Naona kama mke ananikwamisha

Naona kama mke ananikwamisha

Miaka 15 iliyopita nilinunua kiwanja kwa shilingi milioni 4 nikaanza ujenzi wa nyumba kwa kuunga unga na nikahamia na familia nyumba ikiwa haijakamilika.

Namalizia kidogo kidogo huku nikiwa humo humo ndani. Miaka ya kati hapo nikapoteza channel kabisa, na sijaweza kumalizia hiyo nyumba, lengo ilikuwa kuweka madirisha ya alminium, mpaka sasa kuna grills na wavu tu.

Nyumba sio mbaya na finishing ilibaki madirisha tu. Nakadiria mpaka hapo imegharimu kama milioni 45 hivi. Ghafla tu miaka ya karibuni bei za viwanja na nyumba zimepanda sana huku kwetu, majirani zangu watatu ambao viwanja na nyumba zetu zinafanana wameuza kwa shilingi milioni 150, 160 na 180. Sasa mtu anataka kuninunua mimi kwa mil 150.

Kwa sababu nimepoteza channel nikawaza kupauza nianze upya kwa kununua nyumba mbili Mbezi Msumi, Msakuzi au Mpiji Magoe au hata Kibaha, moja ya kupangisha na moja ya kuishi, chenji nitumie kuanzisha biashara ya tyre service na kuosha magari kwa sababu naiwaziaga siku zote, kama chenji ikibaki nifungue na workshop ya carpentry na wife apate milioni 6 za biashara ya ndoto zake ambayo anaiwazaga miaka zaidi ya 8 sasa.

Tukaongea na wife tukakubaliana, hata yeye anaona tulivyopigika, wakati tumekalia ardhi ya bei mbaya ambayo hatuwezi hata kuindeleza. Sasa siku mteja amekuja kulipa tufanye hiyo biashara, nilikuwa nimetoka kidogo.

Nikafika nyumbani nikakuta mteja amefika kabla yangu na wife ameshamwambia tumeghairi hatupauzi tena!!! Nilitaka hata kulia. Na jamaa anasema ameshaghairi moja kwa moja anaogopa kununua nyumba yenye mgogoro.

Nilishakuwa na mipango kama milioni ya kujikwamua kutoka kwenye hili janga la umaskini sasa hivi naona giza tena. Na wife anasema tuendelee kutafakari kwanza kama miaka 2 hivi tukiona bado tunahitaji kuuza ndio tuuze!

HAPA NAANGALIA NAMNA YA KUFANYA ILI NIPATE HIYO HELA IKIWEZEKANA KWA KUACHANA NA HUYU MAMA TUGAWANE. Naamini nikipata milioni 80 naweza kujipanga upya, hili giza la kiuchumi limekuwa zito sana.

Binafsi Naona Mke ndio amekuokoa. Kwanini usitumie nyumba kama dhamana, ukope bank ufanye hiyo biashara? Au ni Hadi uuze ndio hiyo biashara inafanyika?
 
Wanawake wakati mwingine wanakuwaga kama malaika sasa welazimisha uone utalia
 
Huyo ndio anafaa kuwa mke sasa, sio wale wa ndio Mzee ndio Mzee😂😂😂.

Hiyo M80 unaiona nyingi kwa kuitaja ila ikiingia mkononi mwako kama utakua huna plan nzuri itapotea kinamna ya ajabu hadi ushindwe kuamini ni nini kimetokea.

Ingawa watu husema kimfaacho mtu chake ila mkeo nae atakua anahoja ya msingi, so kaeni tena chini muongee kwa maana kitendo cha kusema mjipe miaka miwili ya kujiuliza hii inaonesha bado anaamini unaweza ukapata vyanzo vingine vya utafutaji ndani ya muda huo.

Na kingine kama wewe ndio ulikua mchezaji wa hiyo team basi inabidi na yeye aingie ndani ili muwe mnacheza wote kwa maana yeye akienda kulia nenda kushoto jioni muweke vitu mezani.

NB: kwenye maisha ya utafutaji hautakiwi kujiona unayo plan B kwa maana itakurudisha nyuma kinamna fulani katika harakati zako na hufanya hata akili isione chochote zaidi ya hiyo plan B iliyopo, jiulize kama usingekua na hiyo nyumba unhewaza kufanya nini sasa hivi?

Njia zilizokua zinakupatia pesa hadi ukanunua kiwanja na kujenga hiyo nyumba sasa hivi zimegoma kiasi cha kufanya utamani kuuza hiyo nyumba ili uwekeze sehemu nyingine, unauhakika baada ya kufanya hivyo pesa itaanza kupatikana tena?

Pesa ni zawadi lakini pia pesa ni roho, ukipita kwenye njia zake utaikamata ila ukiwa mbali na njia zake utapishana nayo, yawezekana wewe unahisi shida yako ni mtaji lakini kumbe wala hiyo sio shida yako.

Ndio maana unaweza ukapata huo mtaji ila bado ukaendelea kuteseka na kuchanganyikiwa kisa biashara haiendi ila hasara tu ndio zinazoongozana.

Sasa tumia huo muda ambao mkeo amekupa ili muweze kujiuliza kwa pamoja.
Kweli kutoka 0 hadi 150 hatari pesa zahivo anaweza kupata mawazo yakabadirika
 
Umesema kwamba kipato kimetetereka, kwanini Sasa msiuze nyumba , upeleke milioni 150M UTT, gawio lako Kwa mwezi 1.25M na zaidi hii pesa itakutosha wewe na familia Yako kupanga , kula , kuishi. Na bado 150M yenu itakuwepo palepale. Kuliko kugombana kwanini msifanye hivyo mnakuwa mnapata kipato huku pesa yenu haijapotea, kuchukua pesa kwenda kuanzisha mradi mpya unaweza angukia pua.
 
Mambo yatakua mengi sio😅😅😅... Ila mwana sio mgeni na pesa sema shida ni kwamba atakua ameimiss sana pesa kwahiyo kuna vitu vingi atakua anatamani kuvifanya ila anashindwa kwakua Hana pesa so akizipata ataanza navyo kwanza, na hapo ndipo maji yatakapoenda kuzidi unga.
 
Hatar
 
Uzi ulitakiwa usomeke "Naona kama namkwamisha wife"

Lengo lako ni zuri lakini naona kabisa matokeo yake sio mazuri. Mbeleni utajuta. Afadhali hata utumie hati ya nyumba kuchukua mkopo, kuliko kuuza nyumba. Kwanza ukishauza tu, tegemea kupata wahitaji zaidi yako kwenye familia ama ukoo wenu. Hapo lazima kama milioni 20 au zaidi zitumike kutatua shida za kwenu.

Mkeo akishaona hivyo, atakuomba umjengee mama yake kakibanda ka kujisitiri ka kisasa kule kijijini kwao. Hapo sio chini ya milioni 30 (kuweka heshima ukweni). Hamsini zimeenda.

Kuna wale rafiki zako ambao mmepoteana miaka mingi tangu ulipoyumba kiuchumi? Na wao watakuja kukusalimia kwasababu wamekukumbuka sana. Kuwakaribisha, lazima 5 ziende na maji.

Unataka kununua nyumba mbili? Zote hizo za nini, kwanza unafuja pesa bure. Yule dalali unayetaka umtumie kupata hizo nyumba atakuja na bei mbaya kwa nyumba moja kali (kwa wakati huo) utaambiwa milioni 70 ina kila kitu na iko karibu na barabara kuu. Ukishainunua ndipo utaanza kuona inazeeka haraka, rangi inabanduka, inaanza kuharibika. Unagundua ilijengwa kwa tope na miti kisha ikafanyiwa finishing ya bei mbaya. Mpaka hapo milioni 105 imeenda.

Ili kuweka mambo sawa utakarabati nyumba yako ya milioni 70 ili kuipa hadhi ya milioni 100+.

Milioni 45 iliyobaki, unagundua wife ameshaanza kupendeza na kuingia vicoba huku mnakula mboga nane (siunajua hauwezi kula tembele wakati una milioni mia ndani?) Unagundua ndani ya ile miezi miwili ya kujipanga kuhama mmeshatumia milioni 15. Ghafla unakumbuka uhamisho wa watoto shule. Wife anakwambia angalau muwapeleke English medium (day) tuseme una watoto wawili. Kila mtoto anakulazimu umlipie milioni 1.5 si pesa ipo? Kwanza soon utafungua biashara hivyo haiihitaji uwe bahili ukakosa baraka za familia. Kwenye milioni 30 unebaki na 27.

Ulisema ndoto ya wife ni kumiliki biashara ya milioni 6? Sasa mkuu kweli kwenye milioni 27 umpe 6 tu? Hapana usimuonee shemeji yetu. Utampa angalau 8-10. Tuseme umempa 8. Unabakiwa na milioni 19.

Tenga milioni moja kama gharama za kufanyia window shopping. Unakuja kugundua biashara ya tyrr repair inahitaji mtaji mkubwa ili kufanya service ya uhakika. Unaamua utfungua duka la jumla la bidhaa za nyumbani. Basi unajikakamua unatoa milioni 15. Mbili zinabaki kama kodi. Hapo sasa roho yako kwatuuu. Unastarehe huku ukila pensheni ya biashara yako.

Mtume, kumbe nyumba iko kwenye hifadhi ya barabara. Unatakiwa kuhama ndani ya mwezi mmoja. Yule uliyemuuzia kiwanja na nyumba amepauza milioni 500. Nawaza tu.
 
Hii analysis ya level nyingine kabisa. Basi nemeacha mkuu, siuzi tena! 😀😀😀😀
 
kuna watu wa ajabu kweli hii dunia,...unamshirikisha wife kwenye mambo yako,?🤔🤔❗ yani hapo wife alitakiwa aambiwe hapa tunaondoka na anaondoka bila kuuliza,... mwanamke atakushauri nn?📍📌 hayo ndo madhara ya kumuona mke ni mwenzako,....🚮
I want to laugh but we are solving family issue my grandmother is pregnant 😂😂. They might think am laughing at her
 
Kuna watu wakipata changamoto hukimbilia kuuza mali zao

Lakini bado wanashidwa kunyanyuka tena
Sababau mipango yao mipya inaweza kukutana na changamoto tena na wakashindwa kuitatua wala kuikwepa

Haya mambo ya ukipata changamoto , unaitatua kwa kuiza mali ni risk sana

Wakati mwingine changamoto huwa ni mindset yako..!
Kuwa makini
🎯🎯🎯🎯🎯🎯
 
Mkuu huna starehe yeyote, mfano kubeti,pombe,michepuko? Mbona Mimi nna wasiwasi na wewe? Maana mkeo ujue anakujua vizuri, kuuza sio shida ila mkeo anaona mkiuza safari ya kurudi kwao imewadia Kwa mapicha picha utakayo mfanyia, 😂😂😂

Kuuza sio shida, shida huwa inakuja baada ya kuzipata hizo 150m!

Na ndo maana shemela anakuwa anasitasita!
😀 😀 😀 😀 Mimi mwenyewe najijua vizuri mzee wa kulipuka na pesa. Ndio maana hizo hela mteja angelipa kwake mi ningechukua chache tu za mishe zangu. Pesa yoyote ikiingia sehemu kubwa huwa tunapanga wote matumizi. Zile za bata ndio hazionagi.
 
Basi ujue yeye ana hofu na wewe mtakapopata hizo Hela utabadilika!
 
Umesema kwamba kipato kimetetereka, kwanini Sasa msiuze nyumba , upeleke milioni 150M UTT, gawio lako Kwa mwezi 1.25M na zaidi hii pesa itakutosha wewe na familia Yako kupanga , kula , kuishi. Na bado 150M yenu itakuwepo palepale. Kuliko kugombana kwanini msifanye hivyo mnakuwa mnapata kipato huku pesa yenu haijapotea, kuchukua pesa kwenda kuanzisha mradi mpya unaweza angukia pua.
Una akili ww dah, sijui kwann uliwahi kuolewa😜
 
Mie naona mkeo ana akili kuliko wewe, samahani lakini, vuta miaka miwili ama minne ,unashangaa unapata wa kukupa 300-500M utashukuru wife ama unapata mchongo wa Mana zaidi unapata ugali. Unakuja uuza uzeeni kabisa huko kwa bilioni unatoa urithi kwa wanao na wewe unaoza vizuri huko Kijijini kwenu.
Kama huna hela unadhani
Acha mawazo ya first year huwezi fanikiwa jambo kama unaongopa kutake risk
 
Unapokeaje hela ya mauzo ya nyumba ukiwa nyumbani? hUNA MWANASHERIA huna lolote unauza nyumba kama unauza kijoti! Mkeo mwache wamwoe wanaojua akili ya fedha!
Mxxxxxiiiie!
 
Huyo ndio anafaa kuwa mke sasa, sio wale wa ndio Mzee ndio Mzee😂😂😂.

Hiyo M80 unaiona nyingi kwa kuitaja ila ikiingia mkononi mwako kama utakua huna plan nzuri itapotea kinamna ya ajabu hadi ushindwe kuamini ni nini kimetokea.

Ingawa watu husema kimfaacho mtu chake ila mkeo nae atakua anahoja ya msingi, so kaeni tena chini muongee kwa maana kitendo cha kusema mjipe miaka miwili ya kujiuliza hii inaonesha bado anaamini unaweza ukapata vyanzo vingine vya utafutaji ndani ya muda huo.

Na kingine kama wewe ndio ulikua mchezaji wa hiyo team basi inabidi na yeye aingie ndani ili muwe mnacheza wote kwa maana yeye akienda kulia nenda kushoto jioni muweke vitu mezani.

NB: kwenye maisha ya utafutaji hautakiwi kujiona unayo plan B kwa maana itakurudisha nyuma kinamna fulani katika harakati zako na hufanya hata akili isione chochote zaidi ya hiyo plan B iliyopo, jiulize kama usingekua na hiyo nyumba unhewaza kufanya nini sasa hivi?

Njia zilizokua zinakupatia pesa hadi ukanunua kiwanja na kujenga hiyo nyumba sasa hivi zimegoma kiasi cha kufanya utamani kuuza hiyo nyumba ili uwekeze sehemu nyingine, unauhakika baada ya kufanya hivyo pesa itaanza kupatikana tena?

Pesa ni zawadi lakini pia pesa ni roho, ukipita kwenye njia zake utaikamata ila ukiwa mbali na njia zake utapishana nayo, yawezekana wewe unahisi shida yako ni mtaji lakini kumbe wala hiyo sio shida yako.

Ndio maana unaweza ukapata huo mtaji ila bado ukaendelea kuteseka na kuchanganyikiwa kisa biashara haiendi ila hasara tu ndio zinazoongozana.

Sasa tumia huo muda ambao mkeo amekupa ili muweze kujiuliza kwa pamoja.
Bro umetisha jamaa anatakiwa afate huu ushauri
 
Back
Top Bottom