Nape: Lowassa ameanza kufanya kampeni, yuko hatarini kuenguliwa

LIZABONI

Kwani Nape hakuwahi kusema vigogo wa CCM wajivue magamba?? nini kilitokea? na wakati huopia alisema ametumwa na uongozi wajuu wa CCM hata hili la Lowasa naona nape Amekurupuka tu
 
sawa ndugu Nape , sasa hela zake huyu mtu atazirudishaje jamani ? muwe na utu bhana !
 
Habari wapendwa.

Akihojiwa kupitia kituo cha Radio cha Clouds FM kwenye kipindi cha Power Breakfast juu ya makundi mbalimbali ya kijamii kumtaka Lowasa kutangaza nia yamkugombea nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2015, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Nape Moses Nnauye amesema kuwa kimsingi Lowasa ameonesha na ametangaza nia ya kugombea nafasi hiyo kwa muda mrefu na ndo maana chama kilimwadhibu kwa kuanza kampeni kabla ya wakati wake. Anasema kuwa kinachofanyika kwa sasa ni usanii na ulaghai wa kisiasa wa mwanasiasa huyo ambaye anausaka urais kwa udi na uvumba na kwamba kinachofanyika kwa sasa ni muendelezo wa kampeni za mapema zinazovunja kanuni na misingi ya chama.

Anasema kuwa si kweli kuwa makundi hayo ndiyo yanayomtaka Liwasa agombee bali watu hao wanaandaliwa na gharama zote zinalipwa na Lowasa ikiwa ni pamoja na nauli, malazi, chakula pamoja na fedha zinazotolewa kwa lengo la kugharamia uchukuaji wa fomu. Nape anaongeza kwa kusema kuwa wanazo taarifa kuwa makundi mbalimbali yanaendelea kuandaliwa ambayo yataenda Dodoma siku si nyingi. Anasema kuwa wakiwa Kilimanjaro, wamepata taarifa za baadhi ya watu walioombwa na Team Lowasa kwenda Dodoma. Ameyataka makundi hayo kuwa ni pamoja na Walemavu na Wafanya Biashara ndogo ndogo maarufu kama Wamachinga.

Akitoa ufafanuzi zaidi anasema kuwa nyumbani kwa Lowasa yamewekwa mahema na viti vya kutosha muda mrefu hata kabla ya kundi la kwanza kwenda. Anasema kuwa kama kweli wageni hao hawakutokana na jitihada zake Lowasa, maandalizi hayo ya nini? Kwa nini waitwe waandishi wa habari na pia maandalizi ya chakula cha wageni hao kufanyika hata kabla ya ujio wa wageni hao? Anahoji Nape Nnauye.

Kwa msingi huo, Nape anasema kuwa hatua ambayo amefikia Lowasa haivumiliki na kwamba mwanasiasa huyo amejiondoa mwenyewe kwenye kinyang'anyiro cha urais kwa Tiketi ya CCM labda kama jitihada zake zinalenga kugombea nafasi hiyo kupitia chama kingine ambacho Nape hakukibainisha.

My Take: Naamini kuwa Nape hakukurupuka kusema aliyosema na bila shaka amepata baraka za viongozi wake akiwemo Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ambaye yupo naye sambamba kwenye ziara zake pamoja na Mwenyekiti, Jakaya Kikwete. Lowasa ujumbe ndio huo. Harakati zako ni sawa na mtu anayetwanga maji huku akitaraji kupata unga. Nakuhurumia sana
[/QU
Jiurumie wewe na Nape wako lowassa hazuiliki.
 
mtapigana sanaaaa lakini hamtashinda lowasa wananchi wamesha mkubali
 
Fisadi Lowassa anautaka urais kwa udi na uvumba, kwanini? Yani nguvu zote hizi anazotumia ana agenda gani? hatufai huyu mtu hata kidogo...ufisadi aliofanyia hili taifa inatosha...
 
Demokrasia kutendeka katika nchi amayo watu wake ni masikini wa kipato ni changamoto sana. Napendekeza tuwe na midahalo ya kuwachuja viongozi wetu hasa kwa ngazi za ubunge na urais. Maswali yawe objective ndipo tutapowajua viongozi ni wapi na wahamasishaji ni wakina nani.
 
Pendekezo lako ni zuri sana. Nami naunga mkono. Ila Lowasa akae pembeni baada ya kukiuka maadili na miiko ya chama na taifa
 
Na sasa kuna kundi la watu zaidi ya 10,000 wanajiandaa kwenda kumpokea monduli akitokea dodoma weekend hii na hao tena ni yeye anaandaa?Nape soma alama za nyakati wewe endelea kupayuka kama makamba usije kujuta baadae,makonda kaanza kubadilika
 
Habari wapendwa.

Akihojiwa kupitia kituo cha Radio cha Clouds FM kwenye kipindi cha Power Breakfast juu ya makundi mbalimbali ya kijamii kumtaka Lowasa kutangaza nia yamkugombea nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2015, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Nape Moses Nnauye amesema kuwa kimsingi Lowasa ameonesha na ametangaza nia ya kugombea nafasi hiyo kwa muda mrefu na ndo maana chama kilimwadhibu kwa kuanza kampeni kabla ya wakati wake. Anasema kuwa kinachofanyika kwa sasa ni usanii na ulaghai wa kisiasa wa mwanasiasa huyo ambaye anausaka urais kwa udi na uvumba na kwamba kinachofanyika kwa sasa ni muendelezo wa kampeni za mapema zinazovunja kanuni na misingi ya chama.

Anasema kuwa si kweli kuwa makundi hayo ndiyo yanayomtaka Liwasa agombee bali watu hao wanaandaliwa na gharama zote zinalipwa na Lowasa ikiwa ni pamoja na nauli, malazi, chakula pamoja na fedha zinazotolewa kwa lengo la kugharamia uchukuaji wa fomu. Nape anaongeza kwa kusema kuwa wanazo taarifa kuwa makundi mbalimbali yanaendelea kuandaliwa ambayo yataenda Dodoma siku si nyingi. Anasema kuwa wakiwa Kilimanjaro, wamepata taarifa za baadhi ya watu walioombwa na Team Lowasa kwenda Dodoma. Ameyataka makundi hayo kuwa ni pamoja na Walemavu na Wafanya Biashara ndogo ndogo maarufu kama Wamachinga.

Akitoa ufafanuzi zaidi anasema kuwa nyumbani kwa Lowasa yamewekwa mahema na viti vya kutosha muda mrefu hata kabla ya kundi la kwanza kwenda. Anasema kuwa kama kweli wageni hao hawakutokana na jitihada zake Lowasa, maandalizi hayo ya nini? Kwa nini waitwe waandishi wa habari na pia maandalizi ya chakula cha wageni hao kufanyika hata kabla ya ujio wa wageni hao? Anahoji Nape Nnauye.

Kwa msingi huo, Nape anasema kuwa hatua ambayo amefikia Lowasa haivumiliki na kwamba mwanasiasa huyo amejiondoa mwenyewe kwenye kinyang'anyiro cha urais kwa Tiketi ya CCM labda kama jitihada zake zinalenga kugombea nafasi hiyo kupitia chama kingine ambacho Nape hakukibainisha.

My Take: Naamini kuwa Nape hakukurupuka kusema aliyosema na bila shaka amepata baraka za viongozi wake akiwemo Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ambaye yupo naye sambamba kwenye ziara zake pamoja na Mwenyekiti, Jakaya Kikwete. Lowasa ujumbe ndio huo. Harakati zako ni sawa na mtu anayetwanga maji huku akitaraji kupata unga. Nakuhurumia sana

Ccm na nape hamna ubavu huo kwani hamna vikao vya ndani vya chama mpaka mje tulilia humu mnakuwa kama joka la kibisa bana.
 
Ni kweli mbinu za kununua watu ni staili yake nape, Lakini Nape kaamua kujitoa Fahamu kisa Eti kanunuliwa na Membe kwa pesa Haramu za Marehemu Gadafii, Nape haongei yale maneno toka Rohoni bali kaamua kumfurahisha boss wake Membe.

Pesa zenyewe zilikua za kujenga misikiti nchi nzima.
Sasa badala angalau ya kujenga hata misikiti kila mkoa angalau zionekane zimefanya kazi iliyikusudiwa.
Membe ,Nape na Riz1 wamezifukia kwenye mahandaki.
Sijui wanataka kununua silaha au nini mana kila siku wanasema nchi inaelekea kubaya wanapoona Lowasa anazidi kupaa angani.
 
Mimi nilijua jamani huyu jambazi hafiki popote.hongera ccm tunawasubiri sasa huku ukawa.
 
Nchi hii haiwezi kuongozwa na wezi wa mali za umma
 
Wananchi gani? Hawa wanaonunuliwa? Mwananci mzalendo hakika hanunuliki
ndugu yangu kataa kubali lowasa ameshakuwa rais kabla jk hajamaliza mda wake watu wanamsikiliza kama rais!!
 
Back
Top Bottom