Nape achezea udongo kwenye mazishi ya Membe

Nape achezea udongo kwenye mazishi ya Membe

Yaani Afe Membe halafu iwe Mungu kamjibu Nape?[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Na hawa wengine wanaokufa kila siku Mungu humjibu Nani? Ni Mungu yupi huyo anayejibu Kwa vifo?

Na kifo cha bwana Yule Mungu alikuwa anamjibu Nani[emoji1787][emoji1787][emoji1787]? Wafuasi wa bwana Yule mnachekesha sana
Asingekuwa anachezea vumbi kule makaburini
 
Kifo hakina huruma, alipata kuimba dokta Remmy Ongara.

Akionekana mwenye majonzi na haamini kilichotokea hadi sasa, Nape ameonekana akitafuta faraja japo kwa kuchezea vumbi kama mtoto wakati wa mazishi ya godfaza wake huko kijiji cha Chiponda Rondo kwa Membe.

Akiwa mpweke na asiye na kampani yoyote ya marafiki nape aliendelea kujiinamia peke yake huku kaipa mgongo kadamnasi iliyokuwa inaendelea na mazishi huku watu wakionekana kumpuuza kana kwamba sio mbunge wa huko mpaka bwana mmoja wa usalama alipoamua kumsogelea.

Hali hii imetokana na Mungu kumjibu Nape kwa haraka, kwa wakati na kwa ghafla kufuatia kiburi chake cha kibinadamu na mamlaka dhidi ya familia ya JPM, marehemu JPM na watanzania wengi waliohuzunishwa na kifo cha JPM.

Kweli Mungu fundi.

View attachment 2624587
Labda ni agizo alipewa
 
Usichokijua ni kwamba wema haulingani na uovu! Wamekufa viongozi wengi sana ulishawahi sikia au kuona watu wakishangilia? Kwann yeye? Wazazi wa
Anzory
Ben sanane
Mawazo
Na wale waliokotwa kwenye viroba ilikuwa lazima washangilie maana muovu aliondoka! Sasa unajifariji kwa kifo cha membe? Membe alikuwa nani hapa nchini? Alimuua nani? Alimteka nani? Alipora pesa zq nani? Alibambikiza kesi kina nani?
Ujinga wa kihalaiki unawasumbua nyie
Alishiriki ufedhuli wa kumhujumu JPM na hatimae kufurahia kifo chake
 
We KE una matatizo kwani hujui hata faiza unaweza igeuza ikawa fala.
Wewe geuza upendavyo, haitakuwa. Faiza ni neno la Kiarabu maana yake ni ushindi.

Neno shenzi limetokana na neno la Kijerumani sheiza, ikimaanisha nguruwe. Tena kwa kukufafanulia zaidi, ni ile harufu mbaya ya nguruwe, ndipo pia lilipopatikana neno "ushuzi".


Unaweza kuiona kazi yangu nyingine ya "anthropology" ya lugha hapa...


Huwa sikisii.
 
Kazi unayo. Unapambana nao kila kona.
Mm sipambani na mtu mjinga anayetetea uovu , uaji wizi na utekaji kwa kisingizio cha uzalendo. Napambania haki na wala siyo hango wala upendeleo. Nyie wengine mishipa inawatoka hapa kwasababu ulaji umekatwa na mungu hapo 17.3 imekuwa nongwa
 
Nilikuwa sijui kama ni wengi waliumizwa na kifo cha kipenzi chetu JPM.

Kifo cha Membe ni kama kimeibua upya maumivu ya watu juu ya kifo cha JPM.

Ninaandika huku nikitokwa na machozi. Namkumbuka JPM.

Tunaoendelea kumlilia JPM tunyooshe mikono hapa.
Kosa kubwa ambalo watu wengi walilifanya ni kushangilia kifo cha JPM, Haikuwa sawa kabsa.
Wakati kuna watu walikuwa wanamuona JPM Kama mtu mbaya wao wakasahau jpm huyo huyo ana watu wanaomuona kama mkombozi kwao, Kwa kweli Mbele ya Mungu Watanzania wanaojua habari za Membe kama hawapo au ni kiduchu sana, JPM Anabaki kuwa shujaa wa walio wengi.
RIP John Pombe, Tutakukumbuka siku zote.
 
Mkuu wafuasi wa jiwe wanajipoozea machungu kwa Membe kitu ambacho hakihusiani wala kufanana hata kidogo ..Jpm na Membe hawafanani...
Hatufananishi watu. Tunafananisha tendo la kufa. Kwani Membe alipokuwa anamponda Magu alimfikia hata robo kiukubwa.? Maana Membe hakuwahi kuwa hata waziri mkuu au spika wa bunge.
 
Aliyefariki ni Ben Membe, hizi threads mnazozijaza hapa JF sio uungwana. Ben Membe alikuwa mtu mwema, ameacha famili na marafiki. Hizi dhihaka kuhusu msiba wake sio za kuziendekeza.

BTW, kufurahia kifo cha Magufuli pia haikuwa sawa kwa mtu yeyote. Kila mtu atakufa eventually.

Leo unaweza kuwa unaandika ujinga hapa alafu kesho msiba utahamia nyumbani kwako. Tujifunze utu na uungwana.
Nakazia
 
Mm sipambani na mtu mjinga anayetetea uovu , uaji wizi na utekaji kwa kisingizio cha uzalendo. Napambania haki na wala siyo hango wala upendeleo. Nyie wengine mishipa inawatoka hapa kwasababu ulaji umekatwa na mungu hapo 17.3 imekuwa nongwa
Hapo umeongea kiume. Unapambania asali. Utakuwa team Wema hawafi. Poleni na msiba na bado.
 
Back
Top Bottom