Nape, Mawaziri kufunika Kigoma

Nape, Mawaziri kufunika Kigoma

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,055
​​NAPE, MAWAZIRI KUFUNIKA KESHO KIGOMA.

Nape-leo-2.jpg


NA BASHIR NKOROMO, KIGOMAChama Cha Mapinduzi (CCM) kesho, Jumapili, Julai 22, kinatarajiwa kuutikisa mkoa wa Kigoma, kwa mkutano wake mkubwa wa hadhara, utakaofanyika kwenye Viwanja vya Communicy Centre mjini Mwanga mkoani hapa. Mkutano huo mkubwa umepangwa kuhutubiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye, na baadhi ya mawaziri walioalikwa kueleza utekelezaji wa ilani ya CCM katika sekta wanazohusika nazo.

Mkutano huo, umepangwa kuanza mapema kwa kuwa unatakiwa kumalizika saa kumi jioni ili kuwapa fursa wananchi waliofunga kwenda kufuturu baada ya kushinda ana swaumu ya Mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Awali Mkutano huo ulikuwa ufanyike, Ijumaa iliyopita, lakini ukalazimika kusogezwa mbele baada ya taifa kuingia katika maombolezo ya siku tatu, kufuatia ajali ya meli iliyotokea Zanzibar ambapo watuzaidi ya 50 wamefariki dunia.

Katika mkutano huo wa kesho Jumapili, Nape na baadhi ya mawaziri na manaibu mawaziri walioalikwa akiwemo Steven Wasira na Aggrey Manri, wanatarajiwa kueleza utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani Kigoma na Tanzania kwa jumla. Pia wanatarajiwa kueleza sera za CCM, na kueleza wananchi wa Kigoma, nini CCM imefanya, inafanya sasa na inatarajiwa kufanya nini baadaye katika kukifanya chama hicho na serikali yake, kuendelea kuwa makini na imara katika kuliongoza taifa la Tanzania.

Kufuatia mkutano huo kuahihirishwa karibu kona zote za mji wa Kigoma na vitongoji vyake kama Ujiji, Kahabwa, Gungu na Mwandiga, wamekuwa wakijadili kuhusu mkutano huo, kwenye vijiwe vya kahawa, vituo vyua daladala na kwenye mikusanyiko hasa ya vijana, hamu kubwa ikiwa ni kutaka kumsikiliza Nape na wabunge watakaopanda jukwaani kwa mtindo wa aina yake.

Pia baadhi ya watu wameonyesha hamu ya kuhudhuria mkutano huo kutokana na staili ambayo inaelezwa kuwa ni mpya na nzuri ya CCM kuwapeleka kwenye mikutano ya hadhara baadhi ya mawaziri kueleza wanavyosimamia utekelezaji wa ilani ya Chama kwenye sekta zao.

"Kwanza mimi ningependa nimsikie Nape, nasikia ni msema kweli kama kuna jambo huwa hasiti kusema hata kujwaani, na pia nitapenda niwasikie mawaziri watakaowaleta kwa sababu kwa muda mrefu hatujawahi kumsikia hapa Kigoma waziri yeyote akisimama jukwaani kwenye mkutano wa hadhara kueleza utekelezaji wa ilani", alisema Joseph Chishako wa Mwandiga.

Yetu ni macho na masikio



UPDATE

HIZI NDIZO BAADHI YA PICHA ZA MKUTANO, JULY 22, 2012

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Naibu Waziri wa Uchukuzi, Charles Tzeba akihutubia kwenye mkutano wa CCM uliofanyika, jana , Julai 22, 2012, kwenye Uwanja wa Community Centre, Mwanga mjini Kigoma.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala wa Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI,) Aggrey Mwanri akihutubia, kwenye mkutano wa CCM uliofanyika, jana , Julai 22, 2012, kwenye Uwanja wa Community Centre, Mwanga mjini Kigoma.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akihutubia, kwenye mkutano wa CCM uliofanyika, jana , Julai 22, 2012, kwenye Uwanja wa Community Centre, Mwanga mjini Kigoma.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Waziri wa Nchi Ofsi ya Rais, Mahusiano, Steven Wasira akihutubia kwenye mkutano wa CCM uliofanyika, jana , Julai 22, 2012, kwenye Uwanja wa Community Centre, Mwanga mjini Kigoma.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Wazee wa mkoa wa KIgoma kwenye mkutano wa CCM, Uwanjwa wa Community Cetre Mwanga Kigoma[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Viongozi wa Chama na Serikali[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Mamia ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa CCM katika Uwanja wa Community Centre, Mwanga mkoani Kigoma
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
sijaona mtu anayeenda kigoma wote ni madudu tu ndani ya jamii ya tanzania zito kawatisha nape nenda kwanza kwenu lindi ukawatoe cuf
 
Hakunaga ccm inaendeshwa na cdm miaka yote mbona hawafanyi hivyo? Au kimewaka duu baba wa taifa anaondoka na chama chak
 
its another ccm silly meeting,

nimemshangaa sana mchumi wetu wa daraja la 1

eti ''sisi tununue mtambo kisha tutume meseji za kujitishia sisi wenyewe inakuja akilini hii kweli ''

swali kwa mchumi wetu: kazi ya huo mtambo nini na mauthui yake ni nini??

TBC: mbona habari ya Marando hamkusema ili mtu apate mtililiko wa mabishano
 
hii mikutano yao mara nyingi haitofautiani na ile ya kampeni " utawasikia wakitumia neno "tuta... badala ya tumefanya ..."
 
Nape na timu yako nawatakia heri katika ziara yenu..
 
Star TV walikuwa fair kuonyesha pande zote mbili... Nape vs Marando
 
Aibu waloipata Sumbawanga hawajakoma, wameamua kwenda kwenye mkoa uliochoshwa kabisa na nyinyiem kuliko mikoa yote Tanzania, mkipigwa mayai viza huko msisingizie chama dume Chadema.
 
Naona maana kama si mabaya, bendera utadhani utadhani shamba la mpunga. Tena zote mpya kila la kheri. Lakini CCM ijue kuwa wananchi kwa sasa hawahitaji tena maneno toka kwa CCM wanahitaji vitendo zaidi. Kama maneno waliisha yasikiliza tokea 1961.

1.+Bendera+za+CCM++zilizopambwa+kwenye+Uwanja+wa+Community+Cetre,+Mwanga,+mkoani+Kigoma.jpg
 
ati kufunika.......... wanafunika nini sasa??


upuuzi mtupu, wakae wajiulize kama wapo tayari kuwa wapinzani
 
njooni huku tuwakadhi hizi kadi za chadema muwapelekee huko moshi, tumekichoka chama hiki kwa ukabila na udini.
 
Nimesoma mahojiano ya Nape kwenye BANG! Magazine,

Nimeshangazwa na usemi wake wa kuviita vyama vya upinzani pressure groups!!

Hivyo muungano wenu na CUF ni CCM plus pressure group?

Kama mnapambana na pressure groups hakuna haja ya mikutano yenye kuita na mawaziri kusema mmetimiza ahadi, kwani kama mmetimiza ....chema chajiuzaaaaaaaaaa.....sasa mbona mwajitembeza na pressure groups?
 
imekuwa ndio mazungumzo katika kila kona na vijiwe, wengi wao wamesema tumechoka na hiki chama cha cdm kwa ubaguzi wanaoufanya kwa zitto kabwe kwa kuwa tu katangaza nia yake ya kugombea urais anakuwa anapigwa vita na watu wa kaskazini, wanasema kigoma ilikuwa ngome ya chadema lakini sasa tumechoka na chama, tunaamua kurudi CCM kwanza wametekeleza kwa 90% yale yote waliyoahidi kwa mkoa wetu, hatuoni sababu ya kuendelea tena kukikumbatia chama kina choendesha endesha siasa zake kwa kutumia udini na ukabila!!! tunarejea kwa mama. walisema wakazi hao wa ujiji.
 
imekuwa ndio mazungumzo katika kila kona na vijiwe, wengi wao wamesema tumechoka na hiki chama cha cdm kwa ubaguzi wanaoufanya kwa zitto kabwe kwa kuwa tu katangaza nia yake ya kugombea urais anakuwa anapigwa vita na watu wa kaskazini, wanasema kigoma ilikuwa ngome ya chadema lakini sasa tumechoka na chama, tunaamua kurudi CCM kwanza wametekeleza kwa 90% yale yote waliyoahidi kwa mkoa wetu, hatuoni sababu ya kuendelea tena kukikumbatia chama kina choendesha endesha siasa zake kwa kutumia udini na ukabila!!! tunarejea kwa mama. walisema wakazi hao wa ujiji.

SASA WEWE MKIGOMA NI KAFU, IMEKUAJE TENA LEO UMEHAMIA CCM??

kale kamsemo ka wanakafu kuliwa na ccm ni kweli?
 
UPEPO wa mabadiliko ya kisiasa uliozikumba nchi nyingi duniani, unaelekea kukiathiri Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho sasa kinahaha kujinusuru kung'oka madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Chama tawala hivi sasa kina msuguano mkubwa wa kiuongozi ambapo baadhi ya viongozi wake wamekuwa wakimshutumu Katibu Mkuu, Willison Mukama, kwa kukwamisha mikakati ya kujiimarisha na kurejesha matumiani yaliyofifia miongoni mwa wanachama wake.
Licha ya Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, wiki hii kukanusha kutokuwa na msuguano na Mukama, makada wa chama hicho wamelidokeza Tanzania Daima Jumapili, kuwa vita ya makundi ya kuwania uongozi na ile ya ufisadi inakitesa chama hicho.

CCM yapumulia mashine


[TD="bgcolor: #ffffff"]
CCM yapumulia mashine
• Ajali ya mv Skagit, urais 2015 vyaitesa

na Mwandishi wetu


[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"] [/TD]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom