Daudi Mchambuzi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 62,190
- 128,272
Wananchi gani? Hawa wanaonunuliwa? Mwananci mzalendo hakika hanunuliki
ni lini wanaCCM hamjanunua mashabiki kwa kuwajaza kwenye malori na kuwapa posho na wali kwenye function zenu?
Wananchi gani? Hawa wanaonunuliwa? Mwananci mzalendo hakika hanunuliki
wewe ndio hutumie akili wewe ni mmoja sisi tupo wengi lowasa ndiye rais!!unapochangia tumia akili na sio vinginevyo.mbona mimi ni moja ya hao wananchi na simkubali?
Wana jamvi, hivi muda huu kuna uwezekano wa kuanzisha chama na kushiriki uchaguzi mkuu 2015? nauliza tu.Lowassa anaudharau uongozi mzima wa ccm hivyo awahi kujitoa maana huko mbele ni maumivu makali.
Si kwamba hatakiwi na chama bali ameamua kujiondoa mwenyewe kutokana na jeuri yake ya fedha za kifisadi
Nyerere alisema huyu Lowasa asipewe nchi ni mwizi.tunafuata wosia wa wa baba wa taifa.
Hata Yesu alikataliwa na walimu wa dini wakati wake.
Walijua bado wataendelea kuongozwa na torati ya Mussa milele.
Hawakujua mwisho wa mambo yao umefika.
Mwalimu Nyerere alichukia matajiri,utajiri na nchi matajiri katika utawala wake wote.
Akaiongoza nchi maskini na watu maskini bila kupata misukosuko inayoletwa na nguvu ya umma.
Leo tumeona nchi zote tajiri duniani zinakimbilia Tanzania.
Watanzania wote wanapenda kushirikiana na nchi Tajiri.
Watanzania wote wanapenda kuwa matajiri.
Wazazi wote wanawapenda watoto matajiri.
Wanawake wote wanawapenda wanaume matajiri.
Misikiti yote inawapenda waumini matajiri.
Makanisa yote yanawapenda waumini matajiri.
Wanasoka wote wanapenda kuchezea club tajiri.
Wafanyabiashara wote wanapenda wateja matajiri.
Bila shaka huu ni wakati wa matajiri kwani matumaini ya kila mtu zama hizi ni kuwa tajiri.
Lowassa ndiye anayefaa kuongoza zama hizi za utajirisho.
Kumkataa Lowassa ni kutangaza unafiki kwani kila mtu amelenga utajiri.
Nyerere wakati wake wa umaskini hauwezi kuendelea zama hizi za utandawazi.
Na usiombe akatokea kiongozi wa kuturudisha enzi za Umaskini ule.
Usome tu kwenye vitabu na falsafa na nadharia zile.
​njaa mbaya sana ndugu yangu, hapo kwenye red ndo itakayompitisha May pale ChimwagaSi kwamba hatakiwi na chama bali ameamua kujiondoa mwenyewe kutokana na jeuri yake ya fedha za kifisadi
ocampo four na laki si pesa mgombea wenu hatakiwi na viongozi wa chama
te teh teh teh! hivi ikatokea Lowasa akateuliwa na Chama chake na nape akawa bado ndiye mwenezi ambaye kikanuni za CCM ndiye anayemnadi mgombea wa urais ! hali itakuwaje huko kwenye tour?????????
Nimeripoti nilichokisikia. Sijaongeza chumvi
Habari wapendwa.
Akihojiwa kupitia kituo cha Radio cha Clouds FM kwenye kipindi cha Power Breakfast juu ya makundi mbalimbali ya kijamii kumtaka Lowasa kutangaza nia yamkugombea nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2015, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Nape Moses Nnauye amesema kuwa kimsingi Lowasa ameonesha na ametangaza nia ya kugombea nafasi hiyo kwa muda mrefu na ndo maana chama kilimwadhibu kwa kuanza kampeni kabla ya wakati wake. Anasema kuwa kinachofanyika kwa sasa ni usanii na ulaghai wa kisiasa wa mwanasiasa huyo ambaye anausaka urais kwa udi na uvumba na kwamba kinachofanyika kwa sasa ni muendelezo wa kampeni za mapema zinazovunja kanuni na misingi ya chama.
Anasema kuwa si kweli kuwa makundi hayo ndiyo yanayomtaka Liwasa agombee bali watu hao wanaandaliwa na gharama zote zinalipwa na Lowasa ikiwa ni pamoja na nauli, malazi, chakula pamoja na fedha zinazotolewa kwa lengo la kugharamia uchukuaji wa fomu. Nape anaongeza kwa kusema kuwa wanazo taarifa kuwa makundi mbalimbali yanaendelea kuandaliwa ambayo yataenda Dodoma siku si nyingi. Anasema kuwa wakiwa Kilimanjaro, wamepata taarifa za baadhi ya watu walioombwa na Team Lowasa kwenda Dodoma. Ameyataka makundi hayo kuwa ni pamoja na Walemavu na Wafanya Biashara ndogo ndogo maarufu kama Wamachinga.
Akitoa ufafanuzi zaidi anasema kuwa nyumbani kwa Lowasa yamewekwa mahema na viti vya kutosha muda mrefu hata kabla ya kundi la kwanza kwenda. Anasema kuwa kama kweli wageni hao hawakutokana na jitihada zake Lowasa, maandalizi hayo ya nini? Kwa nini waitwe waandishi wa habari na pia maandalizi ya chakula cha wageni hao kufanyika hata kabla ya ujio wa wageni hao? Anahoji Nape Nnauye.
Kwa msingi huo, Nape anasema kuwa hatua ambayo amefikia Lowasa haivumiliki na kwamba mwanasiasa huyo amejiondoa mwenyewe kwenye kinyang'anyiro cha urais kwa Tiketi ya CCM labda kama jitihada zake zinalenga kugombea nafasi hiyo kupitia chama kingine ambacho Nape hakukibainisha.
My Take: Naamini kuwa Nape hakukurupuka kusema aliyosema na bila shaka amepata baraka za viongozi wake akiwemo Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ambaye yupo naye sambamba kwenye ziara zake pamoja na Mwenyekiti, Jakaya Kikwete. Lowasa ujumbe ndio huo. Harakati zako ni sawa na mtu anayetwanga maji huku akitaraji kupata unga. Nakuhurumia sana
Hoja yako haiswii, coz' kauli ya JK ni hii hapa: Lowassa anadondokea hapo kwenye RED (whether anafaa au hafai)... yeye tayari alishajitokeza tangu zama hizo na kauli ya kuwashawishi ni kwa ajili ya wale ambao hawajajitokeza!
Navyomjua jk hataki kupiga kelele na Lowasa anamsubiri kwenye kanuni dakika za mwisho amtandike hataamini masikio na macho yake.