Naona kama mke ananikwamisha

Naona kama mke ananikwamisha

kuna watu wa ajabu kweli hii dunia,...unamshirikisha wife kwenye mambo yako,?🤔🤔❗ yani hapo wife alitakiwa aambiwe hapa tunaondoka na anaondoka bila kuuliza,... mwanamke atakushauri nn?📍📌 hayo ndo madhara ya kumuona mke ni mwenzako,....🚮
Dah! Hii comment yako imenichekesha sana mkuu 😂😂😂

IMG_20230627_132600_750.jpg
 
Chakufanya mwambie mkeo tunauza na pesa itaingia kwa account yako na malengo ni haya tutayetekelez wote
 
Miaka 15 iliyopita nilinunua kiwanja kwa shilingi milioni 4 nikaanza ujenzi wa nyumba kwa kuunga unga na nikahamia na familia nyumba ikiwa haijakamilika.

Namalizia kidogo kidogo huku nikiwa humo humo ndani. Miaka ya kati hapo nikapoteza channel kabisa, na sijaweza kumalizia hiyo nyumba, lengo ilikuwa kuweka madirisha ya alminium, mpaka sasa kuna grills na wavu tu.

Nyumba sio mbaya na finishing ilibaki madirisha tu. Nakadiria mpaka hapo imegharimu kama milioni 45 hivi. Ghafla tu miaka ya karibuni bei za viwanja na nyumba zimepanda sana huku kwetu, majirani zangu watatu ambao viwanja na nyumba zetu zinafanana wameuza kwa shilingi milioni 150, 160 na 180. Sasa mtu anataka kuninunua mimi kwa mil 150.

Kwa sababu nimepoteza channel nikawaza kupauza nianze upya kwa kununua nyumba mbili Mbezi Msumi, Msakuzi au Mpiji Magoe au hata Kibaha, moja ya kupangisha na moja ya kuishi, chenji nitumie kuanzisha biashara ya tyre service na kuosha magari kwa sababu naiwaziaga siku zote, kama chenji ikibaki nifungue na workshop ya carpentry na wife apate milioni 6 za biashara ya ndoto zake ambayo anaiwazaga miaka zaidi ya 8 sasa.

Tukaongea na wife tukakubaliana, hata yeye anaona tulivyopigika, wakati tumekalia ardhi ya bei mbaya ambayo hatuwezi hata kuindeleza. Sasa siku mteja amekuja kulipa tufanye hiyo biashara, nilikuwa nimetoka kidogo.

Nikafika nyumbani nikakuta mteja amefika kabla yangu na wife ameshamwambia tumeghairi hatupauzi tena!!! Nilitaka hata kulia. Na jamaa anasema ameshaghairi moja kwa moja anaogopa kununua nyumba yenye mgogoro.

Nilishakuwa na mipango kama milioni ya kujikwamua kutoka kwenye hili janga la umaskini sasa hivi naona giza tena. Na wife anasema tuendelee kutafakari kwanza kama miaka 2 hivi tukiona bado tunahitaji kuuza ndio tuuze!

HAPA NAANGALIA NAMNA YA KUFANYA ILI NIPATE HIYO HELA IKIWEZEKANA KWA KUACHANA NA HUYU MAMA TUGAWANE. Naamini nikipata milioni 80 naweza kujipanga upya, hili giza la kiuchumi limekuwa zito sana.
Mke wako kashaongea na ndugu zake wanampango napo hapo kuwa makini Anaweza kukuwekea sumu ufe ili apalisi yeye LAKINI INAWEZEKANAJE WEWE UNAKUWA SIO KICHWA CHA FAMILIA KUNA VINGINE HUWA TUNAFANYA TUNACHUKUA MAAMUZI MAGUMU
 
Tulikubaliana na nilishamhakikishia kuwa mimi ntachukua mil 30 tu kwa ajili ya biashara. Mil 120 mteja ataweka kwenye akaunti yake yeye. Uwezekano wa kutumia kwa malaya ingekuwa mwisho mil 30 au?
We jamaa aisee!!yaani ela yote uweke kwenye account ya mwanamke?huwajui kumbe.
 
Kuna ndugu zangu waliwahi kuuza mashamba kwa Millioni. 100 mwaka 2007. Pesa iliisha ndani ya wiki tatu. Ama kweli pesa ni makaratasi. Ama kweli huyo mke anaakili. Niliwahi fundishwa na mama yangu kwamba usipende kuuza vitu ulivyo nunua kwaajili ya matumizi yako na familia yako. Utakuja kuuza hadi makabati na vitanda.
Kwahiyo hata kama nna mafenicha yamechoka nikaenayo tu?
 
Sasa mnunuzi anakuja vipi nyumbani bila wewe kuwepo?

Isitoshe kama mlishakubaliana bei Sasa iweje aje nyumbani badala ya ofisi ya mtaa?
 
Mwanamke ni emotional being....
Hisia zake zinapoguswa negatively lazima ata react.

Jitahidi sana kulinda hisia zake,moyo wa mwanamke ni too delicate(easily broken)

So ukitaka kuuza kitu,hakikisha vipo zaidi ya kimoja,Kama ungekuwa na nyumba mbili au tatu na unataka kuiuza moja,sidhani Kama angekaza fuvu.

Lakini kwa sasa, I think,it's too late to understand this.
 
Mwambie mkeo kuanzia sasa kapandishwa cheo na kuwa mwenyekiti wa wanawake Tanganyika..!! 😹😹

Pumbavu kweli wewe unauza vipi ardhi kiboya hivyo bila kufanya tathmini ya mnunuaji??

Na ulivyo mbinafsi eti mkeo umpe 6 mln akafungue biashara ya ndoto zake… biashara gani ya 6mln, kuuza miguu ya kuku au?? 😹😹

Kakukomesha vizuri na wanawake wengine mjifunze kwa mke wa huyu bwana, hakuna kucheka na kima yoyote ni HATUUZI TUMEAHARISHA 😹
 
Chukua mkopo Kisha mterekeze humo ndani mpaka papigwe mnadani yeye atafute pakwenda maana amepanga kukukomoa na kukutesa Kwa makusudi
Aliyekwambia mikopo wanatoa bila sahihi ya mwenza wako nani?? Muwe mnakopa kabla ya kucomment bata weeeh 😹😹😹
 
Huyo ndio anafaa kuwa mke sasa, sio wale wa ndio Mzee ndio Mzee😂😂😂.

Hiyo M80 unaiona nyingi kwa kuitaja ila ikiingia mkononi mwako kama utakua huna plan nzuri itapotea kinamna ya ajabu hadi ushindwe kuamini ni nini kimetokea.

Ingawa watu husema kimfaacho mtu chake ila mkeo nae atakua anahoja ya msingi, so kaeni tena chini muongee kwa maana kitendo cha kusema mjipe miaka miwili ya kujiuliza hii inaonesha bado anaamini unaweza ukapata vyanzo vingine vya utafutaji ndani ya muda huo.

Na kingine kama wewe ndio ulikua mchezaji wa hiyo team basi inabidi na yeye aingie ndani ili muwe mnacheza wote kwa maana yeye akienda kulia nenda kushoto jioni muweke vitu mezani.

NB: kwenye maisha ya utafutaji hautakiwi kujiona unayo plan B kwa maana itakurudisha nyuma kinamna fulani katika harakati zako na hufanya hata akili isione chochote zaidi ya hiyo plan B iliyopo, jiulize kama usingekua na hiyo nyumba unhewaza kufanya nini sasa hivi?

Njia zilizokua zinakupatia pesa hadi ukanunua kiwanja na kujenga hiyo nyumba sasa hivi zimegoma kiasi cha kufanya utamani kuuza hiyo nyumba ili uwekeze sehemu nyingine, unauhakika baada ya kufanya hivyo pesa itaanza kupatikana tena?

Pesa ni zawadi lakini pia pesa ni roho, ukipita kwenye njia zake utaikamata ila ukiwa mbali na njia zake utapishana nayo, yawezekana wewe unahisi shida yako ni mtaji lakini kumbe wala hiyo sio shida yako.

Ndio maana unaweza ukapata huo mtaji ila bado ukaendelea kuteseka na kuchanganyikiwa kisa biashara haiendi ila hasara tu ndio zinazoongozana.

Sasa tumia huo muda ambao mkeo amekupa ili muweze kujiuliza kwa pamoja.
Njoo tuoane tutakuwa matajiri fasta na watoto wetu watakuwa smart 😹😹
 
Wazazi wangu waliwahi kuniambia kwamba usikubali kuuza asset zako muhimu kutatua matatizo yako as long as upo mzima wa afya na una akili timamu

Watu wanauza asset zao kwasababu wameona fursa kubwa zaidi na sio kutatulia matatizo

Wewe hapo umeishiwa mbinu na sio pesa tu,
Angalia unakosea wapi badala ya kukimbilia kuuza nyumba...... ukikosea tu utabeba familia na kurudi kijijini kwenu au utakimbia familia

Tatizo ni kwamba utafunga akili yako ukifiria kuuza nyumba ndio solution pekee na kusahau kupambana

Wanasemaga ukianza kuuza vitu vyako vya ndani ni kama kula nyama ya mtu.... hautaacha
Baadae na hizo nyumba utauza tena mwisho utahamia kwenye fenicha, simu nk nk
Igweeeeeeeeeeee 🫡

Huyo kashaishiwa mbinu mpk mawazo kabali na ufujaji wa mali..!!
 
Linapofika swala kama hili,Wanawake huwa ni Changamoto!
Ni waoga sana.
Mara nyingi lazima huwa wanapinga na anaweza kukusema mpaka kwenu

Afu msoto wa maisha unaupata mwenyew,yeye ni kusubiria tu ila ukitaka mali zako zikusaidie anakuwekea ngumu

Kuna wanaume wanazuiliwa hata kuuza ng'ombe
 
Unaweza ona kama mke ni mtu mwenye plan nzuri kumbe anataka amtangulize jamaa chapu Ali auze pekeyake kwasababu kama walishakubaliana hakutakiwa kufanya maamuzi ya kukataa bila kumshirikisha wakati walishakubaliana
Wewe utakuwa mchawi si bure..!! 😹😹
Una mawazo mabaya na ya njaa km huyo mtoa post..!!
 
Mie naona mkeo ana akili kuliko wewe, samahani lakini, vuta miaka miwili ama minne ,unashangaa unapata wa kukupa 300-500M utashukuru wife ama unapata mchongo wa Mana zaidi unapata ugali. Unakuja uuza uzeeni kabisa huko kwa bilioni unatoa urithi kwa wanao na wewe unaoza vizuri huko Kijijini kwenu.
Kama huna hela unadhani
Hapa naungana na wewe mkuu.
Uvumilivu haujawahi kumuangusha mtu,unajua hata wale wanunuzi wanachokifanyaga ananunua kwako kisha anakausha kwa miaka 3 anakuja kuuza bei mara 2 yake.
Njaa ya muda mfupi isikufanye utoke kwenye reli kama bado mtu una nguvu za kupambana hakuna haja ya kufanya pupa,unaweza ukauza halafu pesa uliyopewa ukaenda kununua nyumba nyingine ukapigwa halafu ukakosa kotekote kuna watu wengi tu ishawahi kuwatokea hii.
Kuna vitu kama gari,TV,fenicha hivi ukiishiwa unaweza ukauza chap hela ukafanyia mambo yako halafu mbeleni mambo yakinyooka unanunua tena lakini sio nyumba haitaki masihara hapo ni kama unabet maisha yako.
 
kuna watu wa ajabu kweli hii dunia,...unamshirikisha wife kwenye mambo yako,?🤔🤔❗ yani hapo wife alitakiwa aambiwe hapa tunaondoka na anaondoka bila kuuliza,... mwanamke atakushauri nn?📍📌 hayo ndo madhara ya kumuona mke ni mwenzako,....🚮
💯 True
 
Miaka 15 iliyopita nilinunua kiwanja kwa shilingi milioni 4 nikaanza ujenzi wa nyumba kwa kuunga unga na nikahamia na familia nyumba ikiwa haijakamilika.

Namalizia kidogo kidogo huku nikiwa humo humo ndani. Miaka ya kati hapo nikapoteza channel kabisa, na sijaweza kumalizia hiyo nyumba, lengo ilikuwa kuweka madirisha ya alminium, mpaka sasa kuna grills na wavu tu.

Nyumba sio mbaya na finishing ilibaki madirisha tu. Nakadiria mpaka hapo imegharimu kama milioni 45 hivi. Ghafla tu miaka ya karibuni bei za viwanja na nyumba zimepanda sana huku kwetu, majirani zangu watatu ambao viwanja na nyumba zetu zinafanana wameuza kwa shilingi milioni 150, 160 na 180. Sasa mtu anataka kuninunua mimi kwa mil 150.

Kwa sababu nimepoteza channel nikawaza kupauza nianze upya kwa kununua nyumba mbili Mbezi Msumi, Msakuzi au Mpiji Magoe au hata Kibaha, moja ya kupangisha na moja ya kuishi, chenji nitumie kuanzisha biashara ya tyre service na kuosha magari kwa sababu naiwaziaga siku zote, kama chenji ikibaki nifungue na workshop ya carpentry na wife apate milioni 6 za biashara ya ndoto zake ambayo anaiwazaga miaka zaidi ya 8 sasa.

Tukaongea na wife tukakubaliana, hata yeye anaona tulivyopigika, wakati tumekalia ardhi ya bei mbaya ambayo hatuwezi hata kuindeleza. Sasa siku mteja amekuja kulipa tufanye hiyo biashara, nilikuwa nimetoka kidogo.

Nikafika nyumbani nikakuta mteja amefika kabla yangu na wife ameshamwambia tumeghairi hatupauzi tena!!! Nilitaka hata kulia. Na jamaa anasema ameshaghairi moja kwa moja anaogopa kununua nyumba yenye mgogoro.

Nilishakuwa na mipango kama milioni ya kujikwamua kutoka kwenye hili janga la umaskini sasa hivi naona giza tena. Na wife anasema tuendelee kutafakari kwanza kama miaka 2 hivi tukiona bado tunahitaji kuuza ndio tuuze!

HAPA NAANGALIA NAMNA YA KUFANYA ILI NIPATE HIYO HELA IKIWEZEKANA KWA KUACHANA NA HUYU MAMA TUGAWANE. Naamini nikipata milioni 80 naweza kujipanga upya, hili giza la kiuchumi limekuwa zito sana.
Hivi nyinyi mkioaga huwa mnakuwa washirika na wake zenu? Maajabu kabisa, Mimi nanunua kitu nauza taarifa tu anapata sio kushitikiana maamuzi Kwisha
 
Nenda Bank ukawakadhi hiyo nyumba, watakupa hela itakayokufaa
 
Njoo tuoane tutakuwa matajiri fasta na watoto wetu watakuwa smart 😹😹
Wewe sio wale wa ndio Mzee ndio Mzee😂😂😂... Hoja inawekwa mezani we unaishia kusema "kama ulivyosema babaa"
 
Back
Top Bottom