Mimi ni Muislam kwa baba na mama na hatuna historia ya dini nyingine labda huko nyuma kabisa ambapo hata bibi zangu hawakuwepo au hawajui, imetokea mimi tu kuupenda ukiristo kiasi ambacho tangu niko form one miaka zaidi ya ishirini kubadili majina yangu na kuwa ya Kikiristo na nilikua nikisema baba yangu mkristo mama yangu ndiyo Muislam.
Bahati mbaya nikiwa form two nilikaa hostel ya waroma kwahivyo nilikuwa napenda wakati mwingine kwenda kanisani japo nilikua sielewi kitu, kuna wakati napotezea naanza kusali kiislam kwasababu dini ya Kiislam naijua nimesoma madrasa nikiwa mdogo na hakuna kitabu cha dini kina kina kinanishinda kusoma na hapo zamani nilikua nikisia mtu anasoma kuruan nalia bila kujua nalilia nini nikawa namwambia mama mbona nie nalia nikiona au kusikia kuruan inasomwa? Mama ananiambia tu inaitwa midadi hiyo.
Nimejikuta tu wanangu sijawapeleka madrasa na shule nimewapeleka shule za kikiristo na sipendi kabisa za kiislam wala madrasa na huwa nawaambia wanangu nendeni kanisani, na utu uzima huu kuna wakati nilipata majanga makubwa nikaona njia sahihi ni kuombewa kanisani nikaenda roma kuombewa ndani ya siku tatu pepo likatoka na nimeendelea kusali kiroma nikiwa nyumbani na natumia maji ya baraka wakati mwingi nahisi kabisa yananisaidia, halafu nikiwa kanisani nina amani zote nachokisema nakielewa nachokisali nakielewa! Naona mahubiri ya father nayaelewa vizuri na hapa nyumbani redio nasikiliza redio Maria tu na naifurahia.
Sasa wakuu nisaidieni hili ni pepo au nini? Je nibadili dini na utu uzima huu? Au nifanyaje nifute historia hii? Yaan sasa hivi ndiyo nazidi kuzama kwenye ukristo kiasi ambacho hata wanangu natamani waanze mafundisho, au kuna sehemu sijielewi?
ni pepo, limetoka kwenye nyumba A likahamia kwenye nyumba B. why nasema hivi? hiyo dini yako ya kwanza ni upotofu, sio ya kweli na haitakufikisha mbinguni, itakupeleka moja kwa moja motoni. pia, hiyo ya roma na maji ya baraka sijui nini nini maria sijui nini, hiyo pia ni shortcut nyingine ya kukupeleka motoni moja kwa moja.
USHAURI WA BURE: uuchukue au usiuchukue ni juu yako. unatakiwa kuokoka na kusali na watu waliookoka ili wakusaidie kuishi maisha ya wokovu (ndege wanaofanana huruka pamoja). inaweza kuwa ngumu kwako, lakini jaribu tu hata hapo nyumbani kwako, uwe na desturi ya kusoma Biblia na kutafakari maneno yake, na mwisho wa siku uwe unaingia chumbani, ukiwa peke yako pametulia, elekeza mawazo yako kwa Mungu wa Ibrahim Isak ana Yakobo (Mungu uliyemsoma kwenye Biblia), mwombe/ongea naye chochote, fanya hivyo mara kwa mara ila useme " kwa kupitia JIna la Yesu Kristo wa Nazareth", utaona badiliko na utaujua ukweli.
hayo yote yatafanyika kiusahihi ukiungamanishwa naye kwa kumkiri Yesu Kristo kwa kinywa chako kuwa ndiye Bwana na Mwokozi wa maisha yako kuanzia sasa, na kuamini moyoni kwamba yeye ndiye huyo Mungu alimtoa kafara kwa ajili ya dhambi zetu akafa na siku ya tatu akafufuka na yuko mbinguni. ni kwa JIna la Yesu tu Mungu anatutambua, hataki michanganyo mingine, hataki tumsogelee kwa mgongo wa manabii, au maria, Mungu anakutambua, anakuokoa na kukupokea kama utasogea kwake kwa Jina la Yesu Kristo tu.
kabla ya yote, tafuta kanisa lolote la watu waliookoka (sio hao wanaouza mafuta, maji, chumvi n.k), waliokoka. waambie wakuombee sala ya toba, utubu dhambi na ufanya hayo niliyokuelekeza hapo juu. utamwona Mungu. usipoteze muda wako kwenye uislam, wala kwenye ukatoliki au kwa manabii wa uongo hao masharobaro wa siku hizi. wapo walokole wengi tu hapahapa tanzania hata kama hao manabii wamekuja kuchafua kujifanya na wao walokole wakasababisha watu wadharau wokovu.
angalizo lingine, kimbia wafuasi wa Musa, wasabato. jana niliangalia tv yao moja hapahapa bongo, kuna mchungaji mmoja alikuwa anafundisha kwamba kunena kwa lugha sio lazima, na kama ikitokea hawatakiwi kunena zaidi ya watu watatu, na hutakiwi kuongea lugha usiyoijua. nilishangaa sana. nikajiuliza, Roho Mtakatifu kwao huwa analiaje "ABBA" na huwa anaombaje ndani yao, dini iliyoanzishwa na mwanamke freemason (imethibitishwa). Mungu akusaidie.