Nape na madai ya uchagga ndani ya CHADEMA

Nape na madai ya uchagga ndani ya CHADEMA

Kwani huyu Nape ametokea wapi hasa? Mbona anaonekana kuwa controversial sana?
 
Ndicho nilichokiona kwako.

Mkuu Hata Chiligati hakuwa kutoa Kauli Kama hii

"Tena uandike kabisa, mimi ndiyo ninao ushahidi wa wao kunitaka nikagombee kupitia chama chao nikakataa, kwa sababu siwezi kuhamia kwenye chama cha Wachagga, kile ni chama cha ukoo," alisema Nape.
 
Nilichokipata kwenye thread yako ya jana ni fikra za ukabila zilizopo karibu sana na moyo wako, kwani ni shurti mtu binafsi awe mkabila ndipo atapoweza kuitafsiri kauli ya mtu mwingine katika misingi ya kikabila, hili sikulitegemea kutoka kwako ndugu yangu.

Ni hii ya leo ni hoja nyingine dhaifu kutoka kwako, ulipaswa uelewe kwanza ni lini Chadema imeanza kuwa tishio kisiasa kwa CCM, actually ni kuanzia hoja ya Buzwagi Bungeni mwaka 2007, sasa kwa wewe kutuletea viongozi wa CCM wa miaka ya 1990 ili kukusaidia kujenga hoja ya Nape ni udhaifu mkubwa sana.
Butola

Utakuwa unamuonea bure mleta hoja Albedo, 'usilaumu risasi ilipoangukia laumu aliyefyatua' sijakusikia hata mara moja ukimlaumu Nape aliyeanzisha suala hili la ukabila sijui ni by defaults au kitu gani, tunachojadili hapa ni yaliyoanzishwa na Nape na ili kujadiliwa lazima mtu kama mimi wewe au Albedo aanzishe topic, katika kujadili maneno yako yataonesha aidha uko kulaani kitendo cha Nape au uko upande wa Nape kupongeza kitendo alichokifanya kueneza mbegu ya ukabila.
 
Mzushi ni wewe Albedo kushadadia vitu visivyo na mashiko,inahitajika usome kwa kiwango kipi ujue kuwa Nape kajimaliza mwenyewe kukubali tena kwa njaa yake awe frontline apambane na risasi za cdm?ngoja kwanza ishu ya siku 90 za mafisadi wao zifike tuone atatokea wapi yeye si ndio msemaji wa chama cha magamba atatuambia.
 
Mkuu Hata Chiligati hakuwa kutoa Kauli Kama hii

Usingekuwa na fikra za kikabila usingeona lugha hiyo kihivyo, inasikitisha sana!!

......Ni lazima kwanza mtu awe mkabila ndipo atakapoweza kuitafsiri kauli ya mtu atakayesema CCM ni chama cha Wakwere kuwa ana
chuki na Wakwere.
......Ni lazima kwanza mtu awe mdini ndipo atakapoweza kuitafsiri kauli ya mtu atakayesema CUF ni chama cha Waislamu kuwa ana chuki na
Waislamu.
......Ni lazima mtu awe mdini ndipo atakapoweza kuitafsiri kauli ya mtu atakayesema Chadema ni chama cha Wakristo kuwa ana Chuki na Wakristo..
 
Butola

Utakuwa unamuonea bure mleta hoja Albedo, 'usilaumu risasi ilipoangukia laumu aliyefyatua' sijakusikia hata mara moja ukimlaumu Nape aliyeanzisha suala hili la ukabila sijui ni by defaults au kitu gani, tunachojadili hapa ni yaliyoanzishwa na Nape na ili kujadiliwa lazima mtu kama mimi wewe au Albedo aanzishe topic, katika kujadili maneno yako yataonesha aidha uko kulaani kitendo cha Nape au uko upande wa Nape kupongeza kitendo alichokifanya kueneza mbegu ya ukabila.

Asante Quinine

Mimi niko upande wa KULAANI

Sasa Sijui yeye Butola yuko Upande gani
 
Si dhani kama alichokianzisha Nape unakielewa. Subiria mziki wake ndio utajua. Nahisi anampango wa kutokugusa kilimanjaro. Kumbuka Nape kuwakataa Wachaga na kawatukana Mapadre eti hawana maadili. Ukiangalia mlolongo huu utaona ni mwendelezo wa CCM wa kubagua watu wake na kuwatusi.

Swali je CCM inawachama wachaga? kama wapo na uongozi wa juu unausema hauwezi kukaa nao wala kufanya nao kazi unawaambia nini hawa wananchama? Na kesho ni nani au ukanda gani utatengwa, kumbuka umoja wa vijana wa CCM pwani nao walitenga baadhi ya kanda na mikoa kwenye uraisi 2015. je Nape kafanya ajali au ni maelekezo ya boss wake?

Si kweli kwamba Nape ndo kalianzisha hili, nafikiri huu ni upotoshaji wa wazi. aliyelitaja hili hadharani ktk vyombo vya habari ni aliyekuwa wakati huo Makamu mwenyekiti wa CHADEMA.
 
The Fact ni Kwamba

1. Huwezi Kumsema Dr. Slaa Huku Mitaani kwetu halafu Ukabaki Salama.

2. Kwa Watanzania Walio wengi Dr. Slaa is Their Hero, Huwezi Kumsema Vibaya na Ukabaki Salama

3. CCM haipendwi na Brand ya Ufisadi ndio imeua CCM, Kwa nape Kumshambulia Dr. Slaa ( Mtu wa Kwanza Kutoka hadharani na Kuorodhesha Mafisadi na Ufisadi wao) Its a Wrong and Failed Stratergy to Start With
Albedo,
Kwa hiyo Dr ni malaika fulani?, hata akikosea, au kuambiwa ukweli bado huwezi kubaki salama?. Hakuna ubishi kuhusu nguvu yake, kukubalika kwake na ushujaa wake kwenye ile list of shame, ila inapotokea anataka kutupeleka kusiko asiambiwe?.

Mimi ni miongoni mwa wachache ambao tutasema ukweli daima, ili ikifika 2015, tusipofika pale tunapotaka kufika, angalau tuseme, tuliliona na tulisema na hatukusikilizwa!
 
Safari ya kisiasa ya Nape ni fupi kuliko chupi yangu, atashindwa kabla hajaanza........................
 
Mzushi ni wewe Albedo kushadadia vitu visivyo na mashiko,inahitajika usome kwa kiwango kipi ujue kuwa Nape kajimaliza mwenyewe kukubali tena kwa njaa yake awe frontline apambane na risasi za cdm?ngoja kwanza ishu ya siku 90 za mafisadi wao zifike tuone atatokea wapi yeye si ndio msemaji wa chama cha magamba atatuambia.

Taratibu Usije Ukajikwaa. Kwanza Salaam Baada ya Salaam sasa Eleza Hoja yako na Kama Una Mkojo Umekubana nenda kwanza kautoe ili Uje Unyooshe Paragraphy yako
 
Hivi Nape hapigi Msuba kweli huyu chalii? Kaaaaazi kweli kweli!
Huyu havuti msuba wala ganja coz msuba unarise sana concious and self awareness mla ganja hakurupuki bali anaskilizia Nape itakuwa anavuta makushabu au mapuya which is uchafu au mabaki yanayotokana na msuba kuwa umechambuliwa tena nahisi atakuwa anavutia chooni thats why
 
Hivi milioni 7.1 za Slaa (PhD) na milioni 11 za Mukama zipi ni nyingi? WanaCDM wamelalamikia hayo malori ya matangazo? Hizo sio gari chakavu ni gari amabzo CCM wanatamani walipate japo moja maana ni zaidi ya ile SCANIA ya TOT. Mlitaka Katibu Mkuu wetu (ambaye wengi wetu tunamheshimu kama Rais wetu) alipwe shilingi ngapi? Hata tukiamua kumlipa milioni 14, kinakuwasha nini? kama unakereka, mbona hukujinyonga pale choo cha matundu saba kilipojengwa kwa milioni 700 na mkwele akashangilia? au UKARABATI wa nyumba 2 ulipogharimu shilingi bilioni 5.2?
 
Albedo,
Kwa hiyo Dr ni malaika fulani?, hata akikosea, au kuambiwa ukweli bado huwezi kubaki salama?. Hakuna ubishi kuhusu nguvu yake, kukubalika kwake na ushujaa wake kwenye ile list of shame, ila inapotokea anataka kutupeleka kusiko asiambiwe?.

Mimi ni miongoni mwa wachache ambao tutasema ukweli daima, ili ikifika 2015, tusipofika pale tunapotaka kufika, angalau tuseme, tuliliona na tulisema na hatukusikilizwa!

Mkuu Pasco Dr. Slaa ni Binadamu na anakoseaga sana. Dr. Slaa ana nguvu ya Ajabu nimeshawahi Kuhudhuria Mkutano wake Ulifanyika Makuburi Niliona kwa Macho yangu Watu wakitoka Machozi Bila ya wao Kujijua. Wale watu leo hii ukiwaambia Wachange Mshahara wa Dr. Slaa kwa Mwezi wanaweza kuchanga zaidi ya Milioni 10.

To deal with Dr. Slaa ni Lazima uwe Makini sana la Sivyo unaweza Kupopolewa Mawe na ndiko anakoelekea Nape. Ni Maoni yangu tu yaweza kuwa SI SAHIHI

Ndio Maana nikasema kwamba Mguu alioanza nao Nape Amekosea sana
 
Butola

Utakuwa unamuonea bure mleta hoja Albedo, 'usilaumu risasi ilipoangukia laumu aliyefyatua' sijakusikia hata mara moja ukimlaumu Nape aliyeanzisha suala hili la ukabila sijui ni by defaults au kitu gani, tunachojadili hapa ni yaliyoanzishwa na Nape na ili kujadiliwa lazima mtu kama mimi wewe au Albedo aanzishe topic, katika kujadili maneno yako yataonesha aidha uko kulaani kitendo cha Nape au uko upande wa Nape kupongeza kitendo alichokifanya kueneza mbegu ya ukabila.

Narudia tena.....Mtu anapaswa kwanza awe mkabila ndipo anapoweza kuifasiri kauli hiyo ya Nape kama ni chuki kwa Wachaga, ndicho alichofanya Albedo na Watu wengi hapa jana na kinasikitisha sana.

Ukiangalia kwa umakini utaona kuwa Nape hana ata wazo la kikabila katika kauli ile lakini Watafsiri hawa walio na utando wa fikra za kikabila karibu sana na mioyo yao ndicho wanachokiona kwa sababu ndicho kilichoijaza mioyo yao.
 
Mkuu Nape amesema Hawezi Kujiunga CHADEMA kwa Sababu ni Chama cha Wachaga, Tafsiri yake ni Kwamba Kama CHADEMA kingekuwa ni Chama cha Wahehe Angejiunga

Sasa sijui unataka Tafsiri Gani
 
Acheni upuuzi!
Chadema yenyewe si imeanza kujulikana kwenye uchaguzi uliopita baada ya kupata kampani ya KANISA!
Sasa huo mlolongo wote wa kazi gani?

Nyie watu wa Chadema mnatuletea zilezile za "zidumu fikra sahihi za mwenyekiti" kwa ajinsi mnavyom-venerate Bishop Slaa!
Ndio maana akipora mke wa mtu nyie mnashangilia tuu! Huo ni uzuzu mkubwa!

Hawezi kujenga taasisi ya taifa kama hana taasisi imara ya familia! Slaa ni muasi muovu!
 
Asante Quinine

Mimi niko upande wa KULAANI

Sasa Sijui yeye Butola yuko Upande gani

Unachokionesha ni upindishaji wa mada kwa lengo la kueneza chuki za kikabila na kufitinisha watu, ni udhaifu mkubwa sana kwa mtu makini wa dunia ya leo.
 
Unachokionesha ni upindishaji wa mada kwa lengo la kueneza chuki za kikabila, ni udhaifu mkubwa sana kwenye dunia ya leo.

Nitapindishaje Mada niliyoileta Mwenyewe?
 
Eeka Mangi, aika mae/mbe, naomba usiturudishe nyuma kwenye historia ya kupigania uhuru na mchango wa Mangi Mkuu, Thomas Marealle, sio tuu aliomba uhuru wa Wachagga peke yake, bali pia alimhujumu Mwalimu Tanganyika isipate uhuru!. Mangi Mkuu alikuwa kibaraka wa Wakoloni Waingereza. Waingereza walitumia ule utawala wa indirect rule kwa kuwakweza machifu kwa kila aina ya favours ikiwemo kupewa makazi London, yeye na familia yake kuwa favoured at the expense ya the masses.

Siungi mkono ubaguzi wa aina yoyote hata huu wa kikabila, lakini pia nalaani baadhi ya makabila kujiona bora zaidi kuliko mengine. Mkoa wa Kilimanjaro ni miongoni mwa favourate regions kwa mkoloni kutokana na zao la biashara la kahawa. Kutokana na jina lako, utakuwa unaifahamu vizuri Kilimanjaro, hebu pandisha njia ya Machame au Marangu kupitia Marangu Mtoni, hapo unaambiwa ni kijijini mgombani, ni mambo ya lami mpaka milangoni, mahekalu ya ghorofa yaliyoshehenezwa ma satelite dishes mpaka na AC.

Pata nafasi ukavitembelee vijijini vya Singida, Dodoma au Tandahimba, ile lami ya Kibongoto ni afadhali mara mia. Unaamini kuna mikoa kama Mtwara na Lindi ilikuwa ni vumbi mpaka mjini, Mkapa ndio amepeleka lami juzi juzi tuu!. Sikumbuki tena nyumba za nyasi Moshi, mpaka banda la ng'mbe ni bati, huku wenzao Dodoma, hata nyasi ya kuezekea ni issue wanaezekea matope (tembe) halafu tunazungumzia usawa.

Nimesema kweli Tanzania hatuna ukabila wa kuzungumza, bali kuna ukabila mbaya zaidi ndani ya mioyo ya watu wa makabila yenye ukabila!.

Mkuu,
Na wewe umeanza taratibu kubusu mkia wa nge
 
Back
Top Bottom