* Ni kweli Ufisadi wa Mbowe na Slaa ni Mkubwa zaidi wa EPA, DOWANS, Madini kwa CCM kuwafanya hao viongozi wa Chadema kuhamia CCM? Au ni Pesa?
In matters of style, swim with the current; in matters of principle, stand like a rock.
ALIYEKUWA Katibu wa Chadema Kata ya Ulugu
Saturday, 14 May 2011 12:11 Gazeti la Uhuru
* Ufisadi wa Mbowe, Slaa waivuruga
* Makatibu, makada 172 wakihama
* Nape ajibu mapigo, Chadema wazushi
* Wachakachua takwimu kujisafisha
* Kada wao aanika ufisadi wa fedha za harambee ya maandamano mikoani
NA WAANDISHI WETU
HALI ya hewa imezidi kuchafuka ndani ya Chadema kufuatia kuibuliwa kwa ufisadi wa kutisha dhidi ya viongozi hao wa ngazi ya juu. Watumishi wa ngazi ya chini na makada wa Chadema wameanza kuhoji juu ya Katibu Mkuu Dk. Slaa na Mwenyekiti Taifa, Freeman Mbowe, wanavyotafuna mamilioni za shilingi ya chama hicho. Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku mbili tu tangu Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kuanika siri nzito za ufisadi wa fedha za ruzuku kutoka serikali unaofanywa na vigogo wa Chadema. Kutokana na kukerwa na ufisadi huo, makatibu wawili na wanachama 172 wamekihama chama hicho na kujiunga na CCM mkoani hapa. Mbali na kuihama Chadema inayodaiwa tuhuma mbalimbali, ikiwemo kupeana madaraka kwa ukanda, pia wamefichua siri nzito juu ya viongozi hao kuwachangisha fedha wananchi wakati wa maandamano. Makatibu waliotangaza kukihama na kujiunga na CCM ni Leonard Peter (Kata ya Urugu), ambaye amekimbia na wanachama 150 na Joseph Peter (Kata ya Kyengege), ambaye amejiunga na CCM akiwa na wanachama 22.
Makada hao ambao ni nguzo kubwa ya chama hicho, walitangaza kujiunga na CCM juzi kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Makunda, Jimbo la Iramba Magharibi, Singida. Wanachama hao wapya walikabidhiwa kadi na Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Chiligati kwa pamoja na Nape. Mapema juzi, wanachama wengine 150 wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chadema Kata ya Msisi, Athumani Rajabu, walitangaza kukihama na kujiunga na CCM katika mkutano uliofanyika Stendi ya zamani mjini Singida. Akizungumza kwenye mkutano huo, Nape alimwaga hadharani ufisadi unaofanywa na Mbowe na Dk. Slaa, akidai wamekuwa wakitafuna mamilioni ya fedha ambazo wanashinikiza kulipwa na Chadema kwa njia mbalimbali. Nape aliwaeleza wananchi kuwa Dk. Slaa ameshinikiza kulipwa mshahara wa sh. milioni 7.14 kwa mwezi, kikiwa ni kiasi kikubwa kuliko mbunge, ambapo pia amekuwa akilipwa posho mbalimbali. Pia, Mbowe anadaiwa kushinikiza na kufanikiwa kuiuzia Chadema malori matatu aina ya Fuso kwa sh. milioni 480, licha ya kuwa chakavu.
Kwa upande wake, Peter akizungumza na wananchi alisema, ameshtushwa na ufisadi wa viongozi wa Chadema na kuamua kukimbia.
Alisema awali alidhani viongozi hao ni watu safi, na kwamba wakati wa uchaguzi mkuu Chadema ilishindwa kutoa fedha hivyo kuamua kujitolea mali zake ili kukiwezesha kishinde udiwani, ambapo kilifanikiwa kupata. Alisema alikuwa na imani na Dk. Slaa na Mbowe, ambapo aliuza ng'ombe wake 17 na mtaji wa biashara zake unaofikia sh. milioni nne ili kuisadia Chadema kufanya vizuri, lakini hakuna zuri alilolipwa na sasa amefisilisika. Niliwaomba fedha za kampeni, lakini wakaniambia nikope kwa wafanyabiashara wenzangu. Baada ya uchaguzi na diwani kushinda, nimekumbusha ahadi wakakataa kulipa kwa madai hawana fedha, lakini kila kukicha wanakula fedha na kufanya maandamano, alisema Kingu. Kingu alifichua kuwa alichobaini ndani ya Chadema ni kuwa hakuna siasa za kweli, bali ni mradi wa viongozi wachache, akiwemo Dk. Slaa na Mbowe na ndiyo, maana wanapenda maandamano ili kupata fedha za harambee. Kuna harambee nyingi tunashiriki kwa siri kuchangia maandamano, fedha nyingi zinapatikana, lakini ndiyo hivyo zinakwenda kwa wajanja wachache. Watu wamechoka kuchangishwa, alipasua Kingu, huku akishangiliwa.
Wachakachua takwimu kujisafisha
Kutokana na kutotarajia kuibuliwa kwa ufisadi juu ya mshahara wa Dk. Slaa na ununuzi wa malori chakavu, uongozi wa Chadema umedaiwa kuchakachua takwimu zake ili kuzuia hasira za wanachama wake. Habari kutoka ndani ya Chadema zimedai kuwa, takwimu za kile kilichodaiwa kumjibu Nape baada ya kuwalipua Dk. Slaa na Mbowe, ziliztolewa na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Anthony Komu, zimechakachuliwa. Komu anadaiwa kuwa mshirika mkubwa wa vigogo hao na kwamba, amepewa nafasi hiyo ili kulinda maslahi ya wakubwa na kupitisha mambo mbalimbali hata kama wanachama wengine hawaafiki. Taarifa zimesema kuwa baada ya vigogo hao kulipuliwa, tafrani kubwa ilizuka ndani ya Chadema, huku wakijaribu kumsaka mtu aliyevujisha siri hiyo nzito. Hata hivyo, wakati wakimsaka mtu huyo aliyewavua nguo, baadhi ya viongozi wake walijaribu kuchakachua takwimu hizo na kuzitoa kwa baadhi ya vyombo vya habari ili kuwarubuni wananchi. Hapa watu hawakulala hata kidogo, wanamsaka aliyevujisha siri kwa Nape, lakini walichojaribu kufanya ni kuchakachua takwimu hizo zilizotolewa, kwani si sahihi kabisa, kilisema chanzo chetu.
Nape ajibu mapigo, Chadema wazushi
Mwigulu aponda maandamano Chadema
Katibu wa NEC ya CCM, Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba, ameponda maandamano ya Chadema yanayofanywa mikoa mbalimbali nchini. Amesema maandamano hayo yamekuwa sehemu ya kuchangia maisha magumu kwa Watanzania, kwa kuacha kufanya shughuli za uzalishaji mali. Nchemba aliwaasa wananchi kutokubali kurubuniwa na kukubali kuandamana, kwani wanaonufaika ni viongozi wachache wa Chadema kwa kupata fedha za harambee. Wananchi wanaacha kazi wanakwenda kuandamana, wakati wenzao wana njia za kupata fedha kwa kukinyonya chama chao. Wasikubali kurubuniwa wafanye kazi kuboresha vipato. Kuna siku Mbowe au Slaa waliwahi kuwagawia watu fedha baada ya kuandamana, mbona wao wanagawana posho kubwa kujipongeza? alihoji Nchemba. Alisema, kimsingi, CCM imefanya mengi ya maendeleo, lakini Chadema na baadhi ya vyama vya siasa wamekuwa wakiyabeza hata pale maendeleo yapoonekana wazi wazi. Nchemba aliwataka Mbowe na Slaa kuitambua miradi ya maendeleo kwa kupapasa kwa mikono kama hawawezi kuiona kwa macho.