Nape: Lowassa ameanza kufanya kampeni, yuko hatarini kuenguliwa

Nape: Lowassa ameanza kufanya kampeni, yuko hatarini kuenguliwa

Nape ni nani ndani ya Chama.... Huyu huyu sii ndiyo alimtukana Jakaya 2005? Leo hii yuko wapi?
 
Tusubiri mwisho wa sinema wakati wa uteuzi. Nina uhakika ccm hakuna mwenye ubavu wa kumnyooshea kidole Lowassa. Maamuzi magumu kama hayo yanawezekana kwa CDM tu.

Ni Kweli MKUU. Nape na Makonda hakuna rangi ambayo hawataona kama Edo akiwa Rais
 
Nape ni nani ndani ya Chama.... Huyu huyu sii ndiyo alimtukana Jakaya 2005? Leo hii yuko wapi?
Nape ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM. Ni mtu muhimu sana katika kutoa habari na msimamo wa chama juu ya masuala kadhaa. Si mtu wa kumbeza na kumdharau. Anaongea na Katibu Mkuu na Mwenyekiti muda wowote. Bila shaka alichoongea leo ndio msimamo wa viongozi wake
 
CCM ni ya wanachama wote.... Kila mwanachama analipia kadi kwa gharama ile ile, na wote tunapata kadi ya kijani
 
Tatizo la Nape ni kuwa haaminiki sana, tayari ana mgombea wake kwapani, hebu afikirie Membe angefanyiwa hayo anayofanyiwa Lowassa angeweza kutamka hayo maneno? wao wakubali kuwa, Lowassa kawazidi mbinu za kisiasa, Ikulu haiji kwa kukaa nyumbani, lazima utafute namna ya kufika huko, kwani kanuni za CCM zinazuia watu kumshawishi mtu kwa kwenda kwake?

Lowassa na Nape ni nani aliyetangulia kujiunga na CCM na nani anayeijua vzr CCM? Nape hajui kusoma alama za nyakati...aliwahi kusema kuwa, Jakaya k. akishinda Urais atahama Nchi, lakini hadi leo bado yupo!!!!
 
Habari wapendwa.

Akihojiwa kupitia kituo cha Radio cha Clouds FM kwenye kipindi cha Power Breakfast juu ya makundi mbalimbali ya kijamii kumtaka Lowasa kutangaza nia yamkugombea nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2015, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Nape Moses Nnauye amesema kuwa kimsingi Lowasa ameonesha na ametangaza nia ya kugombea nafasi hiyo kwa muda mrefu na ndo maana chama kilimwadhibu kwa kuanza kampeni kabla ya wakati wake. Anasema kuwa kinachofanyika kwa sasa ni usanii na ulaghai wa kisiasa wa mwanasiasa huyo ambaye anausaka urais kwa udi na uvumba na kwamba kinachofanyika kwa sasa ni muendelezo wa kampeni za mapema zinazovunja kanuni na misingi ya chama.

Anasema kuwa si kweli kuwa makundi hayo ndiyo yanayomtaka Liwasa agombee bali watu hao wanaandaliwa na gharama zote zinalipwa na Lowasa ikiwa ni pamoja na nauli, malazi, chakula pamoja na fedha zinazotolewa kwa lengo la kugharamia uchukuaji wa fomu. Nape anaongeza kwa kusema kuwa wanazo taarifa kuwa makundi mbalimbali yanaendelea kuandaliwa ambayo yataenda Dodoma siku si nyingi. Anasema kuwa wakiwa Kilimanjaro, wamepata taarifa za baadhi ya watu walioombwa na Team Lowasa kwenda Dodoma. Ameyataka makundi hayo kuwa ni pamoja na Walemavu na Wafanya Biashara ndogo ndogo maarufu kama Wamachinga.

Akitoa ufafanuzi zaidi anasema kuwa nyumbani kwa Lowasa yamewekwa mahema na viti vya kutosha muda mrefu hata kabla ya kundi la kwanza kwenda. Anasema kuwa kama kweli wageni hao hawakutokana na jitihada zake Lowasa, maandalizi hayo ya nini? Kwa nini waitwe waandishi wa habari na pia maandalizi ya chakula cha wageni hao kufanyika hata kabla ya ujio wa wageni hao? Anahoji Nape Nnauye.

Kwa msingi huo, Nape anasema kuwa hatua ambayo amefikia Lowasa haivumiliki na kwamba mwanasiasa huyo amejiondoa mwenyewe kwenye kinyang'anyiro cha urais kwa Tiketi ya CCM labda kama jitihada zake zinalenga kugombea nafasi hiyo kupitia chama kingine ambacho Nape hakukibainisha.

My Take: Naamini kuwa Nape hakukurupuka kusema aliyosema na bila shaka amepata baraka za viongozi wake akiwemo Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ambaye yupo naye sambamba kwenye ziara zake pamoja na Mwenyekiti, Jakaya Kikwete. Lowasa ujumbe ndio huo. Harakati zako ni sawa na mtu anayetwanga maji huku akitaraji kupata unga. Nakuhurumia sana

Swala la gamba mpaka sasa limeishia wapi?
 
Lowassa asipogombea ccm,wemekwisha.
Hakuna Presidential candidate ccm anayemkaribia Lowassa hata kwa mbali."Quote my words"

Aidha una Mislead au hujui nani hasa anastahili na anafaa kuwa Rais wa tano wa nchi hii kwa ticket ya CCM. Ushabiki huu ndio unaopoteza Dira na mwelekeo wa nchi, matokeo yake tunatengeneza matatizo tutakayokuta mbeleni. Jaribu kurudi kwenye misingi.
 
Tusubiri mwisho wa sinema wakati wa uteuzi. Nina uhakika ccm hakuna mwenye ubavu wa kumnyooshea kidole Lowassa. Maamuzi magumu kama hayo yanawezekana kwa CDM tu.

Well said mkuu... Hao wanajipa moyo tu, mwisho wa siku hakuna mwenye ubavu wa kumkata Lowassa....
 
Hali isiyo ya kawaida amefikia kuudanganya summa kwamba yeye yuko mzima wa afya kwa kumuarika mpiga ampige picha akifanya mazoezi kitu ambacho kiliandaliwa huku wananchi wakijua kabisa kuwa hayuko sawa kiafya....hahahahaaa jamaa kapania kiukweli

hivi mnakumbuka jk wakati anagombea ccm nape alisema jk ana ukimwi?na jk mpaka leo anadunda,ndicho hicho hicho kinachotokea kwa lowassa,jiandaeni kisaikolojia lowaasa ndiye rais ajaye
 
lowa jembe wananchi tumesha mkubali nape ninani?

wewe na nani? nakubaliana na wewe kuwa lowasa ni jembe kwa kutindua pesa na mali za umma, lakini si kwingine, hata mmsafishe vipi bado nijizi tu, kuna msemo usemao, UKITAKA KUNIJUA MI NI NANI ANGALIA MARAFIKI ZANGU.
 
Well said mkuu... Hao wanajipa moyo tu, mwisho wa siku hakuna mwenye ubavu wa kumkata Lowassa....
Suala hapa si kumkata Lowasa bali kukiuka maadili ya chama. By the way, ni kitu gani kinawapa jeuri kuwa Lowasa hawezi kuondolewa kutokana na makosa anayofanya? Je ni ufisadi Wake?
 
Back
Top Bottom