Kifo hakina huruma, alipata kuimba dokta Remmy Ongara.
Akionekana mwenye majonzi na haamini kilichotokea hadi sasa, Nape ameonekana akitafuta faraja japo kwa kuchezea vumbi kama mtoto wakati wa mazishi ya godfaza wake huko kijiji cha Chiponda Rondo kwa Membe.
Akiwa mpweke na asiye na kampani yoyote ya marafiki nape aliendelea kujiinamia peke yake huku kaipa mgongo kadamnasi iliyokuwa inaendelea na mazishi huku watu wakionekana kumpuuza kana kwamba sio mbunge wa huko mpaka bwana mmoja wa usalama alipoamua kumsogelea.
Hali hii imetokana na Mungu kumjibu Nape kwa haraka, kwa wakati na kwa ghafla kufuatia kiburi chake cha kibinadamu na mamlaka dhidi ya familia ya JPM, marehemu JPM na watanzania wengi waliohuzunishwa na kifo cha JPM.
Kweli Mungu fundi.
View attachment 2624587
Ni nini cha ajabu? Hivi kuna marehemu ambaye kifo chake wanakosekana waliohuzunika mno, waliohuzunika kiasi, wsliohuzunika kawaida na wale walioona ni kawaida kwa vile kifo ni kwaajili ya kila mwanadamu?
Unakuwa kwenye kundi lipi katika huzuni, itategemea ukaribu wako na marehemu, impact yake katika maisha yako either positively or negatively.
Mathalani Magufuli alikuwa Rsis, Mwalimu Nyerere baba wa Taifa, Mkapa alikuwa Rais, Kawawa waziri mkuu, membe waziri; je, unaweza kusema vifo vya hawa viongozi wetu vilikumiza au vitakuliza kuliko vifo vya ama wazazi wako au wadogo zako su wanafamilia wengine?
Usilazimishe mtu ahuzunike kwa kiwango sawa na ulivyohuzunika wewe kwa sababu huzuni au kulia ni hisia, ni reflex action, vinginevyo utafanya maigizo ya kulia au kuhuzunika ili tu watu waone umehuzunika sana kama walivyofanya baadhi ya watu, mpaka kujifanya wamezimia wakati wa msiba wa Magufuli wakati wakiwa wameendelea kushikilia mifuko yao.
Sisi tulimfahamu Membe kama kiongozi, kuna wengine, siyo tu alikuwa kiongozi bali alikuwa mwanafamilia, rafiki na ndugu. Hawa watakuwa wameumizwa zaidi kuliko sisi wengine. Ndiyo maana siku zote utawasikia watu wakisema kuwa tunawapa pole waliopatwa na msiba, wanafamilia, ndugu, marafiki wa karibu na wafiwa wote.
Kwa upande wa Magufuli, Watanzania walipatwa na msiba wa Rais, lakini kuna watu walipatwa na msiba wa Baba, ndugu, rafiki na mwanafamilia mwenzao. Kwa Watanzania, kusema walifikwa na msiba, inakuwa imekaa kiujumla sana, na pengine kisiasa maana kuna watu ambao maisha yao hayakuwahi kuguswa na marehemu, na wengine waliguswa positively, wengine negatively, wengine hawakuwahi kuonana naye uso kwa uso hata mara moja, wengine walionana naye karibia kila siku, hivyo watu hawa huzuni yao itatofautiana hivyo hivyo.
Hivyo itakuwa ni ujinga wa hali ya juu kuamini au kutegemea watu waguswe na msiba wa Magufuli, Membe, Mkapa au wa ndugu yako binafsi kwa kiwango sawa, labda watu hao waigize. Ni uungwana tu huwa unatumika, wa kuhuzunika pamoja na wafiwa.