Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,902
- 3,200
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi (Sugu), amemtaka Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi, kuacha kumzungumzia Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, katika mikutano yake ya hadhara.
Soma pia: Kihongosi amshambulia Heche, CHADEMA katika ziara ya Dar es Salaam
Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Kirando, Jimbo la Nkasi Kaskazini mkoani Rukwa, Septemba 20, 2026, Sugu amesisitiza kuwa viongozi wa CCM wanapaswa kujikita katika kueleza utekelezaji wa ahadi zao kwa wananchi badala ya kutumia mikutano ya hadhara kuwashambulia na kuwazungumzia viongozi wa upinzani kama John Heche.