Nape, Mawaziri kufunika Kigoma

Nape, Mawaziri kufunika Kigoma

hata mimi nimeshangazwa na huu mwamko wa watu wa Kigoma, kweli CHADEMA sasa mmefulia

U wapi mtawala wa hapo, je ni CHADEMA au nyinyiemu?Kama mtawala wa mkoa wa Kigoma ni CHADEMA basi huo utakuwa mkoa wa Tanganyika.
 
mimi sio mwongo, kama huamini baaasi, lakini kiukweli leo CCM wametisha
Acha ushabiki watshe wasitishe mwisho wa siku wanaendelea kuwafisidi watanzania hawafai tena kuaminiwa na watanzania
 
mkuu, hapa kuna wale wa sizitaki mbichi hizi, hivi unafikiri wakipata chance kama hizi wataziacha, mbuzi hula kulingana na urefu wa kamba yake

Hongera umempata shogawe wa kukupa kuwa nae pamoja.Ila mwambie akagombe uongozi uwt huyo cha mpenda vyeo.
 
Mi nashindwa kukuelewa huu sio wakati wa chama tawala kuzunguka kwa wananchi kinacho takiwa ni kutekeleza zile ahadi walizohaidi wakati wa kampeni na sio kuzunguka na kutoa ahadi zingine kama ilivyokuwa JANGWANI, hapa NAPE amekosa mbinu kabisa ya kukiimarisha chama? kwani hiyo siyo mbinu sahihi ya kupiga porojo tu ambazo hazina tija kwa wananchi, tekelezeni ahadi mtaona kama wapinzani watapata cha kuongea. Hapo mnaendelea kupoteza fedha zetu bure kwa mikutano isiyokuwa na tija.
 
Acha ushabiki watshe wasitishe mwisho wa siku wanaendelea kuwafisidi watanzania hawafai tena kuaminiwa na watanzania

Acha nae huyo mchumia tumbo,chama tawala kina mtisha nani? Hiyo yote kwa sababu hajitambui.
 
Ukweli husemwa:

Sunday, July 22, 2012


*NAPE ATUA KIGOMA, KUUNGURUMA UWANJA WA COMMUNITY CETRE MWANGA MCHANA HUU




Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kipampa mkoani Kigoma leo kwa ajili ya mkutano wa hadhara utakaofanyika kwenye Uwanja wa Comunity Centre, Mwanga mkoani humo. Kushoto ni Mbunge wa Kigoma mjini, Peter Serukamba.Picha zote na Bashir Nkoromo

Nape akiwasilimia viongozi wa CCM waliompokea Uwanja wa Ndege wa Kipampa, Kigoma leo.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akishiriki na vijana kucheza ngoma ya Kasimbo ya mkoa wa Kigoma, baada ya kuwasili Uwanja wa Kipampa mkoani humo, leo.

Waendesha pikipiki wakiongoza msafara wa Nape kutoka uwanja wa Ndege wa Kipampa mkoani Kigoma leo.
Picha kwa hisani ya: MUHIDIN SUFIAN


Yetu macho na masikio


 
Kwa propaganda watu hamjambo,kweli love is blind,mleta mada kapenda dhaifu,kapost kidhaifu,naye dhaifu kama dhaifu.
 
Kwa propaganda watu hamjambo,kweli love is blind,mleta mada kapenda dhaifu,kapost kidhaifu,naye dhaifu kama dhaifu.


huwezi kuniita dhaifu kama udhaifu wako hujaonekana ni udhaifu kwako
 
ccm kukubalika kigoma labda ipite miaka mia nane.
Ccm mnatabia ya kujitekenya wenyewe na kucheka wenyewe.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Sasa mkutano ndio unaisha, watu wengi wamerudisha kadi za CHADEMA na kuchukua za CCM
 
Inatia moyo sana!...

Leo mji wa Kigoma umepambwa na shamrashamra za mkutano wa CCM, maeneo yote ya mji kuna makundi makubwa ya watu wanaoelekea viwanja vya Mwanga Community Center, barabara zote zimefungwa kutokana na makundi makubwa ya watu kutoka maeneo ya Mlole, Mwandiga, Mji Mwema, Ujiji n.k

Kuna taarifa kwamba baadhi ya madiwani wa CHADEMA na aliyekuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya chama hicho mwaka 2010 leo wanarudisha kadi za chama hicho dhaifu na kujiunga na chama dume CCM

Kwa mwendo huu inabidi CHADEMA mjipange sana mwaka huu, wananchi wameshawachoka, na propaganda zenu za kujisingizia kuuwawa

More updates & pics. to come, niko kwa MAMA NTILIE hapa Kwa Bella namalizia kula

Kweli ccm kwishney, yaani mnaCOPY hata neno DHAIFU, daah! Walahi mmezeeka hamna jipya! Kama ni kuku kazeeka hatagi tena ni wa kuchinja!
 
kweli ccm kwishney, yaani mnacopy hata neno dhaifu, daah! Walahi mmezeeka hamna jipya! Kama ni kuku kazeeka hatagi tena ni wa kuchinja!


hadi sasa ninapoandika hapa bado ccm ndio chama tawala hapa tanzania
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom