wasingeigeuza kuwa campaign slogan! Mavi ni mavi hata yakiwa ya mzungu!
 
wakibosho, wamarangu na wamachame bado mko CCM..nilitegemea muwe mesharudisha kadi au muchome moto hizo kadi na takataka zote zenye harufu ya ccm maana msitegemee kuombwa msamaha na ****** au msemaji wake nape..maana alianza kwa kuwatuka watu wa kazikazini mkaa kimya akaona nyie mazoba akaona sasa amerudia tena au hammuelewi? Anasema nyie watu kazikazini hamfai kuongoza nchi hii..
 
asanteni kwa maelezo mazuri ilanatatizo moja kwanini zitto alipotaka kugombea ukatibu mkuu ilitokea zengwe ndani chama? na pia kanini hayati CHacha Wangwe kabla hajafa aliongelea uchaga na ubaguzi ndani ya Chadema? lisemwalo lipo na kama halipo linakuja, mi sina chama ila naangalia ukweli na kuwasoma vizuri ili tujue nani ni mkweli na anania thabiti ya kumkomboa mtanzania masikini, sio unafiki wenu nyinyi wanasiasa.
 
Mkuu Nimeweka Full Statement inawezekana wewe Umeliona hilo la Ukoo! After all Chama ni lazima Kianzishwe na Mtuu. Utakuwa ni ufinnyu ( Au Kufikiri kwa Kiwango cha Nape) wa Kufikiri ikiwa Nitakuja Leo na Kusema kwamba Siwezi Kujiunga CCM kwa Sababu ni Chama cha Wazanaki na ni cha Ukoo wa Nyerere

Nani kaliona la ukoo?rudia tena kusoma....Nasema alichomaanisha ni kuwa chama kimeodhiwa na watu wachache na wanakiendesha kama mali yao binafsi, umeshindwa vipi kumtafsiri hivyo na kurukia kwenye ukabila?
 
Nani kaliona la ukoo, rudia tena kusoma....Alichomaanisha ni kuwa chama kimeodhiwa na watu wachache na wanakiendesha kama mali yao binafsi, umeshindwa vipi kumtafsiri hivyo na kurukia kuwa ukabila?

Mkuu Hiyo ni Tafsiri yako ambayo siyo Lazima ifanane na Tafsiri yangu, na wala huwezi kunilazimisha Nitafsiri kama Ulivyotafsiri wewe.
 
Narudia tena.....Mtu anapaswa kwanza awe mkabila ndipo anapoweza kuifasiri kauli hiyo ya Nape kama ni chuki kwa Wachaga, ndicho alichofanya Albedo na Watu wengi hapa jana na kinasikitisha sana.

Ukiangalia kwa umakini utaona kuwa Nape hana ata wazo la kikabila katika kauli ile lakini Watafsiri hawa walio na utando wa fikra za kikabila karibu sana na mioyo yao ndicho wanachokiona kwa sababu ndicho kilichoijaza mioyo yao.
Duh!!! jamani nani kairoga tanzania na watanzania tuna macho lakini tunajifanya hatuoni tuna masikio lakini tunajifanya hatusikii LOL!!!!! Ohh...God help us...........
 
Duh!!! jamani nani kairoga tanzania na watanzania tuna macho lakini tunajifanya hatuoni tuna masikio lakini tunajifanya hatusikii LOL!!!!! Ohh...God help us...........

Tatizo ni Kwamba Butola anataka watu Tutafsiri kauli za Viongozi kama yeye Anavyotafsiri. Nape amezungumza, hakutafsiri so Ni Haki ya Raia yeyote Kutafsiri anavyoweza na Litakuwa Kosa kwa Raia Mmoja kulazimisha Tafsiri yake
 
Mkuu Hiyo ni Tafsiri yako ambayo siyo Lazima ifanane na Tafsiri yangu, na wala huwezi kunilazimisha Nitafsiri kama Ulivyotafsiri wewe.

Its true...

......Ni lazima kwanza mtu awe mkabila ndipo atakapoweza kuitafsiri kauli ya mtu atakayesema CCM ni chama cha Wakwere kuwa ana
chuki na Wakwere.
......Ni lazima kwanza mtu awe mdini ndipo atakapoweza kuitafsiri kauli ya mtu atakayesema CUF ni chama cha Waislamu kuwa ana chuki na
Waislamu.
......Ni lazima mtu awe mdini ndipo atakapoweza kuitafsiri kauli ya mtu atakayesema Chadema ni chama cha Wakristo kuwa ana Chuki na Wakristo..
 
- Ha! ha! ha! yaani nikisema Mwenyekiti ameuzia mbuzi kwenye gunia chama chake, basi ninatakawiwa kunyamaza! sawa bwana ila ninavunjika mbavu zangu, jinsi Mwenyekiti na katibu wake walivyo wajanja saana kama sungura!

haya bwana nimenyamaza sasa! sirudii tena kusema Mwenyekiti na gunia la mbuzi! ha! ha! ha!

FMEs!

Kumbe ufisadi uliopo ndani ya CCM tuhuma zake zinajibiwa kwa kuanika posho za za mtu mmoja au wawili tu pale CDM??.. okay,bila kujali unamaendeleo ya kusoma na kukalili vitabu vingapi na miaka mingapi ya kuona jua,achilia mbali HEKIMA ambayo ni level nyingine ya understanding (ambayo siwezi kukuhukumu kwayo), KWAMBA UFISADI ULIOSABABISHWA NA VIONGOZI WA CCM,NA ATHARI ZAKE KWA TAIFA,BADO UNAMACHO YA KULINGANISHA NA KUTETEA DHIDI YA MSHAHARA WA DR.SLAA?..
 
Chonde chonde, Nape anachafua mambo. Majigambo ya nini? sisi tunataka kuona vitendo na ahadi lukuki za ccm zikitekelezwa na maisha ya wanainchi yanakuwa bora. Hatuwezi kukupima kwa kubwata hovyo hovyo tu. Kwanza kauli zako za ukabila zinakigawa chama badala ya kukiimarisha. Nakushauri utulie na kutumia akili badala ya kusema kila linalofika mdomoni mwako. Enzi za propaganda tupu na kurithishana madaraka zimekwisha, usidhani kuwa kama baba yako aliweza na wewe utaweza, we want results and not empty words
 
Nani kaliona la ukoo?rudia tena kusoma....Nasema alichomaanisha ni kuwa chama kimeodhiwa na watu wachache na wanakiendesha kama mali yao binafsi, umeshindwa vipi kumtafsiri hivyo na kurukia kwenye ukabila?
'Nasema alichomaanisha' how sure are you! by what percentage!, please don't force a square peg in a round hole.
 
...shida ya watanzania si ukabila ..BALI NI WIVU Tu......mara nyingine utafikiri kuwa wachagga wanabaguliwa lakini kumbe ni wivu tu wanawaonea.....na huo wivu si kwa mchaga tu....mtu yeyote akiwa na maendeleo kidogo basi wanamuonea wivu.....

...hali hii inayoendelea ..inawafanya wachagga hata wale walio ndani ya ccm waonekane wako pale kujipendekeza...wivu huu umepanuliwa hadi kwa makabila yenye ukaribu na wachagga ..yaani Makabila ya Kasikazini...hata imefikia watu wanakaa kikao na mtoto wa rais akiwamo wanasema kuwa mwaka 2015 hatutaki rais toka kaskazini...this is too much!
 
Back
Top Bottom