Habari wapendwa.
Ni kama mwaka sasa nimekuwa napatwa na mawazo ya kujiua.
Hayaji kila siku na mara nyingi nafurahia maisha kama kawaida tu. Kiuchumi siko vibaya, sina deni wala vikoba ila kuna siku naweza kuamka zangu na furaha then from nowhere kuna vitu tu nikivifikiria nakua so depressed, najiona kama takataka. Najiona sina thamani, najiona a looser who is missjudged and can't do anything about it.
Kwa wanaonijua ukiwaambia nina mawazo haya watakucheka sbb nina tuvibaraka ambavyo wengi wanaota kuwa navyo ila ukweli ni kwamba kuna saa naona wanaosukuma mkokoteni au wanaouza vitumbua wana maisha mazuri kuliko mimi.
Sitaki kufa na sitakufa kwa kujiua ila najua watu wengi wanaopata mawazo ya kujiua huwa wanaishia kujiua kweli hivyo nipe neno lolote ili haya mawazo ya kijinga yaachane na mimi.
Wale wanaotoa ushauri kwa maneno makali hadi ujione mjinga ndo wazuri.Mimi nikibembelezwa ndo nazidi kuwa emotional hata kama ni mbele za watu ntaanza kulia.
Muwe na weekend njema sana wapendwa.
ASANTE
Roho ya mauti inakuandama!
Inaweza ikawa ya kutupiwa na wenye Hila na mafanikio yako!!
Nakupa kanuni Rahisi sana
Kama we ni mkristo
Ukiamka asubuhi fumba macho mwambie "Bwana yesu nashukuru sana kwa mawazo ya kujiua niliyonayo,kama ni mapenzi yako naomba iwe kama sio mapenzi yako yasiwepo kabisa moyoni mwangu"
Jioni rudia Tena hivyo hivyo kabla ya kulala!
Kama we ni muislamu
Utaanza Kwa kumfukuza shetani,halafu Bismillah arahmaan rahyiim, utasoma suratil fatiha ,ukimaliza soma ikhilaswi mara tatu halafu utamwambia mwenyezimungu kuhusu unavyojisikia ,hiyo Hali itaisha tu,rudia asubuhi na jioni!
Na kama we ni mtu wa Mungu na sio mtu wa dini,changanya maombi yote yaani unaanza kiislam baadae kikristo na mambo yatabadilika!!
Nilipata unafuu kwenye mambo fulani fulani nilipochanganya au kuomba Kwa namna zote mbili!!
Vijana Huwa tunajichnaganya sana KUTOMUOMBA MUNGU HATA KAMA NI WAHUNI KIASI GANI WE OMBA MUNGU KILA ASUBUHI NA JIONI KWENDA PEPONI AU MBINGUNI NI PROCESS YA TARATIBU WALA SIO GHAFULA BIN VUU!