Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,180
- 17,644
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi, amesema CCM imejipanga kujibu hoja na madai yanayotolewa na viongozi wa CHADEMA kwa kutumia takwimu na taarifa sahihi, badala ya kuacha kile alichodai kuwa ni upotoshaji kuendelea kusambazwa kwa wananchi.
Hapi aliyasema hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Same mkoani Kilimanjaro, katika ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira.
Amedai kuwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakitoa taarifa zisizo sahihi kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa kwa lengo la kuigombanisha Serikali na wananchi.
Kwa mujibu wa Hapi, CCM haiwezi kuendelea kukaa kimya wakati taarifa anazodai kuwa za uongo zikiendelea kutolewa hadharani, akisisitiza kuwa chama hicho kitatumia hoja, takwimu na vielelezo kueleza ukweli wa mambo kwa wananchi ili waweze kufanya maamuzi kwa kuzingatia taarifa sahihi.
Katika mkutano huo, Hapi aliwasilisha takwimu mbalimbali kuhusu baadhi ya masuala ambayo yamekuwa yakilalamikiwa na CHADEMA, akidai kuwa madai hayo hayana uhalisia na yanalenga kuwapotosha wananchi. Alitoa wito kwa wananchi kuchambua taarifa wanazopewa na kuzingatia ukweli unaotokana na takwimu na matokeo ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.