Niongee na
Mokiti na
Kisai hivi kuna mmoja wenu amewahi kujifunza kuhusu fractal Geometry? Nataka kutumia analojia yake kuonesha asili ya mnachobishania
View attachment 2231811
Ukitazama ki sura na umbo hako kajani kamoja pembeni kanafanana kabisa na katawi kote kalivyokaa.
Kutokana na Yesu kuwa Mwana wa Mungu basi amezibeba sifa zile za Mungu ndio maana kuna baadhi ya watu wanashindwa kutofautisha vizuri.
Kitawi kikisema kwa seli mimi ndio ninawapa, maji, chakula na uhai, hata kijani pia kwa seli ndicho kinawapa maji, chakula na uhai wao! Umeona?
Kwa analojia seli zilizopo katika kajani kamoja zinaona hako kajani kama ndio kila kitu kwake na zinakatumikia. Ila kwa kutumikia hako kajani ndio hivyo zinalitumikia tawi zima na kuutumikia mmea mzima na mmea mzima ni mapenzi yake kabisa seli zitumikiane na kuzitambua mamlaka zilizo juu yake. Kajani na kitawi ni mmoja ila kuna kajani na kuna kitawi. Kajani[mwana] ndio njia pekee ya kuelekea kwa tawi zima[baba]. Jani na tawi hata siku moja havipingani ki matakwa ni 'kitu kimoja'
Sasa kwa kuwa seli ni ndogo sana kajani kwake kanaonekana ni kitu kuuubwa sana[infinity] kiasi kwamba wakiambiwa kuna tawi kubwa zaidi[infinity infinity] wanakubali na wanaelewa. By the way for all intents and purpose wakimuangalia jani wanapata sura halisi ya tawi na mmea ulivyo kisifa wanazoweza kuzielewa wao finite cells.
Kwa hiyo kwa level yetu ndogondogo ndogo sana Yesu ni Mungu[infinity] hamna kitu hakipo chini yake katika ulimwengu huu. Lakini sasa huyo Yesu yumo ndani ya Mungu tena infinity,infinity,infinity. Sisi tulio wadogo hatutenganishi kiuelewa infinity yoyote ile. Na we can do just fine hata tukiishia kuelewa level yetu mradi tufanye kitu ambacho kina uelekeo mwema kwa seli, mwema kwa kijani, mwema kwa kitawi na mmea mzima!